Tafuta

Vatican News
Mabadiliko ya tabianchi Mabadiliko ya tabianchi 

Kard.Turkson:matarajio yetu yawe ni kwa ngazi zote kuhusu tabianchi!

Kwa nini mataifa makubwa au G20 zinapeana asilimia 50 zaidi za fedha za Covid-19 kwa ajili ya kununua kwa bei nafuu mafuta kuliko nishati safi? Serikali lazima zisitishe uwekezaji katika mafuta.Jamuiya maskini zinahitaji nishati ya kijani ya kisasa na endelevu hawataki kuendelea kunaswa yaliyopita kama ilivyotokea mara nyingi huko nyuma.Ni katika ujumbe wa Kardinali Turkison kwa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kardinali Turkson , Rais wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya binadamu katika fursa ya mwaka wa 5 tangu kutiwa saini  kwa Mkataba wa Paris na sherehe ya Mkutano wa  ngazi ya Juu wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika tarehe 12 Desamba 2020 ametoa ujumbe wake. Katika ujumbe huo Kardinali amesema ni mwaka wa 5 tangu kusaini Mkataba wa Paris na miaka mitano tangu kutangazwa wa Waraka wa Laudato si’, ambao kwa wastani ni  kilio cha dunia na kilio cha maskini (Laudato si', 49) na ambacho kinasikika kwa nguvu na dharura katika maskio yetu.

Janga la sasa lisiwe kizingizio cha majuku yaliyowekwa

Kardinali anandika kuwa janga tunalokabiliana nalo haliwezi kuwa kisingizio cha kutotenda kwa majukumu yaliywekwa, lakini lazima iwe  kama fursa ya kujijenga tena vizuri. Papa Francisko katika kuunda Kamati ya Vatican kwa ajili ya Covid-19, Kardinali anaadika kuwa aliwataka wote kuunganisha nguvu na kuota ndoto ya kuandaa wakati ujao. Umefikia sasa wakati wa kutambua changamoto na matatizo ambayo hayakuangukia kwenye mawe. Upyaisho wa utamaduni wa kutunza na maono ya uchumi ambao unatafuta wema wa pamoja unaosimamizia juu ya mshikamano na juu ya utunzaji wa mazingira, ushirikishwaji, usawa na haki, vinaweza kuhamasisha mabadiliko ambayo yanabadilisha na kufanya binadamu aondokane na mgogoro huu.

Malengo ya muda mrefu hayatatosha ikiwa tunalinda kikomo cha nyuzi 1.5

Kardinali Turkson amesema kuwa kuna haja zaidi ya kupendelea malengo ya dhati na matendo yanayoelekeza kupinguza hewa chafuzi kufikia mwaka 2030. Na “Malengo ya muda mrefu kufikia miaka 30 hadi 2050 hayatatosha ikiwa tunataka kulinda kikomo muhimu cha nyuzi 1.5 ° C. Tunatazama hasa bara la Ulaya, ambapo matumaini na uwajibikaji mpya wa kasi ni kuongezeka wakati huu na kuhakikisha kuwa inatoa sehemu nzuri jitihada za ulimwengu zinazohitajika. Kitu chochote kidogo kwa upande wa  Ulaya au wengine sio jibu la kutosha kwa sayansi, kwa wale wanaoteseka au kwa vijana ambao watarithi mafanikio na kushindwa  kwetu, amesisitza.  Kwa maana hiyo Kardinali anaongeza kwamba: “Makubaliano ya Paris ni mafanikio muhimu, yaliyo patikana kwa bidii, lakini hayataleta mabadiliko muhimu bila kuwa na mabadiliko makubwa ya siasa na sera kisiasa, lakini pia ya mioyo yetu, akili, mtindo wa maisha na njia tunazoishi  na tunavyokutana kama familia ya kibinadamu”.

Swali: nia gani waliyo nayo viongozi katika kuwa na matumizi mazuri?

Kardinali kwa maana hiyo anauliza viongozi wa kisiasa wana nia gani ya kuweka mawazo yao na hisia zao na wito wa kweli waliopokea kwa matumizi mazuri? Mungu ametupatia sayari hii na rasilimali zake tukufu, wanapofikiria ‘NDC1 yao, yaani ambayo ni “Mchango wa Kitaifa wa Kuamua”, kuwa  wasifikirie kuwa ni yao wenyewe, badala yake ni jinsi gani wanavyohakikisha ulinzi wa ustawi wa wote, ambao unapaswa kuzingatia wale ambao ni maskini na walio katika mazingira magumu zaidi.

Kiwango cha matumizi mazuri ya kujiinua kwa serikali ndiyo mstakabali wa miaka ijayo

Kiango ambacho serikali zitachagua namna ya kutumia fedha zao kwa ajili ya kujiinua kwa upya ndivyo itakuwa mstakabali wa makumi ya miaka ya wakati ujao. Hii ina maana lazima iwe na upendo na mshikamano kwa ajili ya kizazi kijacho. Kwa nini nchi za G20 zinapeana asilimia 50% zaidi za fedha za Covid-19 kwa  ajili ya kununua kwa bei  nafuu mafuta kuliko nishati safi? Serikali lazima zisitishe uwekezaji katika mafuta. Jamuiya maskini zinahitaji nishati ya kijani ya kisasa na endelevu; hawataki kuendelea kunaswa katika yaliyopita kama ilivyotokea mara nyingi huko nyuma.  Ahadi za msaada wa kifedha kwa nchi maskini ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kufuata njia mpya za maendeleo hazijatimiza matarajio na shida ya madeni ambayo imekandamiza maendeleo ya nchi nyingi zinazoendelea inatishia kuongezeka zaidi mara moja. Hakuna uendelevu bila usawa. Maskini kabisa kati yetu lazima wawekwe katikati ya mawazo yetu, sala zetu na sera zetu na mipango.

Sisi ni familia moja ya binadamu na kuishi katika dunia inayo tukaribisha

Kwa kuhitimisha ujumbe wake amesema kidogo kidogo tunakaribia mwisho wa mwaka huu ambao ni muhimu na wakati huo  tunaalikwa kujikumbusha kuwa sisi ni familia moja ya kibinadamu, na ambamo tunaweza kutegemeana tu kwa mmoja na mwingine wakati tukisadiana kutunza nyumba yetu ya pamoja dunia tunamoishi, kama watoto wa dunia moja ambayo inatukaribisha sisi sote, kila mmoja na utajiri wa imani yake au kila mmoja na sauti yake, wote ni ndugu (Fratelli tutti, 8).

12 December 2020, 18:22