Tafuta

2018.09.12Nyumba Ndogo ya Huruma ya Gela 2018.09.12Nyumba Ndogo ya Huruma ya Gela 

Papa:Nyumba ndogo ya Huruma huko Gela ni mwanga wa taa ya matumaini katika giza!

Nyumba Ndogo ya Huruma huko Gela ni mwanga wa taa na tumaini katika giza la mateso.Ndiyo maneno ya Papa Francisko katika barua yake aliyoiandika kwa mkono wake akiwatia moyo Padre di Dio mwanzilishi wa nyumba ya kutoa msaada kwa wenye shida na watu wa kujitolea.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko amependelea kuwaandikia barua kwa mkono wake kuonesha ukaribu wake wa  “Nyumba ndogo ya Huruma” ya Gela huko Sicilia, nchini Italia iliyoanzishwa kuwasaidia wale wote ambao wamejaribiwa na matatizo mengi ya maisha na kwa ajili ya kuwatia moyo wale wote ambao kila siku wanajitoa kwa moyo wote  bila kujibakiza kuwasaidia. Kazi ya ukaribu kwa watu wanaoteseka na ambao wanajikuta katika hali ya matatizo ni mwanga wa taa na tumaini katika giza la mateso na kukata tamaa, anabainisha Papa Francisko. Kwa njia hiyo  anaipongeza ishara hiyo ya ushirikishano wa Kanisa na watu walio na matatizo magumu. Huo ni mchango na  mfano wa upendo wa kiinjili kwa Kanisa linalotoka nje na ambalo linafanyaa vizuri kwa Jumuiya kutenda kwa ajili ya Kanisa na kwa ajili ya raia, anasema Papa.

Nyumba Ndogo ya Huruma ilianzishwa mnano mwaka 2013. Wazo hili lilitokana kwa Padre Pasqualino di Dio, kijana kuhani ambaye tokea akiwa Uwanja wa Armerina, mara baada ya kushiriki Misa ya kwanza ya Umma ya Papa Francisko , tarehe 17 Machi alipokuwa amefanya izara yake fupi ya kichungaji, na baadaye alikutana naye  Padre huyo na kumweleza hali halisi ya kijamii katika jimbo lake, matatizo ya familia nyingi na watu walio wa mwisho wa mji wake. Papa Francisko alimsikiliza kwa makini  na kumshauria atoe maisha kwa kuanzisha jambo fulani kama nyumba ambayo ingeweza kuwa ishara ya huruma kwa Mungu. Leo hii, nyumba hiyo inatoa huduma ya chakula na ni kituo cha usikivu kwa ushauri, cha kusindikiza, lakini pia ghara  ya vyakula  ikiwa mikononi mwa watu wengi wa kujitolea ambao wanatoa huduma mbali mbali za ushauri wa familia, kusaidia watoto baada ya shule na shughuli ya kimkakati na Caritas, taasisi mahalia, maparokia na vyama mbalimbali.

Papa Francisko katika  barua yake kwa Padre Pasqualino di Dio amemtia moyo yeye na wale wote wanaoshirikishana naye katika harakati za mpango huo kwa ajili ya wema, na kuwapongeza kwa uvumilivu wa kitume katika kushuhudia upole na upendo wa huruma ya Baba, kwa kutoa ushirikishano na mshikamano kwa walio wadhaifu zaidi na wasio na imani tena. Kwa ushirikiano na Chama cha Kijamii, kitwacho “Raphael”,  ‘Nyumba Ndogo ya Huruma’ inasimamia kitengo cha kliniki ya matibabu, bweni, ukumbi wa shughuli mbali mbali za mikutano, ushonaji, useremala na sanaa ya ufinyanzi ambazo kwa hakika zinakuwa karibu na  wadhaifu. Papa Francisko anandika kuwa “Ninawahakikishia kuwakumbuka katika maombi kwa watu wote wa kujitolea na wale ambao wanakusaidia wewe na, wakati ninawaombea mniombee hata mimi, ninatumia Baraka ya Kitume”, amehitimisha barua yake Papa.

Kwa upande wa Padre Pasqualino di Dio katika maoni yake kuhusu maneno ya Papa Francisko ameyafafanua kama “ishara ya mapendo makuu na pia ya uthibitisho wa kazi hiyo kwamba katika ukimya wanaume na wanawake wengi wenye mapenzi mema  wanafanya huduma yao kwa ajili ya walio wadogo wa Injili”. Aidha kuhani huyo amesema  watu wa kujitolea na wafadhili wanaopeleka mbele ‘Nyumba ndogo ya Huruma’ ni ndoto ya upendo, hasa wakati huu wa kuchanganyikiwa na mateso ambayo yamesababishwa na janga la corona.  “Huduma zote zinazofanyika katika Kituo chetu zina kitovu kamili na hasa katika kuabudu Ekaristi daima” na kuongeza, kutokea hapa hapa ndiyo tunapata  nguvu kutoka kwa  aliye juu”.  Aidha amesema “Tumeitwa katika wakati huu mgumu kuelekeza mawazo yetu kwa wale walio dhaifu na walio hatarini zaidi bila kuruhusu utamaduni wa kutupilia mbali na tuhuma za kutaka kutawala, ambazo lazima zibadilishwe ili  kuhamasisha suala la  utunzaji wa mwingine, tukiwa na hakika kuwa maisha ni milki tu kutoka kwa Bwana na ambaye kamwe hatuachi” amehitimisha.

07 November 2020, 16:06