Tafuta

Assisi, Uwakilishi wa Economy of Francesco Assisi, Uwakilishi wa Economy of Francesco  

The Economy of Francesco:tayari ni harakati ya ulimwengu!

Bwana Luigino Bruni,mhusika wa kisayansi wa mkutano wa kimataifa wa wanauchumi vijana na wajasiriamali,anasimulia athari za miezi tisa ya kazi ya maandalizi baada ya kuahirishwa kutokana na janga la corona.Kutoka katika mkutano huo ni matumaini ya kwamba uchumi utakuwa na uwezo wa kuangalia ubora wa ukuaji na uwekezaji katika hali ya kiroho.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko alikuwa amezungumza kwa nguvu sana katika mzunguko wake wa katekesi baada ya wimbi la kwanza la janga, kwa kujikita juu ya ulazima wa “ kuponesha ulimwengu dhidi ya ukosefu wa usawa, uliooneshwa na mgogoro wa kiafya. Virusi ni mtoto wa uchumi uliougua. Ugonjwa mmoja ambao ni tunda linalokua kwa sasa katika mkutadha wa mabadiliko ya sasa ya uchumi na kutoa roho ya kesho. Kwa maana hiyo Papa Francisko mwezi Mei 2019 alikuwa amezindua  wazo la “The Economy of Francesco”, akiwaalika wote kushiriki mwezi Machi 2020 mjini Assisi maelfu ya vijana wanauchumi na wajasiriamali.

Kwa kuufuta na baadaye kuahirishwa kwa sababu ya wimbi la kwanza la janga, tuko hili sas limefunguliwa kwa njia ya mtanadao kuanzita tarehe 19 kwa ushiriki wa vijana elfu mbili waliojiandikia kutoka nchi 120,  kushikamana, kwa siku tatu, ulimwenguni, kwa njia ya moja kwa moja katika mtandao kwa jukwaa la  francescoeconomy.org  na ushiriki wa  dhati kwa njia ya mtandao na Papa Francisko. Huko Assisi, ambayo inaongoza tukio Profesa Luigino Bruni, Uchumi wa Siasa katika Chuo Kikuu cha Lumsa cha Roma, na mkurugenzi wa kisayansi wa “Economy Of Francesco” yaani  ‘Uchumi wa Francisiko’,  amezungumza na  studio za Redio ya Vatican, Italia juu ya hali ya furaha na matumaini na anaelezea jinsi ambavyo  Papa alivyoomba kuhuisha uchumi kwa dhati.

Kuuisha  inamaanisha  kurudisha roho  kwa sababu kurudisha roho katika  uchumi ni moja wapo ya mada kuu ya mafundisho ya Papa Fransisko. Lakini pia inamaanisha kumuuisha mtu aliye mgonjwa na tena katika mawazo ya Papa uchumi leo  hii  umeugua na hivyo unapaswa  kuponywa. Kwa jinsi  hiyo kuhuisha tena  uchumi ni kucheza na maneno ambayo kwa hakika yanamaanisha mambo mawili. Kwanza kurudisha roho na kuponyesha uchumi uliougua. Na ndivyo hivyo hasa  vijana ambao wamefanyia kazi kwenye tukio  hili na wapo wanafanya kwa shauku yao yote na kujitoa. Profesa amesema kuwa “Hatupaswi kufikiria kuwa vijana kuwa na shauku"tu, lakini  kuna mengi, kujitoa sana kwa upande wao. Mchanganyiko huu wa shauku na kujitoa kwa  labda ni jambo bora juu ya kazi ndefu ya maandalizi”.

Ukuaji ni moja ya maneno makuu na ufunguo wa mkutano huo amesema, lakini pia ni neno linalowezekana, kwa sababu sio ukuaji wote ni mzuri, kama tunavyojua. Hata wasiwasi zinaweza kukua: lakini kiukweli siyo tukio chanya hali nzuri. Kwa maana hiyo kunaweza kuwa na ukuaji mzuri, ukuaji wa ustawi, wa mali za uhusiano, wa mali za pamoja. Lakini ikumbukwe kuwa siyo ukuaji wote ni mzuri kabisa. Kwa kuendelea amesea “Sisi, kwa mfano, tumekua katika miaka arobaini iliyopita, tukiharibu sayari, kwa sababu hatukuzingatia athari za ukuaji. Sisi sote tulifurahi na Pato la Taifa ambalo lilikuwa likikua kwa 3 au 4% kwa mwaka. Mbaya sana kwamba wakati unakua tulikuwa tunaharibu mazingira ya asili yanayotuzunguka”. 

 “Kwa maana hii tunahitaji kukua, lakini pia tunahitaji kufikiria juu ya maendeleo, juu ya maneno mengine mengi ambayo sio ya upimaji tu. Kwa sababu wakati tunazungumza juu ya ukuaji daima kuna shida kubwa sana kwamba hupimwa kwa idadi tu, kwa wingi, wakati vipimo vingi vya maisha ya mwanadamu hupimwa kwa ubora wake. Dhana ambayo siyo sehemu ya hesabu za kitaifa lakini ambayo ni muhimu”amesisitiza  Profesa Luigino Bruni, mchumi na mhusika wa maandalizi ya Economy of Francesco”.

Hatimaye akieleza juu ya suala la kiroho amesema kuna haja kubwa ya mtaji wa kiroho. Wafanyabiashara wanajua hii vizuri, lakini shida ni kwamba hali ya kiroho inahitaji upendeleo. Hali ya kiroho haiwezi kuzingatia suala la kuwa na faida. Hali ya kiroho inazingatia usafi wa watu ambao ndiyo hasa kama kampuni kubwa zinakosa. Hali kama hii amesema siyo rahisi kuitambua vema labda kufanyia kazi ya siku nne katika nyumba nzuri ya watawa huko Umbria... hata hivyo amesema ipangwe ili mapema au baadaye itoe kitu, kwa sababu kampuni inafuata mantiki ya kwanza ya hesabu kuwa mapema ua baadaye lazima irudi. Wakati hali ya kiroho inahitaji hewa iliyo huru, paa za juu kuliko zile za ofisi, inahitaji madirisha mkubwa kuliko yale ya viwanda vyetu. Kwa hivyo ni tumaini kwamba tukio hili pia ni wito wa uwekezaji katika hali ya kiroho ambayo uchumi unahitaji sana.

19 November 2020, 18:58