Tafuta

2020.12.04  Pia ni baadhi ya Wakuu wa mabaraza ya Kipapa Vatican:Kard. Sandri, Tagle,Koch na Quellet 2020.12.04 Pia ni baadhi ya Wakuu wa mabaraza ya Kipapa Vatican:Kard. Sandri, Tagle,Koch na Quellet 

Hati ya Kiekumene ni mwongozo mzuri wa hatua ya matendo ya huduma!

Katika mkutano na vyombo vya habari Vatican katika fursa ya uwakilishi wa mwongozo wa kiekuenea:"Askofu na umoja wa Kikristo" wamezungumza Makardinali Koch,Ouellet,Tagle na Sandri.Wameangazia mshikamano mkubwa kati ya Wakristo pia wakati wa wimbi la uhamiaji,mazungumzo kama njia ya uinjilishaji na mchango wa uamuzi wa Makanisa Katoliki kwa Ibada ya Mashariki.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ni Dira ya kusaidia maaskofu katika safari ya kiekumene na kuwahimiza kufuata njia hii, ambayo ni ya Kanisa lote Katoliki kuelekea muungano kamili. Amesema hayo Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Kikristo akipiga picha halisi kuhusiana na Hati iliyotolewa tarehe 4 Desemba na baraza lake  inaoongozwa na mada "Maaskofu na Umoja wa Wakristo Vadecum ya Kiekumene" , wakati wa kuwasilishwa kwa waandishi wa habari mjini Vatican. Ni mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao ambapo Kardinali alikuwa na wengine watatu: Kardinali  Marc Ouellet, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maaskofu, Kardinali Luis Antonio G. Tagle, Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na Kardinali Leonardo Sandri, Rais wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki.

Kwa hakika uwepo wa Wakuu hawa makardinali wanne wa baadhi ya mabaraza ya Kipapa,  tayari unaonesha umuhimu wa Hati hiyo ambayo kwa mujibu wa rais wa Baraza la Kipapa la Umoja wa Kikristo,  Kardinali Koch amesema ni kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Baraza hilo kwa utashi wa Mtakatifu Yohane XXIII, mnamo 1960. Hati ambayo inapendekeza muhtasari mfupi wa nguzo za mchakato katika njia hiyo hiyo  tangu kutoka kwa "Unitatis Redintegratio wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican  yaani “kurudisha Umoja” ni hati ya Kanisa Katoliki kuhusu uekumene iliyotangazwa  mnamo Novemba 21, 1964 na Papa Paul VI. Hadi “Ut Unum Sint” yaani ‘ili wawe kitu kimoja’, Maneno yaliyochukuliwa kutoka katika sala ya kikuhani ya Yesu, katika Injili ya Yohana; waraka uliochapishwa na Papa Yohane Paulo II mnamo tarehe 25 Mei 1995, umeendelea kushughulika na masuala ya umoja hasa uhusiano kati ya Kanisa katoliki na makanisa mengine ya Kikristo. Waraka huu kwa maana hiyo unatimiza miaka 25 baada ya kuchapishwa kwake, hadi kufikia hati mbili za Baraza la Kipapa kuhusu “Mwongozi wa Kiekumene na  masuala makuu ya kiekumene katika malezi ya wale wanaojitoa katika huduma ya kichungaji.  Ni ufupisho ambao unatajirisha mada zilizopelekwa mbele katika mchakato wa safari ya miaka ya mwisho na kila wakati kupitisha maoni ya askofu. Ni mwongozo ambao ni rahisi kushauriana, pia utajiri na mapendekezo kwa vitendo.

Katika uwakilishi wa Vadecum ya Kiekumene au mwongozo wa kiekumene ambao unajitikia katika jitihada kwa ajili ya umoja wa Kikristo siyo chaguo kwa maaskofu na ambao wanaalikwa tayari katika Sheria ya Kanisa na hata Hati nyingine za kipapa kufanya hivyo kwa maana ya uwajibu wao katika mchakato wao mzima wa shughuli za kichungaji. Kiukweli umoja wa kikristo unaweza kutimizwa  kwa sababu uekumene hautoi ahadi  bali ni kutekelezwa.  Mwongozo mpya wa kiekumene unaoongazwa na mada Askofu na Umoja wa Wakristo, uliochapishwa na Baraza la Kipapa la Umoja wa Kristoa . Ni hati ambayo ipo chini ya uongozi wa maaskofu kujikita katia matendo na juu ya ushirikishano wa Sakramenti ambayo haiwezi kukosekana kwa kile kiitwacho kuhurumia. Ni mada nyeti hasa kwa kuzingatia msukumo uliomo wa kuweza kuungana pamoja.

Mwongozo huo huo ni ufupisho  ambao umegawanywa katika sehemu mbili zenye mantiki 42 , ikiwa na utangulizi ambao unatoa ufupisho wa hati hiyo ya pamoja na ambayo imefuata vipindi mbali mbali vya kiekumene na muhimu kuonesha namna ya kujikita katika  matendo ya dhati hasa  kuwasaidia maaskofu waweze kuendeleza shughuli zao katika harakati za kiekumene, mazungumzo na kuhamasisha sala na shughuli mbali mbali na makanisa mengine ya kikristo. Jambo msingi ni katika sehemu ambayo inajikita kufanua uekumene wa kichungaji mahali ambao kuna mada ya kushirikishana sakramenti. Kwa sababu Sala ya pamoja ituwezesha  kufikia umoja na Bwana wetu  alio utamani na kufikiria kwa ajili ya Kanisa lake, na wakati masuala ya kuendesha na kupokea sakramenti ya ekaristi, maadhimisho ya liturujia ya pamoja na wengine wananabaki kuwa mivutano katika uhusiano wetu. Kwa mfano halisi Kardinali amesema watu wengine wanapowaona wakristo waliobatizwa wanakosa umoja na mara nyingi hata kuonesha migongano ni jambo la kushangaza…..

Kwa upande wa Kardinali Leonardo Sandri, Rais wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki amebainisha kuwa katika Vadecum, inakumbusha kuwa haiwezekani kudharau Mwelekeo wa kikristo, utambuzi msingi kwa ajili ya kupata jibu la kikristo na matarajio ya wanaume na wanawake wa nyakati zetu. Hata hivyo katika swali kuhusiana na mazungumzo na Waangiliana na kuhusu kukubaliwa kuwekwa wakfu wa kikuhani kwa waanglikani, Kardinali Kurt Koch amesisitiza kuwa juu ya mada hiyo bado kuna kazi ya kufanya, kwa sababu Umoja wa kiangliani hivi karibuni wamekubali hata kuwekwa wakfu wanawake maaskofu, suala hili haliwezi kukubaliwa katika Kanisa Katoliki, na ambalo tayari linaunda hata matatizo katika kushirikishana Altare.

05 December 2020, 15:34