Tafuta

Miaka 84 ya kuzaliwa kwa Baba Mtakatifu!

Papa Francisko ametimiza miaka 84 ya kuzaliwa kwake akiwa na ulimwengu rohoni mwake.

Katika masaa haya, salamu na matashi mema ya kumtakia siku kuu njema ya kuzaliwa kwa Papa Francisko zinazidi  kuongezeka! Haya ni maonesho makubwa ya umakini na upendo kwa Papa kutoka kwa watu wa Mungu na katika mwaka ambao janga limeikumba Dunia na kuisimamisha kwa kiasi fulani. Video inayoonekana ni kama kuonesha Album ya picha nyingi zilizo nzuri na za kina, tabasamu, mikumbatio na ukaribu wa wakati uliopita na ambao utafikiri ni mbali kwa sababu ya kutaka kuona ulimwengu unakutana tena kwa haraka.

17 December 2020, 10:55