Tafuta

2014-12-17 Mons Ivan Jurkovic 2014-12-17 Mons Ivan Jurkovic 

Askofu Mkuu Jurkovič: hakuna mazungumzo bila heshima ya hadhi ya binadamu

Katika hotuba yake nchini Saudi Arabia katika fursa ya uwakilishi wa kitabu kuhusu mazungumzo ya kidini, Mwakilishi wa Kidumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa mataifa zilizoko jijini Geneva Uswiss Askofu Mkuu Ivan amesisitiaia njia ya udugu ambao ni mantiki muafaka na halisi kwa ajili ya kuishi na uhusia wa nguvu unaunganisha haki, hadhi ya binadamu na amani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Askofu Mkuu  Ivan Jurkovič, mwakilishi wa kiudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa mataifa jiji Genea, hivi karibuni tarehe 22 Novemba 2020 wakati wa kutoa hotuba yake huko Jeddah, nchini Saudi Arabia wakati wa uwakilishi wa  kitabu kiitwacho “ uhamasishaji wa mazungumzo kiutamaduni na kidini”, kama chombo cha amani na udugu, ameelezea shukrani yake kwa waandaaji wa tukoi hilo. Vile vile hata kwa ajili ya mchango wa kuchapishaji na ambao unapendekezwa kuhamasish mazungumzo kiutamadni na kidini   kama njia ya kuweza kuishi kwa amani na udugu kati ya watu.

Ni kitabu ambacho kinataka kupeleka mbele mchakato ulioanzishwa na  maono ya Sheikh Muhammad bin Abdulkarim Al-Issa, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kiislam Dunia na Papa mjini Vatican miaka mitatu iliyopita  na ziara ya kihistoria ya Marehemu Kardinali Jean Louis Tauran katika nchi hiyo na ambapo inagusa masuala matatu msingi ambayo ni udugu wa kibindamu; haki na mazungumzo kama chombo cha amani.

Akitoa mwaliko wa Shirikisho la Kiislam Duniani na Chuo Kikuu cha Amani ya Umoja wa Mataifa kufanya kazi katika kuchapisha na kwa njia ya majadiliano hayo, Askofu Mkuu Jurkovič ameeleza jinsi gani  wazo lake la kwanza lilivyokwenda katika Hati juu ya ‘Udugu wa kibinadamu kwa ajili ya amani ulimwengu na kuishi kwa pamoja’ iliyotiwa saini na Papa Fracisko na Imam Mkuu wa  Al-Azhar, huko  Abu Dhabi, tarehe  4 Februari  2019.  Hati hiyo ya kuhisotia na ambayo si tu kfikiria watu wa mataifa tofauti, tamaduni na imani lakini pia  inawaalika kufikiria na namna ya kukaa kama watu, ndugu kaka na dada. Kuishi katika jamii zenye tamaduni nyingi na dini nyingi, ambazo tofauti mara nyingi  mzozozo haukosekani” lakini pia kuwa na utambuzi kuwa  undugu ni muhimu”, kama ilivyoonyeshwa tayari na Mtakatifu Paul VI. Na leo, hata zaidi kwa njia ya kifalsafa ya hivi karibuni ya Papa Francisko, katika waraka wake wa Fratelli tutti yaani ‘ wote ni Ndugu’, haujatolewa  kama dhana ya kufikirika  na inayofariji, lakini kama kigezo bora na halisi cha kuishi kwa pamoja”, amesisitiza Mwakilishi huyo wa kudumu wa Vatican.

“Utambuzi wa udugu wa pande zote una uwezo wa kubadilisha, kupindua mzozo na kuwa ujumbe mzito, wenye dhamani ya kidini na hata kisiasa, na pia kuongoza moja kwa moja kutafakari juu ya maana ya uraia. Kiukweli sisi ni kaka na dada, na kwa maana hiyo raua wema na  wote wenye haki sawa na wajibu”, amsisitiza. Lakini kama alivyosema Sheikh Al-Issa  wakati wa ziara yake jijini Geneva  kwamba “Amani haiwezi kupatikana bila haki kamili, haki isiyo na misingi ya kweli inaweza kusababisha amani ya uwongo. Haki inaposhinda, amani inatawala na wakati haki ikikwazwa, amani pia inahatarishwa”.

26 November 2020, 16:59