Tafuta

Askofu Mkuu Paul R. Gallagher Askofu Mkuu Paul R. Gallagher 

Ask.Mkuu Gallagher:Lazima kulinda uhuru wa dini na maeneo ya ibada

Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher,Katibu wa Vatican wa Mahusiano na ushirikiano na Nchi akiwakilisha salam kutoka kwa Papa amehutubia katika Mkutano wa 27 wa Baraza la Mawaziri wa OSCE(Shirika kwa ajili ya usalama na ushirikiano Ulaya)uliofanyika kwa mara ya kwanza katika mtandao kutokana na janga.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Hisia za wasiwasi mkumbwa zime meoneshwa kwa  niaba ya Vatican ya Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na ushirikiano na Nchi mbele ya ongezeko la mashambulzi ya kigaidi, uhalifu wa chuki na maonesho mengine ya ukosefu wa uvumilivu dhidi ya watu, maeneo ya ibada, makaburini na vituo vingi vya kidini katika eneo lote la OSCE na sehemu nyingine. Kinacho shangaza zaidi na msalaba mzito wa vurugu zilizo nying, Askofu Mkuu amesema ni suala kuona wanaingilia waamini ambao wanakuwa wameunganisja katika sala, mahali ambapo maneo ya ibada ni mbingu ya amani na utulivu inageuka kuwa maeneo ya mateso, wakati watoto wasio kuwa na walinzi, wanawake na wanaume wanapoteza maisha yao kiurahisi kwa sababu tu wako wameunganika katika maeneo yao ya kibada ya kidini

Na zaidi hakuna iliyo baya sana, kuona kwamba baadhi ya mashambulizi ya kinyama yanatotendwa, watekelezaji wake wanatumia jina la dini. Kwa maana hiyo mwakilishi wa Vatican ndipo ametoa wito nguvu kwamba “vurugu hazitokani na dini bali zinatokana na tafsiri mbaya na mabadiliko katika itikadi. Vurugu , mates  na mauaji kwa jina la Mungu siyo dini bali ni itikadi kali ambazo lazima  kupambana nazo vikali kwa wote na kwa vyombo vya kisheria. Haki ya binadamu ulimwenguni ni msingi kwa ajili ya usalama wa ndani ya Nchi yoyote na uhuru wa kidini na imani, ambavyo lazima vilindwe na kutetewa na kama ilivyo hata matokeo ya ulinzi wa maeneo yote ya ibada.

Kutokana na hilo OSCE lazima ikabiliane  ili kutoa kila aina ya ukosefu wa uvumilivu na uhalifu dhidi ya Wakristo, Wayahudi, Waislam na wajumbe wa madhehebu mengine  ya kidini bila shutumu  au hierakia ,na kukabiliana na uhalifu wa chuki na mahitaji ya usalama  wa kulinda jumuiya za kidini. Ni lazima kubaki macho, ameshauri Askofu Mkuu kwa sababu wakati wanaendelea kuteseka kwa sababu ya hukumu, ukosefu wa uvumilvi, ubaguzi na vurugu zinazidi kupamba moto. Wakati huo huo, mwakilishi wa Vatican amegeukia hata sehemu nyingine ya changamoto ambayo bado inaunganisha  wote hasa juu ya usalama, kama vile kiitwacho migogoro iliyogandamana, na ambayo sasa imedumu kwa makumi ya miaka na ambavyo vinahitaji kupata suluhisho kwa kweli.

Kwa mtazamo huo, Vatican inawatia moyo wa kuendelea kufanya kazi kwa ajili ya amani na haki na kuunga mkono mazungumzo na heshima ya haki ya kimataifa, kama chombo muafaka kwa ajili ya suluhisho la migogoro. Wito wa Askofu Mkuu Gallagher  ni kwa wajumbe wote wa OSCE , ili kujikita katika jitihada za nguvu walizopewa majukumu na ili iwe ishara ya kuheshimu na kupongeza hata mbele ya shirika lenyewe. Askofu Mkuu amezungumzia hata  hali halisi ya sasa ya janga ambayo inaendelea kuyumbisha ulimwengu na kwa kutazama katika maeneo ya OSCE. Amebainisha kuwa kati ya waliokumbwa zaidi na mgogoro ni jamii  ambazo zilikuwa tayari ni maskini kiuchumi na ukosefu wa usawa. Ni lazima kulinda maisha. Mwaliko wa Askofu ni kufikiria ulazima wa mshikamano na uongofo wa akili na mioyo.

04 December 2020, 17:22