Tafuta

2020.07.01 ASKOFU MKUU PAUL GALLAGHER 2020.07.01 ASKOFU MKUU PAUL GALLAGHER 

Ask.Mkuu Gallagher:Heshima ya dini ni nguzo ya udugu!

Hotuba ya Askofu Mkuu Gallagher Katibu wa Vatican kwa ajili ya uhusiano na ushirikiano na mataifa, kwa njia ya mitandao, katika kikao kuhusu uhamasishaji wa uhuru wa kidini, hali ambazo mara nyingi katika ulimwengu zinakiukwa na zaidi wakati janga hli kumekuwa na vikwazo zaidi

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Ushirikiano na kimataifa ametoa mchango wake katika mkutano uliokuwa unaongozwa na kauli mbiu “Mtandao 2020 huduma ya kuendeleza Uhuru wa Kidini”kwa lengo la kuhamasisha uhuru wa kidini ambapo amebainisha na suala halisi na vikwazo ambavyo vimekuwapo katika muktadha wa janga. Ni katika mkutano uliofanyika tarehe 16 Novemba 2020 ambapo kila mwaka mkutano huo amekuwa akiudhuria, japokuwa kutokana na janga la Covid 19, umefanyika kwa njia ya mtandao.

Katika suala hili, viongozi wa serikali wanapaswa kujua matokeo mabaya ambayo itifaki hizo zinaweza kuunda kwa jamii za kidini au imani, ambazo zina jukumu muhimu katika kushughulikia shida, sio tu kupitia msaada wao katika uwanja wa huduma za afya, lakini pia kwa msaada wao wa kimaadili na kwa ujumbe wao wa mshikamano na matumaini na baadaye Askofu Mkuu Gallagher akiangazia athari juu ya shughuli za kidini, elimu na misaada ya jamii za imani, hasa kutokana na maoni Katoliki amethibitisha kuwa “Kupata  sakramenti ni huduma muhimu”.

Akizingatia umakini zaidi ya dharura ya Covid-19, askofu mkuu alikumbuka njia nyingi ambazo uhuru wa kidini unawekwa hatarini: “kuanzia  na mashambulio mabaya ya watu wenye msimamo mkali hadi kuenea kwa kile kiitwacho utaifa ambapo mara nyingi hudhihirishwa wengine kama aina za utaifa unaolenga watu wa nje  kama sio kama wengine, lakini mara nyingi kuonekana kama maadui” na ambao kwa hakika ni kama ukoloni wa kweli wa kiitikadi.

Askofu Mkuu Gallagher aidha amebwasilisha mapendekezo kadhaa ya kuhamasiha na kulinda uhuru wa kidini, ambao anasema ni njia mbili zinazofanana. Akizingatia mwelekeo wa kiroho na kimaadili wa mtu huyo, amesema siyo maisha haya ya kidunia tu na kwamaana hiyo ameomba kutetea hitaji la mazungumzo ya kidini na kitamaduni ili kukuza uelewano na kuheshimiana na haki ya kimsingi, mwelekeo wa ndani wa mtu binafsi, wa uhuru wa kidini, ambao hauwezi kutumiwa na kudharauliwa  kwa njia yoyote ile. Ni katika mazungumzo ya dhati na ya kweli   inawezekana kujenga udugu na urafiki wa kijamii, ambao ni muhimu katika mshikamano wa amani na katika jamii zetu zenye watu wengi.

19 November 2020, 15:07