Tafuta

2019.06.03 Prof Stefano Zamagni, Taasisi ya Kiapa ya Elimu sayansi jamii. 2019.06.03 Prof Stefano Zamagni, Taasisi ya Kiapa ya Elimu sayansi jamii. 

Prof.Zamagni:Ni wakati sasa wa kubadilisha mfumo wa uchumi usiofanya kazi tena!

Mwenyekiti wa Taasisi ya Elimu ya Sayansi jamii amewakilisha tukio la 'Economy of Francesco',lililopendekezwa na Papa Francisko ili kuonesha njia ya upyaisho kijamii na kiuchumi.Ni tukio linaloanza Alhamisi tarehe 19 hadi tarehe 23 Novemba.Mfumo wa sasa wa kiuchumi haufanyi kazi tena,kwa maana hiyo kuna lazima wa upyaishwe na kanuni hata katika masoko.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ni tukio maalum na ambalo ni zaidi ya miaka elfu mbili ya maisha ya Kanisa. Ndivyo amesema Profesa wa Uchumi, Stefano Zamagni na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kipapa ya Elimu  sayansi jamii, akiwakilisha ‘Economy of Francesco’, yaani uchumi wa Francis, tukio la kimataifa kwa matashi ya Papa ili kuelekeza katika Dunia ulazima wa kuanzisha mchakato wa mabadiliko ya kidunia juu ya mfumo wa uchumi na kijamii. Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa tarehe 19 hadi 23 Novemba 2020 kwa njia ya mtandao na utawaona washiriki zaidi ya vijana elfu mbili wanauchumi na wajasiriamari ambao watakabiliana katika mada muhimu kuhusu kazi, maadili, fedha na akili mbadala.

Kwa mujibu wa Profesa Zamagni amesema, “roho ya mkutano huo kwa hakika ni ile ya matumaini sana kwa kuwa sasa ni nyakati zilizokomaa za kuwa na utambuzi kwa wote hata wale ambao  hadi leo hii, walikuwa hatawaki kukubali suala hili la uchumi ambao haufanyi kazi na ambao kwa hakika unaendelea kuzalisha hatari sana. Kwa mujibu wa Profesa Zamagni njia za kuzuia hatari hizo na ambazo kiukweli watakabiliana nazo katika tukio hili awali ya yote amesema lazima kubadilisha kanuni za kufanya kazi katika masoko kwa sababu bila kanuni mpya ni kugeuka kichaka kikubwa mahali ambamo kwa ulazima wanashinda wale wenye nguvu tu. Lakini hata hivyo mwisho wale wenye nguvu wanapobaki peke yao, basi hatima ni kupoteza kabisa, na baadaye inahitajika  kupendekeza mbadala wa usawa na ulazima wa kurekebisha  utaratibu katika usawa.

Haiwezekani kufunga macho yetu kwa utaratibu wa kiuchumi ambao huongeza ustawi kamili lakini ambao, wakati huo huo, unapanua umbali zaidi kati ya vikundi vya kijamii na mataifa. Tatu, lazima ugeuzwe uhusiano uliopo sasa kati ya demokrasia na soko, ambalo ni, kati ya uchumi na siasa. Leo hii  kila mtu anajua kuwa siasa ni huduma ya uchumi: hii sio jambo la kweli. Kama  vile wanauchumi Adam Smith, John Stuart Mill na Antonio Genovesi tayari waliandika hapo zamani, uchumi lazima uwe katika huduma ya siasa, na  sio kinyume chake, amesisitiza Porfesa Zamagni

Kwa kuhitimisha amejibu swali ikiwa watazungumzia hata juu ya shule na vyuo vikuu, na kuthibitisha kuwa ni hakika. Shule na vyuo vikuu lazima virudi kuwa sehemu za elimu. Hii ni hatua ambayo Baba Mtakatifu Francisko alirudia kusema mnamo Oktoba 15 na Mkataba juu ya Elimu Kimataifa. Kwa bahati mbaya, sekta ya shule imekuwa mahali pa elimu tu: na kumbe neno la kigiriki scholè linamaanisha, kwanza kabisa, mahali pa kuelimisha, vile vile ni  elimu, kama alivyokuwa akisema Aristotle. Ikiwa shule hairudi kuwa mahali pa elimu ni dhahiri kwamba fadhila haziwezi kuongezea na kuenezwa. Ikumbukek Aristotle ni mtu mashuhuri katika falsafa ya Ugiriki wa zamani, ambaye alitoa michango muhimu katika mantiki, ya ukosoaji, usemi, fizikia, biolojia, saikolojia, hisabati, metafizikia, maadili, na siasa.

18 November 2020, 17:32