Papa Francisko amechagua Katibu Msaidizi wa Kitengo cha wa Tatu katika nafasi ya Kidiplomasia ya Vatican, Monsinyo Mauricio Rueda Beltz, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Mshauri wa Ubalozi wa Vatican nchini Ureno.
Kitengo cha Tatu katika Ofisi ya Katibu Vatican, kinashughulikia masuala tu yanayohusiana na watu wanaofanya kazi katika huduma ya kidiplomasia ya Vatican au ambao wanajiandaa kuingia na iliundwa kuonyesha umakini na ukaribu wa Papa na wakuu wa Sekretarieti ya Serikali kwa wafanyakazi wa kudumu wa kidiplomasia.
Aidha Papa Francisko amethibitisha tena nafasi ya Katibu kwa ajili ya uwakilishi wa Kipapa, Askofu Mkuu Jan Romeo Pawłowski, Askofu Mkuu wa Sejny.