Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Philippe Abbo Chen, kuwa Askofu wa Vikarieti ya Mongo nchini Chad. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Philippe Abbo Chen, kuwa Askofu wa Vikarieti ya Mongo nchini Chad.  (ANSA)

Monsinyo Philippe Abbo Chen, Ateuliwa kuwa Askofu Jimbo la Mongo, Chad

Askofu mteule Philippe Abbo Chen alizaliwa tarehe 10 Mei 1962 huko Dadouar, Mongo. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 17 Mei 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Na mwaka 2001 akajiunga na Shirika la Watawa wa Bikira Maria na hatimaye, kuweza nadhiri zake za daima tarehe 14 Agosti 2009. Papa Francisko tarehe 14 Desemba 2020 akamteua kuwa Askofu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu Henri Coudray wa Vikarieti ya Mongo, nchini Chad la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Mheshimiwa sana Padre Philippe Abbo Chen, kuwa Askofu mpya wa Vikarieti ya Mongo. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Philippe Abbo Chen ambaye ni mtawa wa Shirika la Watawa wa Bikira Maria “Notre Dame de Vie Secular Institute” alikuwa ni Makamu wa Vikarieti ya Kitume ya Mongo.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Philippe Abbo Chen alizaliwa tarehe 10 Mei 1962 huko Dadouar, Mongo. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 17 Mei 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Na kunako mwaka 2001 akajiunga na Shirika la Watawa wa Bikira Maria na hatimaye, kuweza nadhiri zake za daima tarehe 14 Agosti 2009. Tangu wakati huo, kama Padre amewahi kuwa Paroko-usu, Mkurugenzi wa miito, Paroko, Mlezi wa maisha ya kiroho na msarifu wa Seminari kuu ya Falsafa ya St. Mbaga Tuzinde de Sarh kati ya mwaka 2010-2014. Kuanzia mwaka 2014 hadi 2019 aliteuliwa kuwa Makamu wa Askofu Vikarieti ya Mongo na Paroko wa Parokia Biktine. Kati ya Mwaka 2019-2020 “alijichimbia” mjini Venasque nchini Ufaransa kwa ajili ya tafakari ya kina kadiri ya Sheria, kanuni na taratibu za Shirika lake. Tarehe 14 Desemba 2020, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu mpya wa Vikarieti ya Mongo.

Uteuzi Mongo

 

 

 

16 December 2020, 14:06