Tafuta

Majumba ya makumbusho na Bustani za Kipapa vitabaki vimefungwa kwa umma hadi tarehe 3 Desemba kutokana na kufuata kanuni zilizotolewa. Majumba ya makumbusho na Bustani za Kipapa vitabaki vimefungwa kwa umma hadi tarehe 3 Desemba kutokana na kufuata kanuni zilizotolewa. 

Majumba ya makumbusho Vatican na Bustani za Kipapa zinafungwa kwa umma!

Uamuzi huo umechukuliwa kufautana na uratibu na hatua zilizotolewa na mamlaka ya Italia ili kikabiliana na hali ya kiafya.Uamuzi huo unaanza kutumika kuanzia tarehe 5 Novemba hadi Desemba 3.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Makumbusho ya Vatican, Jumba la kumbukumbu la Majumba ya Kipapa na Ofisi ya Uchimbaji vitafungwa kwa umma tangia siku ya  Alhamisi tarehe  5 Novemba 2020, kama tahadhari, hadi Desemba 3 ijayo. Hivi ndivyo Ofisi ya Waandishi wa Habari Vatican walivyotangaziwa. Jumba la kushangaza la makumbusho la Vatikani ilifunguliwa tena kwa umma mnamo Juni mwaka huu mara baada ya karibu miezi mitatu ya kufungwa kwa sababu ya janga la covid-19.

Ufunguzi huo ulikuwa umewekwa ishara na ubunifu muhimu, kama vile ukarabati wa ukumbi wa Costantino, moja ya vyumba vinne vya Raphael. Na juu ya yote  alikuwa amesisitiza Dk. Barbara Jatta, mkurugenzi wa Makumbusho ya Vatican katika fursa hiyo akiwa amesindikizwa na roho mpya ya upyaisho wa kushirikisha.

Hivi karibuni katika Uwanja wa Pigna, katika moyo wa Makumbusho ya Papa na makutano ya ziara zote, walikuwa wamekarabati Pigna ya shaba, ambayo ni sanaa muhimu kwa umma katika Roma ya kifalme ya karne ya kwanza baada ya Kristo, ambayo ilikuwa imekamilika, na hadi 1600 katika ukumbi wa Kanisa Kuu la  Constantinian ya Mtakatifu Petro. Baada ya zaidi ya miezi kumi ya kazi, ilikuwa imesafishwa na kulindwa kutokana na mawakala wa anga kama mji mkuu wa Kirumi ambao ndiyo msingi wake. Ukarabati huo ulianza kabla ya mwisho wa 2019, na ambapo baadaye ulipunguza kasi yake kutokana na karantini za  janga la Covid-19.

04 November 2020, 16:09