Tafuta

2014.11.25 Ukumbi wa Baraza la Ulaya huko Strasburg. 2014.11.25 Ukumbi wa Baraza la Ulaya huko Strasburg. 

Parolin:Ulaya iwe nyumba ya kila mtu na kuhisi mazingira ya udugu!

Katika hotuba ya katibu wa Vatican inaangazia umuhimu wa mtu na juu ya ulinzi hadhi yake.Wakati wa janga ni roho ya mshikamano tu itakayookoa wale walio katika mtumbwi mmoja, katika nyumba moja na katika ardhi ile ile.Amesema hayo tarehe 12 Novemba katika Baraza la Ulaya huko Strasbourg, katika maadhimisho ya miaka 50 tangu uwepo wa uwakilishi wa Kudumu wa Vatica katika Baraza hilo.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Katika fursa ya kufanya kumkukumbu ya miaka 50 tangu uwepo wa uwakilishi wa kudumu  wa Vatican katika Baraza la Umoja wa nchi za Ulaya, Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican ametoa hotuba yake kwa kuelezea historia ndefu ya mchakato ambao ulianzia mwaka 1962. Ni historia  ambayo ni muhimu na jitihada za kutetea haki za binadamu, demokrasia na haki  za serikali zote za bara zima. Kardinali amekumbusha jinsi ambavyo Papa alipenda kuwakumbusha wakati wa ziara zake katika Taasisi hizo za Ulaya, kwamba ndoto ya waaanzilishi ni ile ya kuijenga upya Ulaya kwa roho ya huduma ya pamoja ambayo iwe awali ya yote kuhudumia na matendo ambayo yawe jiwe msingi wa thamani kubwa ya  utume wa Baraza la Ulaya kwa jina la amani, la uhuru na hadhi ya binadamu.  Kardinali Parolin anataja hata fursa nyingine za hivi karibuni katika  kusisitiza utunzaji wa mtu kuwa uwe ndiyo kitovu cha kuendelea kuijenga Ulaya kwa mujibu wa Waanzilishi wake. Utunzaji wa hadhi ya mwandamu ni msingi na kusizingatiwa, na kwa Vatican ni  kipaumbele cha Papa Francisko, ambacho kimeoneshwa wazi katika Waraka wake wa Mwisho wa ‘Fratelli tutti’ kuhusu udugu na urafiki kijamii.

Lakini pamoja na tafakari juu ya hadhi ya kibinadamu na kiini cha mtu, wakati wa janga amefafanua  Kardinali Parolin, inahitaji pia kuzingatia heshima ya demokrasia na sheria, kama inavyosemwa katika miongozo, iliyotumwa kwa nchi zote wanachama 47 wa Baraza ya Umoja wa  Ulaya mnamo tarehe  7 Aprili 2020. Katika suala hili, Katibu wa Vatican amebainisha kwamba ni hadhi pia ya mwakilishi wa kudhumu katika Baraza hilo na ambalo haitoshi tu lakini ni katika kufanya  kazi  ili kujenga miundo ya mshikamano kwa faida ya wote, na  kupitia ushawishi wa maadili ambayo yanaonesha katika tathmini yake, kama mtaalam wa ubinadamu na katika ushirikiano thabiti kwa ngazi mbali mbali za maamuzi. Katika kueleza hayo, Kardinali amefafanua baadhi ya mambo ambayo ni kama  ukweli ambao unatazamwa si kama mtu binafsi bali kama mtu mwanadamu, na si kwa ajili ya walio wachache tu bali kwa watu wote.

Ukweli ambao hauna faida kwa  baadhi tu lakini kwa ajili ya Ulaya nzima kama ilivyo ulimwengu mzima. Matakwa yake mema kwa upande wa Ulaya iweze kugeuka kuwa  nyumba binafsi ya kibinadamu na kwamba Baraza la Ulaya, liheshimu kazi yake kwa misingi yake na kuendelea kuangaza daima ule mwanga wa ukweli wa mtu binadamu. Ukweli wa kwanza wa  binadamu wa ulimwengu ni ule wa utakatifu wake. Hii ina maana kwamba binadamu katika mfano wa Bwana muumbaji, akiwa huru dhidi ya kila aina ya utumwa,  iwe kwa vitu au kiroho. Ukweli huu wa kwanza unaangaza na kutoa maswali ya kujiuliza. Leo hii kuna hatari ya mitindo mipya ya utumwa ambayo inamsumbua mwanadamu, hivyo lazima kutolia maanani  kiini cha kazi ya Baraza la Ulaya ili lisibaki bila kutafuta suluhisho, na kuhijihusisha kupata majibu yanayokwenda sambamba na mantiki kwa ajili ya kumwekwa mwingine awe kiini cha huduma na lengo la kazi.

Ukweli huu wa kwanza wa ulimwengu wote unafuatwa na wa pili. Muumba wa mwanadamu pia aliifanya Dunia kuwa makao ya mwanadamu. Alifanya kuwa nyumba ya kila mtu. Kwa hivyo kila mtu, pamoja na taasisi, anapaswa kuitunza. Hata kwa kujibu wito  iliozinduliwa na Papa katika maandishi ya Laudato si ', Baraza la Ulaya, anabainisha Kardinali Parolin  linafanya kazi katika mwelekeo huu na janga la Covid-19, ambapo ni pendekezo ambalo halipaswi kuathiri ahadi hiyo.

Ukweli wa tatu  wa ulimwengu ni huduma ya mtu binadamu. Hili suala la pili limetazama mkutadha wa uhamiaji, ambao Kardinali amesisitiza juu ya kufikiria mwanadamu na mahitaji yake, si mwili tu wa kulisha, lakini hata roho yake, akili, wito katika muungano, udugu wa ulimwengu, upendo ambao haujuhi kikomo. Katika hili Kardinali amepongeza Kamishna  wa haki za binadamu ya Baraza la Umoja wa Ulaya Bi Dunja Mijatović, ambaye ameeleza kama walivyojikita katika programu mbalimbali msingi kuhusu Elimu na mafunzo ambayo si tu kujua kusoma na kuandika, lakini kama pendekezo la Baraza la Ulaya, ambalo halibagui, utamaduni wa amani, ulinzi wa lugha na tamaduni za watu walio wachache na kuhamasisha mtu binadamu. Ukweli wa nne wa ulimwengu ambao Kardinali Parolin amependekeza ni kuthamanisha mtu ambapo amesema  muktadha huu, unatazama mambo mengi, hasa zoezi ambalo limtazame  mtu, ni lile la kuthamini kwa kuonesha kwa Mataifa, mashirika ya kimataifa, dini zote, vyama vyote vyenye lengo la msaada wa kibinadamu, vinaongozwa na ukweli wa upendo, yaani upendo zaidi kwa ajili ya ubinadamu. “Kila mmoja wetu, anayewakilisha nchi mbali mbali, akigeuka kuwa balozi wa amani katika serikali yake, ndipo kweli inawezekana kufanya zoezi la kutengeneza amani zaidi iwezekanavyo kwa ajili yetu sisi na kwa ajili ya Nchi zilizo karibu nasi”

Kwa namna hiyo, Ulaya nzima, iliyoungana na thabiti, inaweza kujionesha kweli kuwa ishara ya haki katika ulimwengu wote. Hilo pia ni moyo wa Papa, lakini pia ni suala ambalo kwa bahati mbaya inabaki bado kuwa mbali kulifikia, amesisitiza” Kardinali Parolin. Pamoja na hayo yote, amethibitisha kuwa na utambuzi wa asili ya dini na utume wake ulimwenguni, ambao unataka kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya amani, na katika kuamini kuwa ni katika jitihada za umoja na dunia, ambayo inapendekezwa kuwa kiini cha ulinzi wa mtu, kwa namna ya pekeea wanawake, watoto na watu wote wasio kuwa na ulinzi, pamoja na kulinda haki zao msingi, ambazo kweli zinawezekana kutafuta amani na maendeleo ya watu Amani lazima itafutwa daima na kila mtu. Hitimisho la Kardinali Parolin ni matashi mema ya jitihasa kwa ngazo zote za Taasisi ili kuelezea katika ujenzi wa Ulaya ya Haki, ya muungano, iliyofunguliwa na jumuishi, jitahada zambazo Vatican inapyaisha kwa dhati katika kuta msaasa kama ilivykuwa miaka 50 iliyopita. “Fanyeni Ulaya kuwa nyumba ya kila mwanadamu, mfanye kila mtu ajisikie yuko nyumbani katika mazingira ya udugu. Kila mtu anatarajia kuona mfano halisi wa ubinadamu, ili kuweza kujitoa kibinafsi”, amehitimisha Kardinali Parolin.

14 November 2020, 15:35