Tafuta

Askofu Mkuu Paul R. Gallagher Askofu Mkuu Paul R. Gallagher 

Vatican:Jitihada za Vatican katika mahusiano na nchi za nje

Katika hotuba yake,Askofu Mkuu Paul Richard Gallaggher,Katibu wa Vatican wa Uhusiano na Ushirikiano na nchi za Nje katika Mkutano kuhusu Diplomasia ya Vatican,katika fursa ya miaka 40 tangu kutiwa saini ya Mkataba wa uhusiano kati ya Vatican na Peru amesisitiza juu ya jitihada za Vatica katika kurahisha udugu kati ya watu ili kuvunja mitindo ya kutokujali ambayo imezidi kuenea.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Tendo la kidiplomasia la Vatican haliliridhiki na kutazama tukio au kutathmini umuhimu wao na haiwezi kubaki tu kama sauti ya kukosoa dhamiri, na mara nyingi hata nje yake. Kwa maana hiyo kazi ya kidini katika mantiki hiyo ni chombo cha ushirikiano kinachomuunganisha Baba Mtakatifu wa Roma  na Maaskofu wa  Makanisa yote mahalia, pia ni njia ya kipekee ambayo kwa njia hiyo Papa anaweza kufikia  kwa njia ya kiroho na nyenzo za ubinadamu. Ni katika hotuba ya Askofu Mkuu Paul Richard Gallaggher, Katibu wa Vatican wa Uhusiano na Ushirikiano na nchi za Nje katika Mkutano kuhusu Diplomasia ya Vatican, tarehe 6 Novemba 2020. Hii ilikuwa ni katika Maadhimisho ya Miaka 40 tangu kutiwa saini  mktaba wa mahusiano ya kidiplomasia nchini Peru uliofanyika mnamo  tarehe 19 Julai 1980 huko Lima. Askofu Mkuu katika hotuba yake amebainisha kuwa Vatican imeitwa kutenda ili kurahisha namna ya kuishi kati ya mataifa mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha ule udugu kati ya Watu, mahali ambapo neno la udugu linakuwa sawa na ushirikiano hai, wa kweli ambao unaleta maelewano na ulio sahihi katika mmahusiano ya  miundo mbinu kwa ajili ya ustawi wa  pamoja na ule wa binafsi.

Askofu Mkuu katika hotuba hiyo amesema ni Baba Mtakatifu Francisko ambaye anaomba Vatican kusonga mbele kwenye uwanja wa kimataifa na sio kuhakikisha usalama wa jumla, uliofanywa hadi sasa kuwa mgumu zaidi kuliko wakati wowote katika kipindi hiki cha kukosekana kwa utulivu na mizozo, lakini pia ni katika  kuunga mkono wazo la amani kama tunda la mahusiano sahihi, ambayo ni ya kuheshimu viwango vya kimataifa, ya kulinda haki msingi za kibinadamu, kuanzia na zile za wachache,  na walio hatarini zaidi”. Kwa maana hii ni wazi, juu ya kazi ya kidini katika mantiki hiyo  ya diplomasia kama “chombo cha ushirikiano kinachomuunganisha Baba Mtakatifu wa Roma  na Maaskofu wa Makanisa yote mahalia ulimwenguni, pia ni njia ya kipekee ambayo kwa njia hiyo Papa anaweza kufikia kwa njia ya kiroho na nyenzo za ubinadamu”.

Katibu wa Uhusiano na Mataifa amekumbuka kuwa mtandao wa kidiplomasia wa Vatican una uhusiano wa nchi hizo mbili pamoja   na Mataifa  mengine 183, ambayo ni lazima  kuongeza   Jumuiya ya Umoja wa Ulaya na Shirika la Kijeshi la Malta. Pia Vatican inadumisha uhusiano thabiti wa pande nyingi na taasisi zingine nyingi za serikali, zinazofaa katika sekta mbali mbali ambazo muundo wa utawala wa kimataifa umeelezewa. Kulingana na Askofu Mkuu Gallagher, Wazo la amani ambalo Vatican ni mbebaji halisi kwa lile ambalo mataifa yanaelezea katika sheria za kisasa za kimataifa.  “Kufanya kazi kwa ajili ya amani haimaanishi tu kuanzisha mfumo wa usalama wa kimataifa na, labda, kuheshimu majukumu yake. Badala yake hiyo inahitajika pia kuzuia sababu zinazoweza kusababisha mzozo wa vita, na pia kuondoa hali hizo za kiutamaduni, kijamii, kikabila na kidini ambazo zinaweza kufungua tena vita vya umwagaji damu ambavyo vimemalizika hivi karibuni”. Kwa mantiki hii, sheria ya kimataifa lazima iendelee kuchukua hatua, kutafuta vifaa na taasisi za kisheria na vyombo vya udhibiti vyenye uwezo wa kusimamia mizozo ambayo imehitimishwa au hali ambazo juhudi za diplomasia zimelazimisha silaha kukaa kimya”, amesisitiza.

Hatua muhimu katika kuingilia kati kwa Katibu wa Uhusiano na Mataifa ni ile ya awamu ya baada ya vita: Askofu Mkuu Gallagher amesema “Kazi ya baada ya vita sio tu kwa kupanga upya maeneo, kutambua serikali mpya au zilizobadilishwa, au hata kuhakikisha usawa mpya uliopatikana na jeshi. Badala yake, inapaswa kutaja mwelekeo wa kibinadamu wa amani, ikiondoa sababu yoyote inayowezekana kuathiri tena hali ya wale ambao wamepata vitisho vya vita na sasa wanangojea na kutumaini, kulingana na haki, kwa siku zijazo ziweze kuwa tofauti. Na hii ikitafsiriwa kwa lugha ya diplomasia, inamaanisha kutoa kipaumbele cha nguvu ya sheria kulingana na kuwekwa kwa silaha, kuhakikisha haki hata kabla ya uhalali. Askofu mkuu Gallagher aidha katika hotuba yake  ameshutumu kuenea kwa kutokujali hali ambayo amesema  haihusu tu maeneo ya mizozo na vita, labda mbali kijiografia. “Leo hii wote pia tumekumbwa,  tupende, tusipende hilo kwani, tunafikiwa katika maisha yetu ya kila siku na wimbi endelevu la habari na nyingine  za kughushi, ambazo karibu zinatuunganisha na ulimwengu wote na ambazo zinatuonyesha umati wa wagonjwa, watu wasio na nyumba, wahanga wengi wa vita wanaolazimishwa kuhama, watu ambao wamevunjika moyo, wale ambao wamepoteza kazi zao, na watu  wanyonge zaidi”. Na kwa maana hiyo ameseme anao uhakika kwamba leo hii, zaidi ya hapo awali, ni muhimu kuvunja njia hizi za kutokujali, kuvunja ganda gumu la kujilinda ubinafsi wetu na ili  kupitia katika  nadharia juu ya amani inayowezekana, kuingia  katika uzoefu halisi wa amani ya kuishi, hata ikiwa inalazimisha kuteseka.

Njia kuu, Askofu Mkuu  Gallagher anaioonesha ni ile iliyoonyeshwa na Baba Mtakatifu Francisko, ambayo ni vita dhidi ya umaskini wa mali na kiroho, ujenzi wa amani,  na kuwa wajenzi wa madaraja kupitia mazungumzo.  Vile vile “kun alama tatu za kumbukumbu zinazoonyeshwa hasa katika safari ya binafsi, ya kijumuia na ya ulimwengu ambayo Papa amemwalika kila mtu, kutoka siku za kwanza za utumishi wake kama Askofu wa Roma” amesisitiza Askofu Mkuu Gallagher, na kuongeza kwamba Papa Fransisko bado anatoa wito mkubwa wa kufanya jitihada zaidi hata leo hii zinazotakiwa. “Hali hiyo inahitaji  sisi sote tuwe na ujasiri mwingi na kuachana na uhakika  wetu rahisi ambao tumekuwa nao nyuma yetu, tukishirikiana katika uongofu halisi wa mioyo, kutoa vipaumbele, mitindo ya maisha, ili kutoka na  kukutana na wengine, hata wakati hao wanaponekana ni wasumbufu, kutomjua vya kutosha, kutoka ulimwengu tofauti wa kiutamaduni na kidini au kuzungumza lugha ambazo bado ni tofauti sana”.  Kwa kuhitimisha Katibu wa Mahusiano na Nchi, amesema  kwamba diplomasia ya Vatican ni diplomasia ya njiani kwa maana  ni ya njia ndefu, ngumu na yenye matatizo, lakini kwa msaada wa Mungu inawezekana!

 

07 November 2020, 15:53