Tafuta

Balozi Marija Efremova tarehe 19 Desemba 2020 amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Balozi Marija Efremova tarehe 19 Desemba 2020 amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. 

Balozi wa Macedonia ya Kaskazini Awasilisha Hati za Utambulisho

Balozi Marija Efremova, alizaliwa kunako tarehe 12 Oktoba 1960 huko Skopje. Ameolewa na kubahatika kupata mtoto mmoja. Kitaaluma ni mwanasheria aliyejipatia Shahada ya Uzamili kunako mwaka 2007. Amebahatika kufanya shughuli mbalimbali katika Mahakama hadi ilipotimu mwaka 1998 akateuliwa kuwa Katibu msaidizi, Jamhuri ya Watu wa Macedonia hadi mwaka 2000.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 19 Desemba 2020 amepokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mheshimiwa Marija Efremova, Balozi mpya wa Macedonia ya Kaskazini mjini Vatican. Balozi Marija Efremova, alizaliwa kunako tarehe 12 Oktoba 1960 huko Skopje. Ameolewa na kubahatika kupata mtoto mmoja. Kitaaluma ni mwanasheria aliyejipatia Shahada ya Uzamili kunako mwaka 2007. Amebahatika kufanya shughuli mbalimbali katika Mahakama hadi ilipotimu mwaka 1998 akateuliwa kuwa Katibu msaidizi, Jamhuri ya Watu wa Macedonia hadi mwaka 2000. Kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2002 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Sheria za Kimataifa, MAE. Mwaka 2002 hadi mwaka 2006 alikuwa ni Mshauri katika Ubalozi wa Macedonia nchini Italia.

Kati ya mwaka 2008 hadi mwaka 2012 aliteuliwa kuwa Balozi wa Macedonia nchini Uingereza. Na kati ya Mwaka 2009 hadi mwaka 2012 alikuwa ni Balozi wa Macedonia asiyekuwa mkazi nchini Ireland na Iceland na mwakilishi wa Macedonia katika Idara ya Elimu, MAE kati ya mwaka 2012 hadi mwaka 2013. Mwaka 2014 akaamua kuwa wakili huko mjini Skopje na hatimate kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa HBO, Chama cha Ushirikiano Kimataifa na Utamaduni wa Kidiplomasia, AICDC, chenye Makao yake makuu huko Trieste nchini Italia hadi mwaka 2018. Tarehe 19 Desemba 2020 amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko.

Macedonia ya Kaskazini
19 December 2020, 14:43