Tafuta

Vatican News
Askofu Mkuu Ivan Jurkovič, Askofu Mkuu Ivan Jurkovič, 

Ask.Mku Jurkovič:kuboresha mfumo bora duniani wa haki miliki&kuhakikisha matibabu na chanjo kwa wote

Katika mjadawa juu ya Hati Miliko na Afya wa kanisa ya Kudumu ya Shirika la Miliki Dunina(WIPO),Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa huo Geneva,amesisitizia juu ya kuboresha mfumo ulimwenguni wa Hati miliki ili kuweza kuhakikisha matibabau na chanjo kwa wote hasa wakati huu ambapo afya ulimwenguni iko mashakani.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Askofu Mkuu Ivan Jurkovič, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa mataifa jijini Geneva, kizungumza tarehe 7 Desemba 2020  katika mjadala juu ya Hati miliki na afya ya Kamati ya Kudumu ya Shirika la Miliki Duniani (Wipo) amesema Haki Miliki lazima kila wakati iwe chini ya mahitaji ya faida ya wote na sio kwa mantiki ya soko ambayo inapaswa kufuatiliwa na mifumo ya kutosha kudhibiti, hasa wakati ambapo afya iko hatarini. Awali ya yote Mkutano huo umekuwa ukianzia katika z kujadili dharura ya Covid-19  ambayo inapendekeza kwa upande mmoja umuhimu wa Hati miliki kama motisha ya kutafuta matibabu na chanjo na, kwa upande mwingine, hitaji la kufanya dawa zipatikane kwa njia ya haki na endelevu kwa wote, hali ya ambayo kimsingi kutokana na  mgogoro wa sasa wa kiafya, kwa sababu, kama asemevyo Askofu Mkuu Jurkovič “Hakuna mtu anayejiokoa peke yake akikumbusha maneno ya Papa Francisko anayorudia kutayataja mara nyingi.

Tayari WIPO inashirikiana katika habari za kisayansi

Hata hivyo kuna hali chanya kwa maana nyingine kwani amesema ni utayari ulioonyeshwa na Wipo wa kukuza ushirikiano wa habari za kisayansi kwa upande huu, kama inavyotakiwa na Umoja wa Mataifa, kati ya mambo mengine, kupitia jukwaa lake jipya la Patentscope. Walakini, bado inabakia wasiwasi fulani wa kimaadili ambao tayari ulioneshwa hapo zamani na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), kuhusu ufikiaji mzuri wa mafanikio ya utafiti. Mchango kwa jamuiya ya uvumbuzi kuwa na Hati miliki haujumuishi tu uvumbuzi kama huo, lakini pia katika kutoa habari ya kiufundi juu ya uvumbuzi huo na hivyo Askofu mkuu Jurkovič, akikumbuka kwamba,  mshikamano wa sera ili  kufikia malengo mawili ya upatikanaji wa dawa na uvumbuzi wa matibabu sasa ni muhimu zaidi kuliko hapo awali.

Kuna mbio za baadhi ya Serikali kutaka kuchuka chanjo mpya

Ni kufuatia na hitaji hili lililo angaziwa na Mwakilishi wa kudumu la kuboresha mfumo wa Hati miliki katika ulimwengu unaolenga zaidi ya yote uwazi zaidi na ufanisi. Mfumo ambao una uwezo wa kulinda haki za wamiliki wa hati miliki, lakini pia zile za watumiaji wa dawa zilizo na hati miliki na usawa wa haki na majukumu. Janga na pendekezo la mbio za  baadhi ya Serikali   kutaka kuchukua chanjo mpya, Askofu Mkuu Jurkovič amesema, inaonesha kuwa upatikanaji wa dawa na chanjo za bei rahisi sio changamoto tena kwa nchi zilizoendelea kidogo na kwa wengine wa maendeleo, lakini imekuwa suala linalozidi kuwa dharura pia kwa nchi zilizoendelea. Janga la pamoja ambalo familia ya wanadamu inakabiliwa mwaka huu linapaswa kuamsha hisia za kuunganishwa kwetu kama jamuiya ya ulimwengu, ameihitimisha, Askofu Mkuu akikumbusha maneno ya Baba Mtakatifu Francisko katika Waraka wa “Fratelli tutti” yaani  “Wote  ni ndugu” kwamba  “sisi sote tupo katika mtumbwi mmoja, ambapo shida za mtu mmoja ni shida za kila mtu”.

10 December 2020, 16:07