Tafuta

Vatican News

Kard. Braz de Aviz:Covid haikusimamisha jitihada za watawa!

Katika mahojiano na Rais wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Vyama vya Kitume,amebainisha juu ya kujitoa na sadaka ya watawa wengi katika mwaka ambao unakaribia kuhitimishwa.Watawa hawakwenda mbali na watu wao na Injili ndivyo inavyoagiza kutenda.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Kwa mujibu wa maoni yake Kardinali João Braz de Aviz, Rais wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Vyama vya Kitume amesema moya ya picha yam waka 2020 ambayo kwa kiasi kikubwa itabaki katika kumbu kumbu yake ni juhudi ya watawa katika kujitoa kwa ajili ya utume wao licha ya matatizo ya janga ambao limeleta ugumu wakati kwa wtoe , lakini daima wamejikitia kukaa karibu na watu.

Karidnali hafichi kuelezea ni kwa njisi gani, watawa wa kike na kiume , hawakuweza kwenda mbali na wapendwa wao, kutoka katika vituo vyao vya kitume badala yake wameendelea mbele. Wengi wameambukizwa na Covis na wengine wamekabiliana na matatizo makubwa hata hatri kwa kufanya kazi katika hospital ina vituo vya huduma ya umma lakini pia hata katika nyumba na kupeleka mbele maisha haya kwa kushuhudia ukaribu kwa watu. Kwa kutoa mfano mmoja, anasema alishangazwa na mtoto mdogo nchini Italia ambaye alikwenda kumsalimia bibi yake kupitia kwenye vioo, kwa sababu, madaktari walitambua kuwa kulikuwa na  ulazima wa kuwa na uhusiano, joto la kifamilia kwa sababu ni upweke ulikuwa unaongezea hali kuwa mbaya.

Na“ndiyo hivyo tunaona sura ya watawa wetu wa Kike na kiume. Sisis tumeumbwa kwa ajili hiyo na Injili inatuomba tufanye kuwa mstari mbele katika utume”. Amesema Kardinali na kuongeza kwamba kwa upande wake, mwaka huu, umekuwa shule ya ukaribu kwa watawa wote wa kuendelea katika utume wao katika nafasi nyingi, huku wakitunza sehemu zao, na kama Papa Francisko anavyofanya akijikita kwenye matendo ya hatua zote za kisheria ambazo Mamlaka ya umma inaagiza. Karidinali Braz de Avis amesema kwa sababu hii ni muhimu kushinda hali hii, lakini wakati huo huo kutowaacha watu katika upweke na kutelekezwa, kwa kuwa na hisia kwamba hakuna mtu yeyote kwao anaye wajali na kwa sababu labda  ya kuwa huo ndio ugonjwa mbaya zaidi. Kwa maana hiyo Kardinali amesema kwake yeye hiyo imekuwa mwaka wa shule kuu.

15 December 2020, 17:32