Tafuta

2013.07.23 Mkesha wa Njia ya Msalaba wakati wa siku ya vijana nchini Brazili:Vijana na msalaba 2013.07.23 Mkesha wa Njia ya Msalaba wakati wa siku ya vijana nchini Brazili:Vijana na msalaba 

Siku ya vijana 2023:Jumapili ijayo kukakabidhiana msalaba wa vijana!

Dominika tarehe 22 Novemba kutakuwa na tukio la kukabidhi ishara za Siku ya Vijana ambayo ni msalaba na picha ya Maria Afya ya Waroma.Ni siku itakayokuwa tofauti na utamaduni wa siku ya Matawi kwa sababu ya janga la virusi vya corona.Makabidhiano yatafanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa wawakilishi vijana kutoka Panama kwa vijana kutoka Ureno.Itakuwa mara baada ya misa ya Papa Francisko.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kwa mujibu wa msemaji wa Vyombo vya habari Vatican Dk,  Bruni amethibitisha kwa waandishi wa habari kuwa “kama ilivyokuwa ametangaza Baba Mtakatifu tarehe 5 Aprili wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 22 Novemba, katika Siku kuu ya Kristo Mfalme na hitimisho la Mwaka wa Kiliturujia, baada ya Misa Takatifu itakayoongozwa na Papa Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kutakuwapo na tukio la kukabidhiana Msalaba wa Siku ya Vijana Duniani. Katika fursa hiyo watakuwapo wawakilishi kutoka Amerika kati na vijana  Ureno”.

Makabidhiano ya ishara mbili Msalaba na Picha ya Matia terehe 22 Novemba

Kwa maana hii, Dominika tarehe 22 Novemba mara baada ya misa, ishara muhimu za siku ya vijana ambazo husindikiza siku hiyo Msalaba na nakala ya Picha ya Salus Populi Romani, yaani Afya ya watu wa Roma, ishara mbili ambazo kwa miaka mingi sasa zimekuwa zikisindikiza maandalizi ya vijana na kwa maana hiyo wawakilishi kutoka Panama watawakabidhi vijana kutoka Ureno ishara hizo. Kutokana na janga la Corona uwakilishi wa vijana ni mdogo sana. Ikumbukwe siku ya vijana iliyopita ilifanyika huko Panama na sasa kwa mwaka 2023, itafanyika nchini Ureno katika jiji kuu Lisbon.

Maadhimisho ya Misa ya Siku Kuu ya Kristo Mfalme katika Kanisa Kuu la Mtatifu Petro

Maadhimisho ya misa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Vatican yatangazwa moja kwa moja katika majukwa ya youtube ya Vatican News. Vile vile, wahusika wa kichungaji wa vijana katika mabaraza yote ya maaskofu na harakati za kimataifa za vijana  wataweza kufuatilia  misa hiyo na ambao kuanzia tarehe 18 hadi Jumamosi tarehe 21 Novemba watashiriki Mkutano wa kimataifa kwa njia ya mtandao, mkutano unaoongozwa na kauli mbiu “ kutoka Panama kwenda Lisbon: tumeishi na  muungano wa kimisionari” ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha.

Siku ya Vijana ilianzishwa mnamo 1984

Kama Baraza la Walei Familia na maisha wanavyokumbusha kuwa katika fursa hii utamaduni wa kubadilishana hizo ishara ilikuwa ufanyika wakati wa Dominika ya Matawi, hasa mara baada ya Misa ya Papa Francisko katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Vaticani tendo ambao halikuwezekana kwa sababu ya janga na hatua za vizuizi ambavyo vipo barani Ulaya na ulimwengu mzima . Utamaduni huu ulianza mnamo 1984 wakati, mwishoni mwa Mwaka wa Jubilei ya Ukombozi, Papa Yohane Paulo II aliwakabidhi vijana Msalaba wa Jubilei, unaojulikana  hata leo  hii kama Msalaba wa Siku ya Vijana duniani (WYD), na tangu wakati huo katikati ya kila toleo la  Siku. Mnamo 2003, Mtakatifu Yohane Paulo  pia aliwapatia vijana nakala ya Picha ya Maria Salus Populi Romani,( Maria Afya ya watu wa Roma ambayo inasindikiza  Msalaba katika hija zake ulimwenguni kote.

Maandalizi moto moto ya siku ya vijana jijini Lisbon 2023

Kwa wakati huu, ni kama mashine kubwa katika kuandaa siku ya vijana duniani (WYD) huko Lisbon ambayo inafanya kazi ya kujiandaa vizuri katika siku hiyo ya mwaka  2023. Mada tayari imechaguliwa “Maria aliamka na akaenda haraka”, na ndivyo  hivyo hata nembo iliyozinduliwa tarehe 16 Oktoba  iliyopita  katika siku ya kumbu kumbu ya tarehe na mwezi wa uchaguzi wa Mtakatifu Yohane Paulo II, mwanzilishi wa Siku ya Vijana duniani (WYD). Kwenye wavuti ya www.lisboa2023.org, kuna sasisho zote na mipango ya kungojea tukio hilo ambalo linaashiria mustakabali wa vijana kwa vizazi vingi.

17 November 2020, 15:15