Tafuta

2020.10.25 Kusimikwa makardinali wapya tarehe 5 Oktoba  2019 2020.10.25 Kusimikwa makardinali wapya tarehe 5 Oktoba 2019  

Tarehe 28 Novemba kusimikwa kwa makardinali wapya na kufuata kanuni za afya

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa vyombo vya habari amesema tukio la kusimikwa kwa makardinali wapya Jumamosi 28 Novemba na Papa litakuwa ni saa 10:00 jioni.Makardinali wawili wateule hawatakuwapo kwa sababu ya janga,hivyo watashiriki moja kwaja kwa njia ya majukwaa ya kidigitali.Ziara za kutoa pongezi kwa makardinali wapya zimeondolewa na kupunguza ushiriki wa waamini watakaoudhuria tukio hilo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kama ilivyokuwa imetangazwa tarehe 25 Oktoba mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana na Papa Francisko, Jumamosi ijayo tarehe 28 Novemba saa 10.00, katika Altare ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, maadhimisho ya kuwasimika Makardinali wapya 13 itaongozwa na Papa Francisko. Kati yao makardinali 9 hawajafikisha miaka themanini hivyo kuwa na haki ya kupigiwa kura wakati wa uchaguzi ujao wa Khalifa wa Mtakatifu Petro na wengine 4 wamekwisha fikisha miaka zaidi na themanini hivyo kupoteza haki hiyo kutokana na umri wao kuwa mkubwa zaidi.

Hawatakuwapo makardinali wawili wateule

Katika kuelezea tukio hilo  litakavyokuwa, msemaji wa vyombo vya habari Vatican  Dk. Bruni amesema “ushiriki huo makardinali wawili kati ya 13 ambapo mmoja akiwa ni Kardinali mteule  Cornelius Sim, Balozi wa kitume huko Brunei, Kardinali Mteule Jose F. Advincula, Askofu Mkuu wa Capiz (UFilipino), hawataweza kushiriki kwa sababu ya hali halisi ya kiafya, lakini wataundwa sawa na  makadinali wapya. Mwakilishi wa Papa, wakati mwingine utakapopangwa, atawapelekea kofia, pete na hati ya utambulisho huo wa ukardinali.”

Ushiriki wa waamini ni wachae na hata hakuna ziara za pongezi baada ya tukio

Kwa kuzingatia hali halisi hiyo ya kiafya ya janga na kanuni zilizowekwa za kuzuia maabukizi, hapatakuwa na ziara  kama  utamaduni, kwa maana ya kufanya  siku kuu kwa ajili ya makardinali wapya katika kushirikishana  furaha na ndugu na marafiki na waamini wengine ambao kwa kawaida hukutana kwenye vyumba mbali mbali katika Jumba la kitume hata katika Ukumbi wa Paulo VI.

Maadhimisho ya kusimikwa hayatafanyika katika Kikanisa cha Kipapa 

Pamoja na hayo hata maadhimisho ya kusimikwa kwa mujibu wa taarifa hizo, “ “haitafanyika katika  Kikanisa cha Kipapa na ushiriki utakuwa wa watu wachache (waamini walei, watawa, makuhani na maaskofu)”. Kwa namna ya pekee, katika maadhimisho, makardinali wateule na wazamani watakuwa karibia 100, kutoka kwa wanaosindikiza makardinali wateule, zaidi ya maparoko, wakuu wa makanisa ambayo watakabidhiwa makardinali wapya.” Kutokana na wengine kutoweza kushiriki katika baraza  hili la makardinali jijini Roma , lakini wataweza kuungana moja kwa moja kupitia majukwaa ya kidigitali ambayo yatawawezesha kushiriki moja kwa moja katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican. Kesho yake Jumapili  tarehe 29 Novemba saa 4.00 kamili , katika Altare ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Papa Francisko ataongoza Misa kwa ushiriki wa makardinali wapya tu.

23 November 2020, 18:05