Tafuta

Vatican News
2020.09.16 Mons. Janusz S. Urbańczyk, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika makao ya OSCE 2020.09.16 Mons. Janusz S. Urbańczyk, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika makao ya OSCE  

Mons.Urbanczyk asema kuna haja ya ujumuishwaji na kulinda utakatifu wa maisha!

Ujumuishwaji wa wote na kulinda utakatifu wa maisha ya binadamu katika wakati huu wa dharura ya kiafya ndiyo ilikuwa moyo wa hotuba ya Monsinyo Janusz Urbanczyk,mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Baraza ka Usalama OSCE huko Vienna wakati wa mkutano wao wa Mediterranea 2020.

Na Sr. Angela Rwzaula - Vatican

Monsinyo  Janusz Urbanczyk, mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika makao ya OSCE huko Vienna  akizungumza tarehe 3 Novemba kwenye Mkutano wa Bahari ya OSCE 2020, kuhusu mada ya  “Kuhamasisha usalama katika eneo la Mediterranea ya OSCE kupitia maendeleo endelevu na ukuaji wa uchumi”, kwanza ametaka kusisitiza jinsi masuala ya usalama lazima yashughulikiwe kwa njia kamili , kwa kuzingatia masuala kama usalama wa nishati, mabadiliko ya hali ya hewa, uhamiaji na shida ya sasa ya kiuchumi na kifedha iliyozidishwa na janga la Covid-19.

Mara nyingi kiwango cha ukuaji wa uchumi wa nchi ndiyo sababu pekee inayozingatiwa katika maendeleo, lakini maendeleo yanayozungumza hayawezi kuzuiwa kwa ukuaji wa uchumi peke yake mesisitiza. Kiukweli, ili iwe halisi, lazima ipendelee maendeleo ya kila mtu na ya mtu mzima. Kwa kukazia amesema “ Hatuwezi kutenganisha uchumi na ukweli wa kibinadamu au maendeleo tofauti na ustaarabu mahali unapotokea. Monsinyo Urbanczyk, kwa maana hiyo kwa kuzingatia tafakari hizi, kwenye hotuba yake amezungumzia juu ya aina mpya za umaskini zilizoundwa na janga la Covid-19,ambazo  amesema hazikuongezaumaskini tu uliopo, lakini pia imeongeza wengine. Vile vile amezungumza  juu ya mapungufu ya mifumo yetu ya afya, ukosefu wa upatikanaji wa habari sahihi na elimu, mateso yanayosababishwa na kutengwa kwa jamii, kuongezeka kwa vurugu na shida.

Monsinyo katika hotuba hiyo ameonesha pia jinsi ilivyo hali halisi ya wanawake wote ambao wameathiriwa zaidi na athari za janga hilo, akikumbuka jukumu muhimu lililochukuliwa katika uchumi na katika jamii kwa ujumla. Ndiyo ambao wana kazi nzito zaidi, pamoja na kufanya kazi , msaada, kazi za nyumbani, likizo bila malipo, au kupata hasara ya kazi yenyewe. Wajibu wa serikali kwa maana hiyo ni kulinda hadhi yao na kuwapa mfumo wa ulinzi wa kijamii na fidia ya kutosha, katika jamii ambayo imeonyesha usawa mkubwa katika wakati huu wa janga.

Ujumuishaji wa wote na ulinzi wa utakatifu wa maisha ni kanuni mbili madhubuti, kulingana na kiongozi huyo, ambayo sera za serikali zinapaswa kutegemea, kusaidia wahitaji zaidi katika dharura hii ya kiafya, kutumia fursa inayotolewa na janga hili kutafuta suluhisho mpya na ubunifu unaolenga faida ya wote na maendeleo fungamani ya binadamu wote.

04 November 2020, 16:00