Tafuta

Harufu ya manukato:mwongozo wa tasaufi ya Shirika la Kaburi Takatifu

Duka la vitabu limechapisha kitabu kiitwacho“Nyumba yote ikajaa harufu ya manukato.Kwa ajili ya tasaufi ya Shirika la Kaburi Takatifu”.Toleo la kwanza la kitabu ambalo limeaandaliwa na Kardinali Fernando Filoni,Mkuu wa Shirika la Ulinzi wa Kaburi Takatifu Yerusalemu kwa ajili ya safari ya kiroho kwa ajili yake na Shirika zima.Katika kufafanua kitabu hicho amesema ni kwa anayetaka kusali kwa roho ya kuelekeza katika ardhi ya Yesu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko akikutana miaka miwili karibu iliyopita na wajumbe wa Shirika la ulinzi wa Kaburi Takatifu, alikuwa amewashauri wasisahau kwamba lengo msingi la Shirika lao linakua katika roho kwa wajumbe wake na kwa maana hiyo katika shughuli zote za mshikamano kuelekeza wakristo wa Nchi Takatifu na hawawezi kukosa kuwa na mipango madhubuti ya mafunzo ya kidini ambayo yanalenga kila mwanashirika na pia waweze kuwa na msimamo thabiti wa uhusiano na Bwana Yesu, hasa katika sala, katika tafakari ya Maandiko Matakatifu na kujikita kwa kina katika Mafundisho ya Kanisa.

Mwaliko huo ndiyo ulitoa msukumo kwa Kardinali Fernando Filoni, tangu tarehe 8 Desemba mwaka jana  kuanza  kuandaa na kutoa tunda hilo na zaidi katika kipindi cha karantini na kuendelea hadi kuwezesha kuandika kitabu chenye kurasa 88 chenye kichwa “Nyumba yote ikajaa harufu ya manukato. Kwa ajili ya tasaufi ya Shirika la Kaburi Takatifu”. Ni kitabu ambacho kimechapishwa tarehe 15 Desemba 2020 kwa lugha ya kiitaliano katika Duka la Vitabu Vatican na kuanzia 2021 kitakuwa tayari hata katika lugha nyingine, kikiwa kinataka kuwa msaada wa wanashirika 30,000 ili kuishi kila siku katika tasaufi ya mwanga wa maisha ya kifo cha ufufuko wa Kristo.

ARDHI YA YESU IBAKI KAMA MAWE YALIYO HAI

Katika kitabu chake, Kardinali Filoni anatafakari kuhusiana na mpango wa maisha, kuamini, thamani na chaguzi binafsi wa kiongozi huyo na shirika zima. Ni shirika lenyewe kwa kutoa umuhimu wa kwanza katika wito wa ukaribu wa wajumbe wake, anaandika katika utangulizi. Ni tamanio lake kwa kwamba kitabu kinaweza kuwa kifaa cha maendeleo na kujifunza katika maendeleo ya kiroho ya kila mmoja katika mazingira ambayo imani inakuwa uzoefu na kuyaishi yaliyomo ndani yake. Kwa kifupi kitabu hiki ni mwongozo ambao kwa mfano unaweka mikononi mwa washiriki wa Kaburi Takatifu ule uungwana.

Karidinali Filoni akifafanua anasema luwa suala hili sio tu kama heshima lakini ni chombo kinachofanya kazi na muhimu na majukumu na ahadi zilizopewa na Mapapa, kwamba manukato ambayo Maria wa Bethania alimpaka mafuta miguu yake Yesu na baadaye kumkausha kwa nywele zake. Hata hivyo Tukio la kiinjili, linaonesha kwa ufupi katika sanaa ya Padre Marko Ivan Rupnik  kwenye Kikanisa cha ‘Redemptoris Mater ‘kwenye Jumba la Kitume mchoro mzuri ambao umechaguliwa wa picha ya  kifuniko cha Kitabu kipya.

Kwa mujibu wa Kardinali Filoni aidha amesema, pendekezo kwa yule anayejiunga na Shirika hilo lina mwendelezo wa kazi ya Maria wa Bethania. Hiyo ni hali ya kujipaka hata sisi wenyewekama Mwili wa Kristo, ambao ni Kanisa ambalo Yesu anaishi sasa. Kanisa katika ukweli wake wa ulimwengu na wa mahalia lakini, hasa kama wanashirika,   kwa Mama Kanisa la Makanisa yote, lile la Yerusalemu na waamini wake, mahujaji, wakimbizi, maskini ambao Yesu alituachia. Amesisitiza Kardinali akizungumza na Vatican News.

15 December 2020, 16:57