Tafuta

2020.11.28 Kusimikwa kwa Makardinali wapya 13 2020.11.28 Kusimikwa kwa Makardinali wapya 13 

Kard.Grech:Ikiwa watu watakatifu wa Mungu wanatembea pamoja hawakosei njia

Katibu wa Sinodi ambaye amesimikwa kuwa Kardinali wakati wa maadhimisho hayo ametoa shukrani kwa Papa Francisko kwa niaba ya makardinali wateule.Ni muhimu kusikiliza watu wa Mungu na katika kutembea kwa pamoja siyo rahisi kukosea njia amefafanua kardinali katika kutoa mwongozo wa kile ambacho kinaweza kufanyika katika Kanisa la ulimwengu kwa kufuata maelekezo ya Papa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika salam za Kardinali mpya Mario Grech ambaye ambaye ni Katibu wa Sonodi ya Maaskofu kwa niaba ya makardinali wote wateule amezungukia juu ya utume wa Kanisa ambalo amesema ni sakramenti ya wokovu wa ulimwengu ambalo linaitwa kufungua njia hata lenyewe kujikita katika njia hizo, yaani Kanisa linalotoka nje. Ikiwa watu watakatifu waamini wa Mungu wanatembea pamoja, hawakosei  kwa sababu wale waliobatizwa wanatumia ule uwezo usioshindwa wa imani kwa namna imani ambayo amemtaja Papa kuwa  daima amekuwa akisisitiza na kuhimiza  kuomba Roho Mtakatifu ili Kanisa lipate kusikiliza na kufanya mang’amuzi ya kile ambacho linaambiwa, na kwa maana hiyo kuwa wazi kwa Mungu na ukweli wake daima.

Wakati wa tukio la kusimikwa Makardinali wapya
Wakati wa tukio la kusimikwa Makardinali wapya

Akitazama masuala ya Kanisa katika muungano, ametafsiri  Sinodi ya maaskofu kama zaidi ya tukio lakini ni mchakato ambao unahusisha mkakati mzima wa watu wa Mungu,  Baraza la Maaskofu na Askofu wa Roma, kila mmoja kwa kadiri ya utendaji wake hasa kuoa  nafasi muhimu kwa ajili ya watu wa Mungu. Kardinali Grech amesisitiza juu ya umuhimu wa kusikiliza na katika mkutano ambao unawekwa kwa ngazi ya maisha na utume wa Kanisa kama mwenendo na mzunguko wenye kuleta matunda. Makanisa mahalia, majimbo, na Kanda za  kikanisa , Kanisa la ulimwengu ambamo kuna hata Baraza la Makardinali linatoa sehemu yake, na wote wamewekwa katika mchakato wa kisinodi ambao unajionesha katika umoja unaongoza maamuzi ya kikanisa.

Kardinali Mario Grech akitoa shukrani kwa Papa
Kardinali Mario Grech akitoa shukrani kwa Papa

Kwa njia hiyo Kardinali amesema wamewathibitishia umuhimu wa kusikiliza. Na ambapo kwa hakika amependa kuwa nafasi ya ukatibu inaweza kufanya zaidi. Shughuli ambayo ameibainisha pia ni tumaini lake , kwa mfano kuweza kusaidia maaskofu na mabaraza ya maaskofu katika ukomavu wa mtindo wa kisinodi bila kuingilia kati, lakini kwa kuwasindikiza katika michakato inayo endelea kwa ngazi mbali mbali ya maisha ya kikanisa, kwa ushiriki katika Kanisa linalotoka nje. Na zaidi katika kipindi hiki ambacho tunapitia, Kanisa bado linahitajii kuwa skramenti ya wokovu ulimwenguni(LG 48).  Na kwa mtazamo huo wa fadhila ya matumaini ndiyo hitimisho na salam za mwanzo wa makardinali hao wapya. Matumaini ambayo Roho Mtakatifu kwa nyakati hizi ngumu zilidhaniwa kama Peguy kuwa ni  dada wawili wadogo  ambao ni imani na upendo, lakini kama yule anayevuta baada ya dada wengine wakubwa.

Papa akitafakari kwa ukimya
Papa akitafakari kwa ukimya
28 November 2020, 19:05