Tafuta

VATICAN: PAPA FRANCISKO NA ASKOFU MKUU WA CANTERBURY  JUSTIN WERBY VATICAN: PAPA FRANCISKO NA ASKOFU MKUU WA CANTERBURY JUSTIN WERBY 

Ask.Mkuu wa Canterbury:Wakristo waungane katika kipindi cha janga

Katika mahojiano na Mkuu wa Kanisa la Kianglikani Askofu Mkuu Justin Welby na Vatican News,amezungumzia juu ya changamoto zilizowakumba wakristo na dharura ya virusi vya corona,umuhimu wa Waraka wa Fratelli tutti kwa ajili ya harakati ya kiekumene na matumaini ya amani kwa ajili ya Sudan Kusini.

VATICAN NEWS

Mwaka mmoja uliopita, tarehe 13 Novemba 2019, Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby alikutana na Papa Francisko mjini Vatican. Miezi kumi na moja baadaye, hali halisi ya ulimwengu imebadilika kabisa kutokana na janga. Pamoja na mlipuko mkubwa wa virusi vya Covid-19 mada kubwa za mshikamano wa ekolojia, uhuru wa dini na amani haujapungua lakini badala yake umeimarishwa zaidi na ambao umeonesha kwa kiasi kikubwa maelewano fulani kati ya Askofu wa Roma na Mkuu wa Kianglikani. Mwaka mmoja baada ya ziara hiyo na zaidi ya mwezi mmoja baada ya kuchapishwa kwa Waraka  wa “Fratelli tutti yaani”  “wote ni Ndugu”, Askofu Mkuu Welby amekubali kufanya  mahojiano kwa  jumla na Osservatore Romano na Vatican News juu ya masuala ya mada ya sasa akianzia na kutafakari ya  mchango ambao Wakristo wanaweza kuutoa kwa wakati huu ambao umekumbwa kwa kina na mateso. Akijibu swali ni kitu gani viongozi wakristo kama Yeye na Papa wanaweza kufanya ili kuhamasisha matumaini katika kipindi cha woga na mateso duniani, amesema awali ya yote “ matumaini ni Yesu Krsito ambaye  ni  wa jana leo na daima ( Wab 13,8). Wakati huu  ulimwengu unaweza kubadilika, kwani upendo wa Mungu kwa njia ya Kristo haujazima. Fadhili za mwenyezi Mungu hazikomi (maombolezo 3, 22). Jukumu  kwa wale wanaoongoza Kanisa ni kushuhudia matumaini katika kipindi kigumu. Yesu hakuja kuleta matumaini katika ulimwengu ambao mambo yake yanakwenda vizuri, bali katika ulimwengu ulio dhaifu na kumegeka; ulimwengu uliojaaa watu dhaifu, wenye majeraha na wadhambi. Kile ambacho Yesu anatwambia  ni kwamba “ tusiogope. Yeye ni tumaini letu”, amethibitisha Askofu Mkuu.

Akendelea amesema Wakristo wanaalikwa kuwa watu wa matumaini wanaoonesha kwa namna ambayo wanaishi pamoja kama jumuiya. Ujumbe wa Matumaini katika Kristo unatazama zaidi ya upeo wa hapa, na saa, kwani utazama kile ambacho kitakuja, unatazamia  ahadi ya maisha ya milele. Maisha ya binadamu ni dhaifu, magojwa, na vifo vilivyotokea  vinatufanya tutambue  vema janga lilivyo baya. Pamoja na hayo maisha ya milele ndiyo hayo. Mungu anatuonesha  kana kwamba maisha ya dunia yanaangaze vema yale ya mbinguni, kwa sababu moja linaongoza jingine. Kwa kufuata mfano wa Yesu na mafundisho yake ya kupenda jirani, tunaweza kuchangia kufanya  vizuri. Ikiwa tutaishi kwa imani katika Kristo na kuweka katikati walio dhaifu zaidi, maskini na walitupwa pembeni huo ndiyo ujumbe wa matumaini, amesisitiza Askofu Mkuu Welby.

Katika swali  kwa Askofu Mkuu ili kuelezea kile  kilichomgusa sana katika  ujumbe wa Papa Francisko unaojikita katika Udugu na urafiki kijamii, amesema ni ujumbe wa nguvu na ambao unapendekeza maono ya kimfumo, kabambe na ujasiri kwa ulimwengu ulio bora wa baadaye. Ujumbe huo una msingi thabiti wa elimu ya Kristo (Christology), na Kristo katikati. Pia ni barua ambayo inazungumzia kwa umakini ukubwa na ugumu wa ubinadamu. Marejeo ya Papa juu ya mikutano yake na watu kama vile Patriaki wa Kiekumene, na Imam mkuu, msukumo anaoutoa kutoka kwa Mahatma Gandhi, na marejeo mengine kutoka kwa  Dk. Martin Luther King Jr na Askofu Mkuu Desmond Tutu kwa dhati yanaonesha kuwa maono yake siyo tu kwa ajili ya Kanisa Katoliki, lakini kwa ubinadamu wote; na moja ya sababu ya maono yake ni ya kutamani pia kuamini.

Askofu Mkuu vile vile akijibu kuhusu mchango gani unaweza kutolewa katika harakati za kiekumene kutokana na sala ya mwisho inayomalizia Waraka wa Fratelli tutti, amesema kuwa moja ya shida  inayowasumbua Wakristo wengi ni wazo kwamba Kanisa lao ndilo kiungo pekee cha Kikristo kilichopo, au, ikiwa wanatambua uwepo wa Wakristo wengine, basi wanafikiria kuwa kiukweli hao wanakosea. Hii inawatazana mara kwa mara Waanglikani, lakini pia kwa wengine. Tunapoangalia kaka na dada wa Kikristo ambao tumetengana nao kwa sababu ya tukio la kihistoria au masuala ya mafundisho, tunaona watu wa kweli wa Kristo, mahujaji wengine wakiwa njiani na watu, waliopendwa na Mungu na kutumikiwa na Mungu, ambaye tunaweza kujifunza kutoka kwao.

Kwa kutoa mfano wamekumbusha Wimbo wa Kiingereza unaosema:

Katika Kristo hakuna mashariki wala magharibi,ndani yake hakuna kaskazini au kusini, lakini kampuni kubwa ya upendo katika ulimwengu wote mkubwa.

Ndani yake mioyo ya dhati kila mahali watapata ushirikiano wao mkuu;

huduma yake ni uzi wa dhahabu, ambayo hufunga ubinadamu kwa nguvu.

Kwa hivyo unganisha mikono, watoto wa imani, na kila kabila mtokako;

anayemtumikia Baba yangu kama mwanae hakika ni mwanafamilia wangu. (Wimbo wa John Oxenham, 1908).

Akiendelea ma mahojiano hayo, amani, ecolojia na haki kijamii ni mada ambazo yeye pamoja na Papa Francisko wamekazania sana, na zaidi suala la kukutana na viongozi wa Sudan Kusini, kwa maana hiyo  matumaini yake ya wakati ujao kuhusu uhusiano wake na Papa  kwanza amesema anashukuru sana urafiki wake na Papa  Francisko. Walianza huduma yao karibu wakati huo huo, na kwamba “tunashirikiana mambo mengi ya pamoja. Kwa wote, amani na upatanisho ni muhimu”. Mafungo ambayo Papa Francisko na Yeye walishirikiana na viongozi mbali mbali wa kisiasa wa Sudan Kusini, amethibitisha “ leo ni moja wapo ya uzoefu mkubwa sana maishani mwangu.  Suala la kuweza kusafiri pamoja kwenda Sudan Kusini bado ni tumaini halisi. Kufikia sasa haijawezekana, lakini Makanisa, Katoliki, ya kianglikani na kipresbyterian, nchini Sudan Kusini na kwa ngazi ya  kimataifa, wameendelea kufanya kazi kwa ajili ya amani na siku zijazo za haki ya  kudumu zitafika katika nchi hiyo”. “Ni matumaini yangu kwamba, wakati itawezekana kusafiri tena, kutakuwa na maendeleo kama hayo katika mchakato wa amani wa Sudan Kusini na kwamba tutaweza kwenda huko kusherehekea na kuhamasisha  kuongezeka kwa amani na ukuaji katika jamii”.

17 November 2020, 18:49