Tafuta

2020.12.15 Kardinali Tagle 2020.12.15 Kardinali Tagle 

Kard.Tagle:Noeli wakati wa janga inaalika kuwa na mshikamano!

Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu ameshirikisha matumaini yake ya Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana na anatoa maneno ya kutia moyo kwa wale wote wanaoteseka kwa sababu ya Covid-19.

Sr. Angella.Rwezaula – Vatican.

Uchungu na matumaini ndizo tabia ambazo zinaonekaka katika sku za kwanza za maandalizi ya Kuzaliwa kwa Bwana. Mwaka 2020 unakaribia kumalizia ambao kwa hakika umekuwa ni wa mateso lakini pia jitihada za watu wengu ambao wameweza kuwasaidia wale wanaoteseka.  Ni katika maneno ya Kardinali Luis Antonio Tagle, Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, Pia arsia wa Caritas Inernationalis wakati wa mahojiano na Vatican News. Anazungumza hata katika nafasi yake ya uzoefu wa maambukizi ya Covid na kusisitiza umuhimu wa kuzaliwa kwa Bwana kama wakati wa matumaini na kuzaliwa kwa upya ubinadamu wote.

Kardinali  Tagle amewakumbusha umuhimu hasa wa kukumbuka  siku ya kwanza wakati Yesu alipozaliwa, kuwa hali haikuwa ya kawaida. Nchini Isareli hali ya maisha ilikuwa ni ngumu sana na katikati yao akazaliwa Mtoto wa Mungu. Kwa maana hiyo mawazo yake ni kwamba matatizo na mateso ya mwaka huu, yanaweza kusaidia hata  sisi kutafakari kwa ndani juu ya ujumbe wa matumaini ya Siku ya Kuzaliwa kwa Bwana. Je ni nini maana ya Kuzaliwa kwa Bwana? Maana yake ni Mungu aliye katikati yetu, amesisitiza Kardinali Tagle. Na kwamba "Hatutakuwa peke yetu kamwe, ikiwa Emanueli Mungu pamoja nasi akiwa katikati yetu", amesisitiza. “Na kwa hiyo vitu vingine ambavyo viko pamoja nasi vitatoweka: uwekezaji, mafanikio, zawadi, pesa zetu ... zitatoweka. Vitu hivi vyote ambavyo tumefananisha na Siku kuu ya kuzaliwa, vinaweza kutoweka. Lakini Yesu anayekuja kati yetu, Mungu pamoja nasi, atakaa nasi milele. Hili ndio tumaini letu” amesema Kardinali Tagle.

Akitoa neno kwa wale ambao wanateseka pia kuwa na hofu ya ugonjwa huu, Kardinali Tagle  amesema, awali ya yote anaweleza kwamba wanaye kaka yao ndani mwao ambaye anatambua kwa namna ya pekee duku duku za ndani, uchungu na hofu. “Ningependa kuwaambia na kila mtu ambaye atanisikiliza, kwamba tunaweza kushtushwa na kitu kama hicho, kwa maana hutarajii! Kwa hivyo, kama Injili inavyosema: ‘Hujuhi ni lini atakuja, lini Bwana atakuja, jitayarishe’.  Ninatumaini kuwa tunaweza kuishi kila wakati, kila siku ya maisha yetu, kwa amani na Mungu na kwa amani na jirani yetu. Tusiahirishe matendo mema ambayo tunaweza kufanya sasa,  na ishara ndogo, kwa kitendo rahisi cha ufadhili, kitendo kidogo cha haki, simu rahisi, tabasamu, kumbu kumbu, kwa sababu hatuwezi kuwa na nafasi nyingine ya kufanya”.

Kardinali Tagle akikumbusha juu ya msisitizo wa mara kwa mmara wa Papa Francisko kwa mwaka huu kwamba 'hakuna anayeweza kujiokoa mwenyewe' na ni nini wakristo wanaweza kutenda amesema: “ni vitu vingi. Siku zote nakumbuka jinsi Wakristo wabunifu kutoka sehemu tofauti na kutoka vizazi tofauti katika kusheherekea siku kuu; unapita kutoka nchi moja kwenda nyingine na unaona ubunifu wa Wakristo. Siku kuu ya mwaka huu 2020 katika janga hili inatualika kuwa na mshikamano. Ninatumaini tutakuwa wabunifu na kwamba tutaweza kupata njia, hasa katika kuwakumbusha ndugu zetu  kaka na dada kwamba wana rafiki ambaye wanaweza kumtegemea. Labda, badala ya kuokoa pesa  zangu binafsi kwa nini nisihifadhi kwa ajili ya jirani yangu ambaye hana chochote? Badala ya kuwa na karamu kubwa kwa ajili yangu tu na familia yangu binafsi, kwa nini siwezi kuagiza chakula kwa ajili ya mtu mwingine pia? Kuna njia nyingi ambazo watu wengi wanaweza kuelewa! Nina kaka, nina dada, nina rafiki”, Kardinali Tagle amefafanua.

Kwa kuhitimisha, Kardinali Tagle ameonesha shauku yake hasa kwa ì kuhitimisha mwaka 2020 akisema kwamba: “Ninatumaini kuwa watu waweze kuwa na nguvu, matumaini, imani na furaha ya kuufanya mwaka mpya uwe na mwanga zaidi. Hatuwezi kutarajia mambo ya nje yabadilike. Labda hawatabadilika. Lakini tunaweza kubadilisha mitazamo yetu na hii itafanya mwaka mpya uwe na mwangaza katika  matumaini yetu, mshikamano wetu, na furaha yetu”.

15 December 2020, 18:09