Tafuta

Papa Francesco na Kardinali Mteule Marcello Semeraro Rais wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza watakatifu Papa Francesco na Kardinali Mteule Marcello Semeraro Rais wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza watakatifu 

Watakatifu wapya wa Kanisa watatangazwa

Papa alikutana na Rais wa Baraza la Kipapa la mchakato wa kuwatangaza watakatifu na kuridhia Baraza hilo kuwatangaza watakatifu na wenye heri wapya,baadhi ni wafiadini wa Uturuki,Italia na Brazil.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Tarehe  27 Oktoba 2020, Papa Francisko alikutana na Kardinali mteule Marcello Semeraro, rais wa Baraza la Kipapa la mchakato wa kuwatangaza watakatifu. Katika mkutano wao, Papa ameridhia Baraza hilo kuwatangaza watakatifu wapya wa Kanisa wafuatao:muujiza ulitokana na maombi ya mwenyeheri Giustino Maria Russolillo, Padre na Mwanzilishi wa Shirika la Miito kwa wanaume na Watawa wa kike  wa Miito Mitakatifu; Alizaliwa tarehe 18 Januari 1891 huko Napoli (Italia) na mauti yake yakatokea kunako tarehe 2 Agosti 1955.

Miujiza kwa ajili ya maombezi ya Mtumishi wa Mungu Maria Lorenza Requenses wa Longo, Mwanzilishi wa Hospitali ya magonjwa yasiyotibika huko Napoli na watawa Wakapuchini. Alizaliwa kunako karibia mwaka 1463 huko Lleida (Uhispania na kifo chake tarehe  21 Desemba 1539, Napoli (Italia. Miujiza kwa maombezi ya Mtumishi wa Mungu Elisabetta Czacka, Mwanzilishi wa Shirika la watawa wa Kike Wafransiskani wa Mabinti wa Msalaba. Alizaliwa tarehe  22 Uktoba 1876 huko Bila Tserkva (Ukraine) na kifo chake tarehe 15 Mei 1961e huko Laski (Poland).

Wafiadini Watumishi wa Mungu Leonardo Melki na Tommaso Saleh, Makuhani watawa wa Shirika la Ndugu Wadogo wafransiskani Kapuchini; waliuwawa kutokana na chuki ya imani yao nchini Uturuki kunako mwaka 1915 na 1917;Mfiadini Mtumishi wa Mungu Luigi Lenzini, Kuhani wa jimbo; aliuwawa  kwa ajili ya imani yake, huko Crocette ya Pavullo (Italia) katika usiku wa tarehe 20 na 21 Julai 1945; Mfiadini, Mtumishi wa Mungu Isabella Cristina Mrad Campos, Mwamini Mlei; aliuwawa kwa chuki ya imani yake huko Juiz de Fora (Brazil) kunako tarehe  1° Septemba 1982.

Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Roberto Giovanni, ndugu wa Shirika la Madonda Matakatifu ya Bwana Wetu Yesu Kristo. Alizaliwa tarehe 18 Machi 1903 huko  Rio Claro (Brazil) na kifo chake huko Campinas (Brazil) tarehe 11 Januari 1994; Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Maria Teresa wa Moyo wa Yesu; mwanzilishi msaidizi wa Shirika la watawa wa Mabinti wa Moyo Mtakatifu wa Yesu. Alizaliwa tarehe 11 Februari 1844 huko  Fuentes de Andalucía (Uhispania) na kifo chake huko Siviglia (Uhispania Spagna) tarehe  2 Juni  1908.

29 October 2020, 09:45