Tafuta

Pope Francisko akutana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya mjini Vatican. Pope Francisko akutana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya mjini Vatican. 

Papa Francisko akutana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya!

Papa Francisko,Ijumaa tarehe 6 Novemba 2020 amekutana na kuzungumza na Rais wa Kenya Bwana Uhuru Kenyatta ambaye baadaye amekutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin,Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher,Katibu mkuu wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ijumaa tarehe 6 Novemba 2020 Papa Francisko amekutana na Rais wa Kenya, Bwana Uhuru Kenyatta ambaye baadaye amekutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

Kwa mujibu wa taarifa za msemaji wa vyombo vya habari Vatican kwa waandishi wa habari amebainisha kuwa katika mazungumzo yao, wamefurahishwa na uhusiano mzuri uliopo na kuimarishwa kwa kati ya Vatican na Kenya. Na katika muktadha huo haikukosekana kusisitizia mchango mkubwa wa Kanisa katoliki unaolewa kwa ajili ya wema wa jamii yote ya Kenya kwa namna ya pekee katika huduma za kibinadamu hasa zaidi katika sekta ya elimu, afya na huduma za kijamii.

Katika kuendelea na mazungumzo hayo pia wametazama kwa pamoja hali halisi ya sasa ya Nchi na mchango ambao unatolewa kwa ngazi ya Bara zima  na kimataifa. Vile vile wagusia mada nyingine za pamoja miongoni mwake ni janga la sasa la corona katika nchi hiyo na kwa ulimwengu kwa ujumbala, mabadiliko ya tabianchi na masuala ya wahamiaji. Hawakukosa kama kawaida kubadilisha zawadi kwa pande zote mbili. 

 

06 November 2020, 15:42