Tafuta

Vatican News
2015.07.12 Papa Francisko akimsalimia mzee mmoja wakati wa ziara ya kipapa nchini Ecuador, Bolivia  na Paraguay. 2015.07.12 Papa Francisko akimsalimia mzee mmoja wakati wa ziara ya kipapa nchini Ecuador, Bolivia na Paraguay. 

Kard.Czerny:umuhimu wa umoja ni kujenga utambulisho wa kikanisa!

Katika makala iliyochapishwa tarehe 31 Desemba katika gazeti la “La Civiltà Cattolica”,tunaonesha kwa ufupi mawazo ya Katibu wa Kitengo cha Wahamiaji na wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani akikabiliana na mada ya umoja ndani ya Kanisa na huduma ya kichungaji ya Papa Francisko.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Katika makala yake Kardinali Michael Czerny, Karibu msaidizi wa Kitengo cha Wahamiaji na wakimbizi cha Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya binaadamu, iliyotangazwa kwenye Gazeti la “La Civiltà Cattolica” tarehe 31 Desemba 2020 anasisitizia umoja kuwa ni tabia ya msingi ya utambulisho wa Kanisa. Umoja ni mtindo ambao Kanisa linajiwekea katika uwajibishaji wa wajumbe wake wot na ambao unathamanisha karama na huduma, wakati huo huo, uongeza zaidi mahusiano ya upendo kidugu, anaandika Kardinali Czerny. Katika maana hiyo kwa hakika na unapata nafasi katika “Hati ya Mtaguso wa II wa Vatican wa  “Lumen Gentium”, yaani mwana wa mataifa   ambao unabinisha wazi umuhimu wa walei katika maisha ya Kanisa.

Walei wanaaalikwa kushirikia katika shughuli zao kwa mujibu wa kazi, nafasi na mtindo wao wenyewe  huku wakishiriki katika maisha ya Kanisa. Lakini sio hiyo tu  kwani  ujumuishwaji unaorudisha kutazama hasa, zoezi la huduma ya maaskofu, umoja unakuwa mpana zaidi kwa kile ambacho kinatakiwa katika ushiriki na  kuwahusisha watu wote wa Mungu katika maisha na katika utume wa Kanisa. Hii ndiyo maana ambayo Papa Francisko anaipatina neno la  “Sinodi” au, sio ile ya muundo wa kanisa tu, lakini pia ya aina inayoonekana muugano, ya njia ya udugu wa kikanisa ambao wote waliobatizwa wanashiriki na kuchangia kibinafsi.

Umoja huu ni njia ambayo Mungu anatarajia kutoka kwa Kanisa lake la milenia ya tatu, anaandika Kardinali na kutaja  maneno ya Papa Francisko anayosema kwamba  ni Kanisa moja ambalo linakuwa kama piramidi iliyogeuzwa, na inaleta maeleano na kila upande na kila kitu kinachohusishwa, ikiwa na maana  watu wa Mungu, Baraza la Maaskofu  na Mfuasi wa mtakatifu  Petro. Hata hivyo mantiki hii inaelezwa vile vile vizuri katika Wosi wa wa Kitume wa “Evangelii gaudium”, mahali ambapo umoja umeelekezwa kama sharti la lazima kwa kulipatia Kanisa msukumo mpya wa umisionari. Kutoka kwa walei, Kanisa hasa, lina mengi ya kujifunza, kwa mfano katika maeneo ya uchamungu au ibada za  wa watu, kujitoa kwa  ajili ya shughuli za kawaidia za kichungaji, katika ustadi wa kiutamaduni na kuishi pamoja kijamii. Na zaidi kama alivyosema Mtakatifu John Henry Newman  kuwa: Kanisa lingekuwa kichekesho bila kuwa nao”. Kwa hakika vizingiti havikosekani, anabainisha Cardinale Czerny, huku akionesha ukosefu wa mafunzo ya kutosha na tabia ya mawazo ya makasisi ambayo huwaweka waamini walei katika jukumu la chini”.

Kukutana na maskini, ni fursa ya kuacha unjilishwe na Kristo. Kwa maana mantiki hiyo Kardinali anashauri hata utunzaji wa kazi ya uumbaji, nyumba yetu ya pamoja, katika mazingira na umakini zaidi kwa maaskini ambao wanafungamanishwa, kwani kila kitu kimeunganishwa, kwa mujibu wa Waraka wa pili wa Papa Francisko wa  “Laudato si’  unahusu utunzaji bora wa mazingira nyumba yetu ya pamoja. Je ni jinsi gani ya kufanya ili umoja uweze kukua katika Kanisa? Kardinali anashauri michakato ya uongofu kwa kukazia juu ya muungano jumuishi, ambao unawajumuisha watu wote wa Mungu na zaidi maskini. Bila ukarimu wa kukaribishana, kiukweli miundo ya kikaninisa haiwezi kuzaa  umoja, na inaweza kuonesha haitoshi katika kufikia mwisho au hatima  tulioombwa kwa ajili hiyo.

Sehemu ya mwisho, ya makala ya Kardinali Czerny amesisitiza kuhusu mtindo wa utoaji huduma wa Papa Francisko, anasema kwamba “Papa hana mawazo yaliyopangwa tayari kutumika kiukweli, wala mpango wa kiitikadi wa mageuzi kama  ‘prêt-à-porter’, yaani( tayari kutumika au kupelekwa) zaidi ya kufanya mikakati iliyoundwa mezani ili kupata matokeo bora ya takwimu. Badala yake, Papa anaendelea juu ya msingi wa uzoefu wa kiroho na maombi, ambayo anashirikisha katika mazungumzo, mashauriano, katika jibu thabiti kwa hali za udhaifu, mateso na ukosefu wa haki. Kutokana na  hii inafuata kwamba jitihada zilizo kipaumbele na kigezo cha kila hatua ya kijamii ya watu wa Mungu ni kusikiliza kilio cha maskini na cha dunia na kukumbusha kanuni msingi za mafundisho jamii ya Kanisa ambamo miongoni mwake ni pamoja na heshima ya kibinadamu isiyoweza kutengwa, hatima ya mali ya ulimwengu wote na ubora wa mshikamano, mazungumzo yanayolenga amani na utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja.”

31 December 2020, 16:22