Tafuta

2020.11.06 Mipine katika Bustani za Vatican 2020.11.06 Mipine katika Bustani za Vatican  

Bustani za Vatican:Jaribio la kiasili la kuthibiti bakteria za miti imefanikiwa!

Wataalam wa huduma ya bustani wamefanikiwa jaribio la dawa yenye nguvu ya kuua bakteria na ya asili ambayo inalinda miti ya mipine,iliyoathiriwa na vimelea hivyo iwe Roma hata katikati-kusini mwa Italia,kutokana na aina ya mdudu kama gamba la kobe.Uendelezaji wa mbinu za asili zilizopitishwa na Vatican zilizoongozwa na misingi ya Waraka wa‘Laudato si.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Dawa ya kibaolojia dhidi ya aina kimelea kama ganda kobe imejaribiwa na kuleta ufanisi katika Bustani za Vatican, ambayo imetafsiriwa kama sindano inayookoa miti. Gamba kobe ambalo linaharibu miti ya mipine ya Vatican, Roma na miji mingine mingi Kusini mwa Italia, ina masaa yaliyohesabiwa wanasema. Imethibitishwa kuwa ni viungo vingine vyenye kazi kwa namna ya pekee katika vile vilivyomo kwenye mafuta ya mwarobaini, na ni dawa yenye nguvu ya kuua bakteria na kuharibu wadudu. Ni njia ya kibaiolojia ambayo inaweza kutekelezwa kwa heshima kamili ya mazingira. Majaribio ya kwanza ya kutia moyo kumaliza hivyo vimelea ni sehemu ya mpango uliozinduliwa mnamo Septemba 2017 na Huduma ya Bustani (sasa Bustani na Mazingira) ya Serikali ya Jiji la Vatican. Katika kujibu ombi la Laudato si ', mchakato wa kuondoa taratibu  vile vimelea hivyo ili kulinda  miti wametumia mbolea  ya mimea za bustani, kwa maana walibadilisha bidhaa za asili na mbinu za kilimo zilizo na athari za mazingira. Haya yameelezwa na mhusika mkuu Rafael Tornini, ambaye katika mahojiano hayo  na  Gazetti la “Osservatore Romano” amesimulia juu ya mafaniko kwamba  matokeo ya majaribio ni bora.

Awali ya yote akianza kusimulia amesema Mpango huo wa Bustani ya asili, ilitegemewa kumalizika kati ya mwaka 2022, lakini lengo hilo sasa limetimilizika mjini Vatican kabla ya muda wake. Kiukweli, vimelea hivyo huondolewa kwa ujumla kutokana na kuweka  dawa za asili na mbolea za kibaiolojia zilizothibitishwa na asili. Mazoezi ya kupalilia na kemikali, ambayo mara nyingi baadhi yana athari kubwa kwa mazingira, yameondolewa kabisa, huku wakifanya mazoezi ya kudhibiti magugu peke yake na njia za kiufundi na bidhaa za asili kama asidi ya pelaronic.

Akielezea vimelea hivyo amesema ni mdudu ambaye hukaa kwenye matawi na ana uwezo wa kuzaa sana. Katika kipindi cha msimu wa karibu na joto, yaani majira ya kuanz joto, kwa kuzingatia lishe yake, inakula juu ya utomvu wa matawi machanga yaliyowekwa kwenye kilele cha mpine ikitoa kioevu cha sukari kinachoitwa “asali ya kisaikolojia”. Katika hali nyingine, inadondosha chini kutoka juu, huku ikipaka kila kitu kilichopo chini yake. Tundu la asali pia huwa linajisambaza kwenye sindano, na kuwa kama tovuti ya ukuzaji wa kuvu nyeusi, ambayo inasababisha kupunguzwa kwa usanidimlo wa klorophyll, na kusababisha kukausha kwa sindano na kuzorota kwa mmea, hadi kusababisha kifo chake ndani ya miaka miwili au mitatu tu.

Kwa maana hiyo katika jaribio hili matokeo ni mazuri sana  kwani  ni ufanisi wa viungo vyote vitatu ambayo vimejaribiwa hasa cha Abamectin ambacho kimeonyesha shughuli kubwa ya vimelea. Kwa kuchunguza sampuli ya watu 126, waliotumia na ambaowamepata matokeo ya ufanisi wa asilimia 95.24 ya kifo cha aina hii ya ganda kobe. Hata hivyo kwa namna ya pekee inastahili kutajwa Azadirachtin, aina ya kinga inayotumika ya mafuta ya mwarobaini, dawa ya asili inayojulikana ya wadudu na acaricide, ambayo matokeo yake yana ufanisi wa takriban asilimia 80 ya kifo cha vimelea hivyo. Ni wazi kwamba pamoja na ufanisi huo lazima itakuwa kipaumbele cha kuendelea kutathmini ufanisi huu kama kinga inayotumika ya kibaolojia na kulingana na mpango wa sasa, sambamba na Abamectin.  Haya ni mambo ambayo yanatumika na ambayo yataendelea kujaribiwa kwa sasa katika mimea ya mipine na juu ya yote, uendelevu wake kwa suala la ulinzi wa viumbe muhimu na wachavushaji, ambayo ni wadudu wanaosafirisha poleni kutoka ua moja hadi lingine, amehimitisha.

07 November 2020, 15:43