Tafuta

Vatican News
2020.03.19 Mtaktifu Yosefu 2020.03.19 Mtaktifu Yosefu 

Maelekezo ya msamaha wa dhambi katika Mwaka wa Mtakatifu Yosefu

Ibada ya Mlinzi wa Mwokozi imezidi kupanuka katika mchakato wa historia ya Kanisa na si tu katika kuchangia ibada kati ya zile kuu zilizopo baada ya ile ya Mama wa Mungu mchumba wake,lakini pia hata zile nyingi zinazohusiana na usimamizi.Katika mwaka Maalum wa Mtakatifu Yosefu,ipo fursa ya kupata msahama wa dhambi kwa maelekezo ya Idaya ya Kitume ya Toba

Leo ni miaka 150 tangu kutolewa kwa Hati ya Quemadmodum Deus, ambayo Mwenyeheri Pio IX, alisukumwa na hali halisi mbaya iliyokuwa inazingira Kanisa na watu na kutangaza Mtakatifu Yosefu kuwa Msimamizi wa Kanisa Katoliki. Katika lengo la  kumkabidhi Kanisa lote kwa Msimamizi wa Mlinzi wa Yesu, Papa Francisko ameamua kuwa siku ya leo katika maadhimisho ya kumbu kumbu ya  Hati hiyo katika siku Takatifu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili na mchumba wa  Yosefu, hadi tarehe 8 Desemba 2021, iadhimishwe ‘Mwaka Maalum wa Mtakatifu Yosefu’, na  ili kila mwaamini kwa kuongozwa na mfano wake anaweza kila siku kujitahidi katika maisha ya imani kutimiza mapenzi ya Mungu.

Ndivyo Kardinali Piacenza Mkuu wa Idara ya Toba ya Kitume anabainisha kuhusiana na Barua ya kitume ya ‘Patris corde’ ya Papa Francisko iliyochapichwa  tarehe 8 Desemba 2020 katika Siku kuu ya Bikira Maria mkingiwa dhambi ya Asili.  Katika barua hiyo Kardinali anasema kuwa, waamini watakuwa na uwezekano wa kufanya jitihada ya sala na matendo mema ili kwa mfano wa Mtakatifu Yosefu mkuu wa familia ya mbingu  ya Nazareth, kupata nguvu na faraja katika matatizo mengi ya kibinadamu na kijamii ambayo yanakatisha  ulimwengu wa sasa.

Ibada ya Mlinzi wa Mwokozi imezidi kupanuka katika mchakato wa historia ya Kanisa na si tu katika kuchangia ibada kati ya zile  kuu zilizopo baada ya ile ya Mama wa Mungu mchumba wake, lakini pia hata zile nyingi zinazo husiana na usimamizi. Mafundisho ya Kanisa yanaendelea kugundua yale ya zamani na mapya  ambayo ni ya thamani kama  Mtakatifu Yosefu msimamizi wa nyumba ya Injili ya Matayo na ambayo inaonesha wazi ile thamani kubwa ya maombi mapya na ya zamani ” (Mt 13,52).

Ni  muafaka wa mapendekezo zaidi katika zawadi ya msamaha wa huruma ambapo Idara ya Kitume kwa njia ya Hati iliyowekwa kwa ajili ya utashi wa Papa Francisko, itasaidia katika  mwaka wa Mtakatifu Yosefu. Kwa maana hiyo utatolewa msamaha wa dhamb na ambao kwa kawaida kabla ya kuupokea unahitaji kufanya yafuatayo:  sakramenti ya kitubio, komuni ya ekaristi, na sala kwa ajili ya nia za baba Mtakatifu, kwa waamini katika moyo wa kutubu kila aina ya dhambi hasa kwa wale ambao watashiriki Mwaka wa Mtakatifu Yosefu katika fursa na katika mtindo ambao unaelekezwa na Idara ya kitume.

08 December 2020, 12:05