Tafuta

Mti wa mapambo na Pango vimeangazwa na taa katika Uwanja wa Mtatifu Petro!

Ijumaa jioni tarehe 11 Desemba 2020 tukio la kuwasha taa katika mti wa mapambo na Pango kama utamaduni katika fursa ya Siku kuu za Kuzaliwa kwa Bwana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,Vatican limetendeka.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Tangu mwaka 1982 Mtakatifu Yohane Paulo II alianzisha tendo la kuzindua pango na kuwashwa kwa taa za mti katika uwanja wa Mtakatifu Petro. Na tangu wakati huo tukio hili limekuwa likisubiriwa sana na wadogo na wakubwa wa Roma pia hata watalii wengi na wanahija kutoka ulimwengu wote.

Mwaka huu kutokana na kanuni za kiafya ili kuweza kuzuia maambukizi zaidi ya Covid-19, wanahija na watalii hawakuweza kufika wengi kutokana na hali halisi, lakini hata hivyo sherehe hizo walio wengi wamefuatilia kwenye mtandao wa moja kwa moja kupitia vyombo vya habari Vatican, TV 2000 na Eurovisione.

UZINDUZI WA PANGO
UZINDUZI WA PANGO

Aliyeongoza sherehe hizo za kuwasha taa kwenye Mti na Pango ni Kardinali Giuseppe Bertello, Mwenyekiti wa Utawala wa Mji wa Vatican. Wakati wa kutoa neno amesema: “Pango hili linatufanya kuelewa kuwa Injili inaweza kuandaliwa kwa kila tamaduni na kwa kila shughuli. Inakuwa kituo cha kufika na cha kuanzia kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Teramo,  ambalo wamejikita kwa kina katika safari ya kichungaji ya kufanya maandalizi. Mchakato huo pia umekwenda kukutana na nchi ya Slovenia ambamo Mti uliopambwa mjini Vatican umetokea huko na kufanya kana kwamba wanakuwa mapacha kiroho. Mti huo unatukumbusha uzuri wa ajabu wa Nchi ile na tamaduni zake”. Amesisitiza Kardinali Bertello. 

MTI WA MAPAMBO
MTI WA MAPAMBO
12 December 2020, 07:54