Tafuta

Maombi nchini India Maombi nchini India 

Ujumbe wa matashi mema ya siku kuu ya kihindu ya Deepavali 2020!

Katika fursa ya Siku kuu ya Kihindu iitwayo Deepavali 2020,Baraza la Kipapa la mazungumzo ya Kidini,imetuma ujumbe wake wa matashi mema katika tuki hilo ambalo litafanyika tarehe 14 Novemba kwa kuhimiza mshikamano na ukarimu kama njia ya iliyoelekezwa na Papa Francisko kuipitia kuelekeza ulimwengu baada ya covid.Janga limeleta athari nyingi lakini ni kuwa na tumaini la kuondokana tukiwa bora.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini wametuma ujumbe wao kwa kutoa heri na baraka  katika fursa ya sherehe za kihindu iitwayo Deepavali, 2020 ambazo mwaka huu zinafanyika tarehe 14 Novemba. Katika ujumbe huo uliosainiwa na Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot, MCCJ na katibu wake mkuu Monsinyo Indunil Kodithuwakku Janakaratne Kankanamalage, wanabainisha kwamba  katikati ya janga la Covidi-19, sikukuu hiyo yenye maana inaweza kufagillia  mbali wingu kubwa la hofu, wasiwasi na kila aina na woga na kuwajaza ndani ya akili na moyo  ule mwanga wa urafiki, ukarimu na mshikamano. Ujumbe huo mwaka huu wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini umebaba hisia nzito za uhamasishaji wa mazungumzo, na ushirikiano kati ya dini na kwa kufuata kwa kina  utamaduni huo wa kuwatumia heri za siku kuu huku wakiwasindikiza na tafakari muhimu.                                       

Katika ujumbe huo wanaandika kwamba unakusudia kujua, kulinda, kuhamasha mambo mema yaliyomo katika tamaduni mbili za kidini na urithi wa kitasaufi(rej Nostra Aetate, 2),na kwa maana hiyo  mwaka huu ni miaka 25 tangu kuendeleza kutuma ujumbe wa siku kukuu. Kutokana na kwamba si  ishara hizo tu ndogo za hatua ya kuelekea kuheshimu na kushirikiana kidini, miaka hii ujumbe uliotolewa umechangia kuhamasisha mazungumzo na  maelewano kati ya Wahindu na Wakristo wa ngazi mbalimbali. Ujumbe unashauri kuendeleza  utamaduni huo kwa lengo la kuunda, kutia moyo na kuwa na mahusiano ya kina  ya pamoja kati ya Wahindu  na Wakristo kama chombo cha ushirikiano kwa ajili ya wema wa wote na ubinadamu wote.

Mwaka huu, katika hali halisi ya Covid -19, ujumbe huo unataka kushirikisha baadhi ya mawazo kuhusu ulazima wa kutia moyo wa kuwa na roho chanya na matumaini kwa ajili ya wakati ujao  hata kama mbele ya vizingiti ambavyo kwa urahisi utafikiri havipitiki, changamoto za uchumi kijamii, kisiasa, na kiroho, lakini pia hata hisia mbaya, ukosefu wa uhakika na woga ulioenea.  Jitihada zao kwa maana hiyo zijikite juu ya kuamini kwamba Mungu aliyetuumba, atatusaidia, na wala hatatuacha kamwe. Lakini pia hata kutiwa moyo kwa hakika inaonesha kuwa ni jambo dogo, kutokana na wale ambao wamepoteza wapendwa wao au wafanyakazi wenzao na rafiki. Kiukweli, ujumbe unasisitiza, hata matumaini na maana chanya ya nguvu inahatarishwa kupotea katika majanga na hali hizi zilizosababishwa na janga na matokeo yake hasi ya maisha ya kila siku, kama vile uchumi, msaada wa kiafya, elimu na mazoezi ya kidini.

Lakini kiukweli ndiyo ni matumaini ambayo yanatoka katika huruma ya Mungu kusaidia kuwa hai na utashi wa kutenda ili kuweza kuwasha matumaini hayo zaidi katikati ya jamii zetu. Janga kwa hakika, limeeleta mabadiliko makubwa sana, katika mtindo wetu wa kufikiria na kuishi, hata kama kwa ngazi ya ulimwengu, limesababisha mateso mengi mno na karantini ambayo umebadilisha maisha ya kawaida. Uzoefu wa mateso na maana ya uwajibikaji wa pamoja, umefanya kuunganisha jumuiya zetu katika mshikamano, mahangaiko, katika matendo ya ukarimu na upendo mkubwa kwa wale ambao wanateseka na wenye kuhitaji msaada. Ishara hizi za mshikamano, ujumbe unaelezea, zimefanya kutambua na kuongeza zaidi kwa dhati  umuhimu wa maisha, kwa sababu ya kuwa na uwezo wa kila mmoja na mahitaji ambayo kila mmoja anahitaji. Hii ni kwa sababu ya ustawi wa wote na nyumba yetu ya pamoja, kama vile alivyobainisha Papa Francisko, kwamba: “mshikamano leo hii ni barabara ya kupitia kuelekea ulimwengu wa baada ya janga, kuelekea uponywaji wa magonjwa ya ubinafsi na ya kijamii” ni “ barabara kwa ajili ya kuondokana na kuwa bora katika mgogoro(rej. Katekesi, 2 Septemba 2020).

Ujumbe wa baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini aidha unasema “Matarajio yetu ya utamaduni wa kidini, yanatufundisha kubaki na tabia chanya  na matumaini hata katika mambo ambayo ni kinyume. Kwa kuzingatia tamaduni na mafundisho ya kidini tunaweza kupambana katikati ya mgogoro wa ulimwengu ili kueneza kile ambacho Papa Francisko anakiita “ambukizo la  tumaini” (rej Ujumb wa Urbi et Orbi, 12 Aprili 2020) kwa ishara za utunzaji, ukarimu na huruma ambazo ndiyo zaidi ya maambukizi ya virusi vyenyewe vya corona. Na kwa kuhitimisha, Ujumbe huo unasema kuwa “kwa kuwa tamaduni na mafundisho ya kidini yamejengwa juu ya thamani na maadili yetu ya ushirikishano na juu ya jitihada kwa ajili ya ubora wa ubinadamu, tunaweza sisi kama wakristo na wahindu kuungana na watu wote wenye mapenzi mema  ili kujenga utamaduni chanya na matumaini katika moyo wa jamii zetu, si tu katika siku ngumu lakini hata katika wakati ujao ambao upo mbele yetu”.

06 November 2020, 15:51