Tafuta

  Wakristo wakatoliki nchini China Wakristo wakatoliki nchini China  

Askofu mpya aliyeteuliwa nchini China ni chini ya mkataba wa muda

Ni Tommaso Chen Tianhao,ambaye ataongoza Jimbo la Qingdao.Ni kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican Dk,Bruni amnaye ametoa taarifa kwa waandishi kuwa "michakato kwa ajili ya uteuzi wa maaskofu inaendelea na wengine wanatarajiwa katika siku zijazo".

VATICAN NEWS

Mkataba wa muda kati ya Vatican na Jamhuri ya Watu wa China umezaa matunda. Askofu mpya  wa tatu tangu makubaliano hayo yasainiwe mnamo Septemba 2018, ameteuliwa kwa ajili ya muungano na Mfuasi wa Petro na amewekwa wakfu. Hii imethibitishwa na Msemaji wa vyombo vya habari Dk. Matteo Bruni kwa waandishi wa habari.

Kuhusu habari za kuwekwa wakfu askofu huko Qingdao (mkoa wa Shandong), Dk. Bruni amesema: “Ninaweza kuthibitisha kwamba Mhs. Thomas CHEN Tianhao ndiye askofu wa tatu aliyeteuliwa na kuwekwa wakfu katika mfumo wa udhibiti wa Mkataba wa Muda kati ya Vatican na Jamhuri ya Watu Wachina kuhusu uteuzi wa maaskofu”. "Ninaweza pia kuongeza amesema msemaji wa vyombo vya habari, akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari kwamba, hakika wengine maaskofu wanatawazamiwa kuwekwa wakfu kwa siku za usoni kwa sababu michakato ya uteuzi mpya wa maaskofu inaendelea”.

Kama inavyokumbukwa kuwa, Mkataba wa Muda, uliopyaishwa  kwa miaka mingine miwili katika wiki za hivi karibuni, hautazami uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na China, wala hali ya kisheria ya Kanisa Katoliki la China au uhusiano kati ya makasisi na mamlaka ya nchi.  Makubaliano ya muda yanahusu mchakato tu wa kuwateua maaskofu: ni moja ya suala muhimu katika maisha ya Kanisa na katika muungano wa wachungaji wa Kanisa Katoliki la China na askofu wa Roma  na maaskofu wa ulimwengu. Lengo la Mkataba wa Muda limekuwa kiukweli la kichungaji daima. Lengo lake ni kuwaruhusu waamini Wakatoliki kuwa na maaskofu ambao wako kwenye muungano kamili na Mfuasi wa Mtakatifu Petro na wakati huo huo wanatambuliwa na mamlaka ya Jamhuri ya Watu wa China.

25 November 2020, 16:34