Tafuta

Vatican News
2020.12.24 Misa ya mkesha wa Noeli 2020.12.24 Misa ya mkesha wa Noeli  (Vatican Media)

Papa hataongoza ibada ya mwisho na mwanzo wa mwaka kutokana na maumivu ya mguu

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa vyombo vya habari Vatican,Dk.Matteo Bruni amejulisha waandishi kuwa Papa hataweza kuadhimisha masifu ya jioni na kesho asubuhi kwa sababu ya maumivu ya mguu.Badala yake Te Deum itaongozwa na Kardinali Re na Misa Siku kuu ya Maria Mama wa Mungu itaongozwa na Kardinali Parolin.Sala ya Malaika wa Bwana itaongzwa na Papa kama ilivyopangwa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kufuatia na maumivu ya mguu ambao umelazimisha kupumzika, maadhimisho ya masifu ya kwanza ya jioni ,tarehe 31 Desemba 2020 na misa ya kesho asubuhi katika Altare ya Kanisa Kuu mjini Vatican, havitaongozwa na Baba Mtakatifu Francisko.  Ni kwa mujibu wa wa habari kutoka kwa msemaji wa vyombo vya habari Vatican, Dk. Matteo Bruni akiwambia waandishi wa habari.

Badala yake, Masifu ya kwanza ya jioni na wimbo wa Te Deum wa kumshukuru Mungu kumaliza mwaka 2020,  vitaongozwa na Kardinali Giovanni Battista Re, Dekano wa Baraza la Makardinali, wakati misa ya tarehe Mosi 2021 katika  siku kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu, sambamba na Siku ya Amani duniani  itaongozwa na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican.  Hata hivyo Kwa mujibu wa Msemaji wa vymbo vya habari Vatican amebainisha kuwa Papa Francisko, tarehe Mosi 2021, ataongoza sala ya Malaika wa Bwana akiwa katika Maktaba ya Jumba la Kitume kama ilivyopangwa.

.

 

31 December 2020, 12:37