Tafuta

2020.11.27 vikofia kwa ajili ya makardinali wateule 2020 2020.11.27 vikofia kwa ajili ya makardinali wateule 2020  

Tarehe 28 Novemba kusimikwa kwa makardinali wapya kwa kufuata kanuni za kiafya

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa vyombo vya habari Vatican amethibitisha kuwa tukio la Papa kuwasimika makardinali wapya Jumamosi tarehe 28 Novemba litakuwa ni saa kumi jioni masaa ya Ulaya,wakati huo misa ya Papa na makardinali wapya Jumapili katika Mwanzo wa Majilio itakuwa ni saa nne asubuhi majira ya Ulaya.

Na Sr. Angla Rwezaula – Vatican

Kila kitu tayari kimekwisha tayarishwa kwa ajili ya tukio zuri la Kanisa! Papa Francisko Jumamosi tarehe 28 Novemba atasimika makardinali wapya 13 lakini Makardinali 2 wateule hawatakuwapo kwa sababu ya janga, hivyo watashiriki moja kwa moja kwa njia ya majukwaa ya kidigitali.  Misa ambayo itafanyika saa kumi jioni  majira ya Ulaya katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican. Itakuwa ni sherehe rahisi  lakini ya dhati kutokana na dharura ya kiafya ambapo itawaona makardinali wapya, wazamani, maaskofu, mapadre, watawa na walei  wachacha katika Kanisa kuu.

Katika tukio la Baraza la Makardinali kwa mwaka huu wa dharura covid-19 liimekuwa na  mabadiliko na kwa maana hiyo litafanyika kwa mujibu wa kuheshimu utamaduni wake japokuwa kwa kuzingatia umbali kutokana na kanuni za kiafya ili kuzuia maambukizi. Kwa mujibu wa maelezo kutoka ofisi ya Mshereheshaji wa Sherehe za kiliturujia za Kipapa (Ucepo), wanaema: “kama ilivyo kwa maadhimisho katika kipindi cha dharua, hata ibada ya kusimikwa kwa makardinali wapya itafanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na siyo katika eneo la Maungamo na kwa ushiriki waamini wachache, karibia miamoja”.

Maadhimisho ya Misa ya siku itakayofuata tarehe 29 Novemba 2020 ambayo Papa Francisko ataadhimisha akiwa na makardinali wapya itakuwa ni saa 4.00 asubuhi katika Dominika ya Kwanza ya Kipindi cha  Majilio, kipindi cha kujiandaalia kuzaliwa kwa Mkombozi wetu. “Misa zote mbili mwaka huu hazitakuwa na mtindo wa Kikanisa cha Kipapa na pia ushiriki wa waamini wachache ambao ni, watawa, makuhani na maskofu. Kwa namna ya pekee, katika maadhimisho, makardinali wateule na wazamani watakuwa karibia 100, kutoka kwa wanaosindikiza makardinali wateule, zaidi ya maparoko, wakuu wa makanisa ambayo watakabidhiwa makardinali wapya.” Kutokana na wengine kutoweza kushiriki katika Baraza hilo la la makardinali jijini Roma, lakini wataweza kuungana moja kwa moja kupitia majukwaa ya kidigitali ambayo yatawawezesha kushiriki moja kwa moja katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican. 

27 November 2020, 14:07