Tafuta

2020.11.19 Kardinali  Pietro Parolin azungumza katika mkutano " kamwe hakuna tena" 2020.11.19 Kardinali Pietro Parolin azungumza katika mkutano " kamwe hakuna tena" 

Kard.Parolin:inawezekanakutokomeza chuki dhidi ya wayahudi kwa

Katika hitimisho la Mkutano kwa njia ya mtandao ulioandaliwa na Ubalozi wa Marekani jijini Vatican,kuchambua kuongezeka kwa chuki dhidi ya Wayahudi na jinsi gani ya kuweza kutokomezwa kupitia mazungumzo ya kidini ndiyo ilikuwa kiini cha mazunguzo yake Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican.

Kardinali Pietro Paroli Katibu wa Vatican ametoa hotuba katika hitimisho la Mkutano kwa njia ya mtandao ulioandaliwa na Ubalozi wa Marekani jijini Vatican kwa kuchambua kuongezeka kwa chuki dhidi ya Wayahudi na jinsi gani ya kuweza kutokomezwa kupitia mazungumzo ya kidini. Katika hitimisho la mkutano uliondaliwa na Ubalozi wa Marekani jijini Vatican kwa njia ya mtandao, kwa kuongozwa na mana ya “mbele ya kuongezeka kwa chuki dhidi ya wayahudi ulimwenguni kamwe usirudiwe tena. Ni mkutano uliofanyika mchana katika jengo Ubalozi wa Marekani Vatican. Katika  mkutano huo “Kardinali Pietro Parolin, ametoa hotuba yake akisisitizia juu ya mazungumzo ya kidini kuwa ya lazima dhidi ya chuki hizi dhidi ya wayahudi. Ameunga mkono maneno ya Papa Francisko, akikumbuka kwamba aina yoyote ya chuki dhidi ya Wayahudi ni “kukataa asili yetu ya Kikristo”, na kwa maana hiyo ni kupingana. Waraka wa Fratelli tutti unatoa tafakari, juu ya upotoshaji wa “dhana za kimsingi” kama demokrasia, uhuru, kutojali, “upotezaji wa maana ya historia” na ubaguzi wa rangi ambao pia unaonyeshwa katika chuki dhidi ya Uyahudi.

Katika hotuba hotuba yake, Kardinal ametaja  hata barua iliogunduliwa hivi karibuni, ya mtangulizi wake Katibu wa Vatican wa wakati ule Kardinali Gasparri. Katika hati hiyo Ilikuwa imeandikwa katika mantiki ya  kutoa jibu la barua ya Kamati ya Kiyahudi ya Marekani ambayo ilikuwa inaomba jibu kuhusiana na vurugu dhidi ya wayahudi katika mantiki ya vita ya kwanza ya dunia. Akiandika kwa niaba ya Papa Benedikto  XV, Kardinali  Gasparri aliandika kwamba haki za asili za mwanadamu zinapaswa kuzingatiwa na kuheshimiwa pia kwa uhusiano na watoto wa Israeli kama inavyopaswa kuwa kwa watu wote, kwa sababu haingekuwa sawa na haki na dini yenyewe kwa sababu tu ya tofauti katika imani ya kidini. Kardinali aidha ametaja majibu ya barua hiyo ya Kamati ya Kiyahudi ya Marekani ambayo iliiita “waraka wa kiutendaji akionyesha kwamba “Kati ya maandishi yote ya  kipapa ayaliyowahi kutolewa dhidi ya Wayahudi katika historia ya Vatican, hakuna uthibitisho ambao unalingana na mahitaji haya ya moja kwa moja yanayoomba usawa kwa Wayahudi, na dhidi ya chuki kwa misingi ya kidini.

Kardinali Parolini pia amesisitia mahali pa kumbu kumbu ya kihistoria kwa kuthibitisha kwamba ili kushinda aina nyingi za kusikitisha za chuki tunahitaji uwezo wa kujihusisha pamoja katika kumbukumbu. Kumbukumbu ni ufunguo wa kufikia siku za usoni na ni jukumu letu kulipitisha kwa njia ya heshima kwa vizazi vijavyo. Katibu wa Vatican  amemalizia kwa kusisitiza kuwa mazungumzo ya kidini ni zana muhimu kwa kupambana dhidi ya ubaguzi wa  wayahudi. Udugu,ni iliyojengwa juu ya ukweli uliothaminiwa na dini ambayo  kila mtu ameitwa kuwa mwana wa Mungu. Ni matumaini yake kwamba Wakristo na Wayahudi  wanaweza kukua katika udugu, urafik kijamii na mazungumzo, na wale wanaopinga Uyahudi itawezekana kwa sababu 'udanganyifu upo akilini mwa yule anayepanga uovu, lakini anayeshauri amani ana furaha' (Mithali 12:20).

20 November 2020, 16:13