Tafuta

Vatican News

Vatican imechapisha mwongozo wa kuhamashisha umoja wa wakristo

Baraza la Kipapa la Umoja wa Kikristo limechapisha “Vademecum ya Kiekumene”, yaani mwongozo wa kiekumene ambao ni hati yenye utajiri unaoonesha matendo ya dhati kwa ajilli ya kuwapa msaada wa utume wa maaskofu katika kuhamasisha umoja wa Kikristo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ni wajibu na ulazima, sio nyongeza, katika shughuli ya hiari ya utoaji huduma ya mtu. Hicho ndichi kiwango kilichopo katika nafasi ya askofu,  yaan uwajibikaji wa kuhamasisha shughuli za kiekumene. Umakini huo na mawazo yapo katika Hati iliyotangazwa tarehe 4 Desemba  2020 ya Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo.  “Askofu na umoja wa Kikristo: Vadecum kiekumene”, ndilo jina la mchango uliofanyiwa kazi na Baraza hilo la Kipapa na kupitishwa na Papa, mwenyewe kwa makusudi ya kuwa msaada kwa kila mchungaji na jibu, ambalo limeelezwa na kuhamasishwa mara nyingi katika mikutano ya miaka michache iliyopita . Katika utume huu maalum wa kiekume iliokuwa umetangazwa na Papa Francisko katika barua yake wakati wa fursa ya maadhimisho ya miaka 25 ya Waraka wa Ut unum sint  (1995), yaani  ili wawe na umoja, mahali ambapo ni sasa ni matashi mema kwamba Hati  hiyo inaweza  kutia  moyo na kuongoza jitihada za maaskofu kuelekeaumoja kamili wa  mwili wote wa kikristo. Ni jitihada ambazo zinathibitishwa katika utangulizi wa Hati hiyo kwamba  ni kutazama Kanisa lote.

Changamoto kwa wakatoliki: Hati hiyo imegawanywa katika sehemu mbili, moja imejikita kuhamasisha uekumene na, nyingine kwa ajili ya uhusiano kati ya Wakristo na sehemu tofauti zinazohusiana na njia ambazo kwayo  inawezekana. Katika sehemu ya kwanza, utaftaji wa umoja unaoneshwa kama changamoto kwa Wakatoliki na askofu kama mtu wa mazungumzo na kuendeea kujitoa katika kuendeleza uekumene, anayehusika na mipango katika uwanja huu. Kwa kuongezea mitindo ya  malezi imeainishwa, katika meneo  ambayo yanaendelezwa, njia muhimu za kuihamasisha na dalili nyingine za vitendo, kama vile kuhakikisha kuwa katika seminari zote na katika vyuo vyote vya kitaalimungu kuna kozi ya lazima kuhusu uekumene  au nyaraka na nyenzo kuhusiana na  mada hii  ziweze kusambazwa kupitia tovuti ya za majimbo.

Kuwa tayari katika hatua ya kwanza: Sehemu ya pili inafafanua harakati za kiekumene kama moja na isiyogawanyika japokuwa na aina tofauti kulingana na vipimo tofauti vya maisha ya Kanisa. Hati hii inazungumzia juu ya umoja wa kiroho na kwa maana hiyo, kati ya mambo mengine, ni hitaji la kusali  na Wakristo wengine na kushirikishana  wakati, siku kuu na nyakati za kiliturujia, shukrani kwa  kuwa na kalenda ya pamoja  ambayo inaweza kuruhusu Wakristo kujiandaa pamoja kwa ajili ya kusherehekea sikukuu muhimu zaidi pamoja. Katika hati hiyo pia ni  juu ya mazungumzo ya upendo au kwa maana nyingine hisani na kuchochea utamaduni wa kukutana ambao Wakatoliki, wanahimizwa, kwamba hawatakiwi kusubiri Wakristo wengine kuwa karibu nao badala yake ni  wao wawe tayari  kila wakati kufanya hatua wakiwa wa kwanza. Mkutano wa kichungaji, utume  na katekesi, kushiriki maisha ya sakramenti, baadaye  kufikia kwenye umoja wa vitendo  ambayo ni ushirikiano kati ya Wakristo, kwa mfano katika kulinda maisha au katika vita dhidi ya ubaguzi na umoja wa kiutamaduni.

Katika mahojiano yake na Vatican news, Rais  wa Baraza la Kipapa la kuhamasisha umoja wa Kikristo Kardinali Kurt Koch, amezungumzia namna ya ya kutumia  wa Hati hiyo na kwamba  imezaliwa kutokana  na maombi ya wajumbe wa Baraza hilo kunako mwaka 2016. Kulikuwa na hisia  za ulazima wa kuwa na Hati fupi yenye kuwatia moyo, kuwasaidia na kuwaongoza maaskofu katoliki katika huduma yao ya kuhamasisha umoja. Na zaidi kuchapishwa kwa Hati ya kiekumene ilikuwa ni katika fursa ya kuadhimsha mwaka wa 50 tangu kutangazwa wa Waraka wa Ut unum sint, na miaka 60 tangu kuundwa wa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Umoja wa Kikristo. Akifafanua kwanini hati hiyo inalenga  hasa maaskofu  Kardinali amesema kuwa majimbu ya Maaskofu katika kuhamasisha Umoja wa Kikristo amesema huko  wazi hasa katika dhihirisho la  Sheria za Kanisa. Jitihada ya Kiekumene ya Askofu sio chaguo katika huduma yake bali ni wajibu na ulazima.

Kardinali Kuch a amefafanua mchakato wa maandalizi ya Hati hiuo kwamba imedumu kwa miaka mitatu. “Utayarishaji wa Vademecum ya Kiekumene ilidumu kama miaka mitatu. Rasimu ya kwanza iliandaliwa na maafisa wa Baraza hili la Kipapa na  baadaye  kuwasilishwa wakati wa mkutano mwa mwaka wa Baraza mnamo 2018. Nakala hiyo baadaye ilitumwa kwa Mabaraza ya Kipapa Roma”. Hatimaye, Baba Mtakatifu aliidhinisha Vademecum, yaani Hati hii akiifafanua kama kutia moyo  na mwongozo katika utekelezaji wa majukumu ya kiekumene ya Maaskofu. Vademecum  hii msingi wake ni kutoka katika Mwongozo wa Kiekumene wa  mwaka 1993. Japokuwa, haikuwa suala  la kurudia Hati hiyo na  badala yake  kupendekeza kwa  ufupi,  kusasishwa  na kutajirishwa na mada zilizofuatwa wakati wa hati za mwisho, na kila wakati ilikuwa ni kupitisha maoni ya Askofu; na kwa maana hiyo ni  mwongozo ambao unaweza kukuza uhamasishwaji wa  hatua za kiekumene, amesisitiza.

Vile vile Kardinali amesema kwamba mantiki ya Vademecum inasisitiza hasa umuhimu wa Maandiko Matakatifu, ya umoja wa watakatifu na umoja wa damu, na utakaso wa kumbukumbu. “ Hii Hati inaelezea mazungumzo ya  upendo au hisani, ambayo inahusika na kuhamasisha utamaduni wa kukutana katika kiwango cha mawasiliano ya kila siku na ushirikiano. Mazungumzo ya ukweli yanafuata na  ambayo yanahusu mazungumzo ya kitaalimungu na Wakristo wengine. Hatimaye kuna mazungumzo ya maisha. Kwa usemi huo  tunachagua fursa za kubadilishana na kushirikiana na Wakristo wengine katika nyanja kuu tatu: utunzaji wa kichungaji, ushuhuda kwa ulimwengu na utamaduni”.

Hati hiyo aidha amesema “siyo tu kukumbusha misingi ya jitihada za kiekumene za Askofu, lakini pia inaorodhesha mambo mengi ya kufanyiwa mazoezi na  ambayo inafupisha, kwa maneno rahisi  moja kwa moja majukumu na mipango ambayo Askofu anaweza kukuza katika ngazi ya jimbo na  kikanda . Hatimaye  katika utangulizi, inatoa maelezo mafupi juu ya washirika wa Kanisa Katoliki katika mazungumzoya kitaalimungu kimataifa na masuala makuu yaliyokabiliwa.

Hatimaye Kardinali amesema  Papa Francisko mara nyingi husisitiza kwamba umoja unapatikana kwa njia ya kutembea  yaani ikiwa tutatembea pamoja na Kristo, yeye mwenyewe ataleta umoja. Na kwamba Umoja hautakuja kama muujiza kwani umoja unakuja njiani, kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye anafanya hivyo wakati wa  safari” (Kanisa kuu la Mtakatifu Paulo, 25 Januari 2014). Kwa maana hiyo “Ninatumaini kuwa Vademecum hii, ambayo  maana yake ni "njoo nami", inaweza kuwa msaada katika safari ya Maaskofu na ya Kanisa  lote Katoliki  kuelekea katika umoja  kamili ambao Bwana aliuombea”.

04 December 2020, 17:40