Tafuta

2020.03.27 Kardinali Luis Antonio Tagle 2020.03.27 Kardinali Luis Antonio Tagle  

Kardinali Tagle awaalika waamini wasome Waraka wa Fratelli tutti!

Kardinali Tagle,rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na wa Caritas Internationalis amewashauri waamini kutafakari kwa kina Waraka mpya wa Papa Francisko wa'Fratelli tutti' kwa ajili ya kujifunza vema kupenda kwa dhati,ulimwengu na bila hukumu.Amesema hayo katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Sr. Angela Rwezaula-Vatican.

Caritas Internationalis imeandaa mkutano kwa njia ya Mtandao kwa kuongozwa mada “Fratelli tutti, yaani wote ni Ndugu, kwa kutilia umakini zaidi mafao yako kwa ajili ya kazi ya shirika. Lengo la Mkutano  lilikuwa ni kufanya ufumbuzi zaidi katika Waraka wa Papa ili uweze kugeuka kweli kuwa hali ya dhati kwa ajili ya jumuiya yote ya ulimwengu. Kardinali Luis Antonio Tagle, Rais wa  Caritas Internationalis, kwa maana hiyo anawatia moyo wote kusoma kweli waraka huo wote, kwa sababu amesema: “Papa Francisko analeta baadhi ya mawazo yake yaliyo tangulia katika ufupisho mpya kama jibu la hali ya sasa ya ulimwengu uliofungugwa” na kuongeza kusema, “anafanya hivyo kwa kuchota daima katika  utajiri wa utamaduni wa biblia ya Kanisa,  mafundisho maadili namafundisho jamii ya Kanisa”

Kardinali Tagle katika mwendelezo wa tafakari ambainisha juu ya huzuni mwingi wa ishara za ukosefu wa upendo ambao  unaendelea kutesa ulimwengu. “ Tunaweza kweli kutazama wazi idadi kubwa za maonesho ambayo yanaonesha jinsi ulimwengu unaendelea kujifungia binafsi. Na kutokana na ulimwengu huo kufunguwa ndiyo maana sisi sote tunateseka, lakini maskini wanateseka zaidi. Ni wale ambao ambao wanasahulika kwa upesi, wanadharauliwa, wanatupiliwa mbali na kila mmoja anapaswa achukie matokea hayo mabaya ya ulimwengu uliofungwa, na hasa kwa kuzingatia kuwa matokeo hayo yanaukumba ubinadamu wote hata  katika wakati ujao na juu ya kazi ya uumbaji”.

Kardinali Tagle kadhalika ametoa msisitizo juu ya mantiki mbili msingi zilizomo katika Waraka wa Fratelli tutti. Msingi wa kwanza ni upendo wa ulimwengu, kwa sasbabu ameeleza kwamba ‘Fratelli tutti’ picha yake ya upendo ni ile ya  upendo wa ulimwengu maana ndivyo Mungu anavyopenda. Mungu anapenda wote. Ndiyo upendo ambao Yesu anaonesha. Yeye alipenda wote na zaidi wale ambao katika jamii ilikuwa inawafikiria kutopendwa, waliopembezoni. Mfano wa Msamaria Mwema unaonesha wazi hali hiyo na katika upendo wa ulimwengu kulekea mgeni.

Msingi wa Pili aliousisitiza amesema unahusu uhusianoa wa  Utamaduni wa kukutana. Upendo wa ulimwengu, unaweza kwa urahisi kuangukia katika   kauli mbiu tu, na kumbe  ulimwengu unawezi kuwa halisi ikiwa unasindikizwa na kukutana na matendo ya kweli. Amekumbusha kardinali kwamba Papa mara nyingi anarudia kusema kwa,  ikiwa mtu atashiriki katika mazungumzo, lazima pia ajue utambulisho wake mwenyewe ili asiukane. Vivyo hivyo, kila taifa lina haki ya mfumo wake wa kisiasa, lakini siasa za kitaifa lazima ziongozwe kwa misaada sera za siasa kimataifa.

Tumaini lililooneeshwa na Kardinali Tagle ni kwamba kupitia utamaduni wa kukutana itawezekana kweli kupata njia bora ya kufanya sera za siasa, kushughulikia uchumi, kutafuta njia bora ya kuanzisha urafiki wa kiutamaduni na kusuluhisha mizozo. Yote hayo yanapelekea wema  ustawi wote.  Na itakuwa wema wa wote ambao hatimaye utanufaisha hata mtu binafsi. Hatimaye Kardinali Tagle ameonesha baadhi ya mafunzo ambayo Caritas inaweza kujifunza kutokana na Waraka wa ‘Fratelli tutti’ yaani  ‘wote ndi Ndugu’ pamoja na ile ya kuuungana na Baba Mtakatifu katika kufahamu na kuonya juu ya ishara za kufungwa kwa mioyo, mikono, akili, maeneo na utamaduni. Ishara hizi ni finyu mno, lakini waraka wa Fratelli tutti, yaani wote ni Ndugu unatuomba tufungue macho yetu na tuwe wenye kudai, nyeti katika mitazamo ambayo badala yake inaonesha uwazi wa ulimwengu wote.

13 November 2020, 17:07