Tafuta

Vatican News
Wahamiaji katika makambi ya ugiriki kuelekea Ulaya Wahamiaji katika makambi ya ugiriki kuelekea Ulaya  (AFP or licensors)

Wahamiaji:kutoka mabara matano,sauti moja ya Kanisa.Ukarimu na haki!

Kutoka Marekani,Australia,Asia,Africa hadi Ulaya,Kanisa Katoliki liko mstari wa mbele kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi wakiwa nao karibu kuhasisha haki na hadhi yao.

Sr.Angela Rwezaula-Vatican

Kukarimu,kuhamasisha , kutetea haki , ushirikishwaji, maendeleo ni singi ambayo inaalikwa Kanisa Katoliki katika mabara matano katika masuala ya uhamiaji. Ni katika taarifa yak ila wiki kuhusu watu waathirika na wadhaifu waliko kwenye safari katika kipindi cha Covid-19 inayoandaliwa na Baraza la kipapapa la Maendeleo Fungamani ya watu kitengo cha wahamiaji na wakimbizi. Hii imeandaliwa kwa mtazamo wa Siku ya 106 ya wahamaiaji na waimbizi iliyofanyika tarehe 27 Septemba 2020.

Katika taarifa yao pana inajikita kulezea idadi kubwa ya mipango iliyoazishwa na makanisa ulimwenguni kwa ajili ya wahamiaji. Mipango yote hiyo inaangaziwa na Ujumbe wa Papa Francisko kwa ajili ya Siku hiyo kwa mwaka huu na hasa kuhusiana na uahamisho wa ndani. Kwa mfano katika Bara la Amerika ya Kaskazini, Kanisa katoliki linaadhimisha miaka 15 ya kamenoni ya Haki kwa ajili ya wahamiaji iliyozinduliwa kunako mwaka 2005 kwa kuwa na umakini wa kuunganisha na kuendeleza mtando wa taasisi na watu katoliki kwa ajili ya kusaidia watu wahamiaji na wakimbizi na mfumo moya wa uhamiaji. Katika fursa hiyo maaskofu wametangaza hati mpya ya kisiasa kuhusiana na uhamiaji.

Sambamba na hiyo  hata Kanisa la Amerika ya Kusini, kwa mfano nchini Argentina , Rais wa Tume ya maaskofu kwa ajili ya wahamaiji na wakimbizi(Cemi),Askofu Hugo Manuel Salaberry, amewaalikwa jumuiya ya Kanisa kuunda familia ya kweli na wale ambao leo hii ulimwenguni wanatembea kwa mahangaiko makubwa na hawajuhi hatima ya wakati wao endelevu na wanayo shauku ya kuwa na maisha yaliyo bora hasa kwa kufikiria kipindi hiki cha kushangaza cha covid-19.

Mwaliko wa Kanisa la Argentina ni ule wa kuweza kuwasaidia wahamiaji kile ambacho wanahitaji ili waweze kuwa na hadhi ya kazi na nyumba yenye utulivu kwa kukimbia mitindo mipya ya kutumia nguvu kama vile: mateso makubwa, biashara ya binadamu, unyonyaji  katika kazi, manyanyaso ya kingono, na biashara haramu ya viungo.  Huko Ciudad Juárez, Nchini Mexico katika fursa ya Siku ya wahamiaji na wakimbizi wamezindua mipango miwili ya kijumbo kwa ajili ya msada wa jumuiya nzima. Wa kwanza unahusiana na utengenezaji wa kituo cha kiparokia  cha msaada wa kwanza; ya pili inatoa ushauri nasaha wa afya ya akili, ili kusaidia kisaikolojia wanaotafuta hifadhi na ambao mara nyingi wanalazimika kukaa katika jamii za mpakani kwa muda mrefu.

Kwa upande wa Bara la Afrika hasa Nairobi Kenya mahali ambapo ,Padre Joseph G. Healey, katika mahubiri yake Siku ya Wahamiaji na wakimbizi, aliwasihi waamini kupaza sauti zao na kupendelea waliotengwa kutoka katika jamii,  katika ulimwengu wa leo, pamoja na wakimbizi na wahamiaji.  "Leo Yesu anatuomba  kuwafikia wahitaji wote kwa kutoa huduma, upendo na huruma" mesisitza Padre huyo. Kwa upande mwingine, Barani hasai hasa huko Ufilipino, Tume ya Kitaifa ya Baraza la Maaskofu kitengo cha  Wahamiaji na Watu Wakimbizi zinaelezea juu mpango wa Jimbo la  Imus ambalo, katika kipindi hiki cha dharura ya kiafya kutokana na janga la  Covid-19, limejiandaa kutoa msaada wa kifedha kwa wahamiaji, huku ikisambaza vifurushi vya chakula  na vya vifaa na usafi wa mazingira. Msaada wa ziada ulibuniwa kwa wafanyakazi waliokimbia makazi yao na wa nje ya Ufilipino kutokana na teknolojia, ambayo ilifanya iwezekane kupanga msaada wa kisaikolojia na huduma za kuwasindikiza  kiroho moja kwa moja kupitia mtandaoni.

Kwa upande wa Australia, Askofu  Christopher Prowse, mhusika wa kitengo cha  Kichungaji wa wahamaiaji na wakimbizi cha  Baraza la Maaskofu nchini humo ametangaza ujumbe wake katika fursa ya Siku ya wahamiaji na wakimbizi, tarehe 27 Septemba 2020 ambapo anathibitisha kuwa uelewa wa wasiwasi unahusiana na janga la covid-19 haupaswi kuondolea hata mgogoro wa uhamiaji uliopo. Uhamiaji ulimwenguni unawakilisha moja ya changmoto za ulimwengu leo hi na ndiyo kipaumbele cha Kanisa amesema na kwa sasa hiyo Kanisa liko karibu sana na wathaifu na mamilioni ya watu walioko hatarini wakati wa kusafiri katika ulimwengu huu kutafuta nyumba yenye hadhi.  

Kwa upande wa Ulaya, mshikamano umekuwa wa muda mrefu na madaraja ya mawazo kama yalr  ambayo yamejengwa na maaskofu wa Uswiss ambapo tarehe 27 Septemba kwa kushirikiani na Mfuko wa Kipapa wa Msaada wa Kanisa hitaji waliandaa ukusanyaji wa mchango kwa ajili ya kusaidia mipango mitatu. Kwanza unatazama nchi ya Lebanon, kwa namna ya pekee wakimbizi wa Siria huko Zahle. Kwa upande wao watapewa vifaa vya watoto. Mpango wa pili unahusu kusaidia makatekista na wahudumu wa kisaikoloji kwa ajili ya wakimbizi wa Sudan Kusini na Ethiopia. Mpango wa tatu wa mshikamano unatazama nchi ya Uswiss  yenyewe yaani ya Kichungaji kwa ajili ya makabila watu walio wachahe. Baadhi ya utumekwa  jumuiya ndogondogo ambazo zinazungumza lugha nyingine hazisaidiwi kifedha na serikali na hivyo kuekwa pembeni na bajeti ya kitaifa  Kwa njia hiyo  Maaskofu wanathibitisha kuwa matendo  ya mshikamano katika kesi hiyo ya kifedha ni kuwasaidia wao. Haki na amani ya Caritas ya Jimbo Kuu la Edimburg na Mtakatifu Andrea zimeunda kitengo cha pili cha wahamiaji. Kiungo hiki kitakuwa na kazi ya kutafuta namna ya kuboresha maisha ya wakimbizi na wanaoomba hifadhi lakini pia hata kuelimisha jumuiya mahalia kuhusu matatizo yanayowakumba na ambayo yanapaswa kukabiliwa.

02 October 2020, 15:51