Tafuta

Kukomesha njaa,kufanikisha usalama wa chakula,kuboresha lishe na kukuza kilimo endelevu ndivyo vibaki vipaumbele muhimu,kwa mujibu wa mwakilishi wa kudumu katika Ofisi za UN,New York,Marekani Kukomesha njaa,kufanikisha usalama wa chakula,kuboresha lishe na kukuza kilimo endelevu ndivyo vibaki vipaumbele muhimu,kwa mujibu wa mwakilishi wa kudumu katika Ofisi za UN,New York,Marekani 

Vatican:Ask.Mkuu Caccia asema kuwa kukomesha njaa duniani iwe ni kipaumbele!

Kukomesha njaa,kufanikisha usalama wa chakula,kuboresha lishe na kukuza kilimo endelevu vibaki kuwa vipaumbele muhimu,amesema Askofu mkuu G.Giordano Caccia,Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Umoja wa Mataifa,kwenye mkutano wa 75 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa,uliofanyika tarehe 16 Oktoba 2020 huko New York,Marekani.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Askofu mkuu Gabriele Giordano Caccia, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Umoja wa Mataifa, kwenye mkutano wa 75 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, uliofanyika tarehe 16 Oktoba 2020  huko New York, Marekani na ambao unaendelea katika hotuba yake amesema kuna ukweli wa kitendawili ambao unaona chakula kwa wote, lakini kiukweli kuna njaa ya kila siku kwa walio wengi. Kukomesha njaa, kufanikisha usalama wa chakula, kuboresha lishe na kukuza kilimo endelevu ndivyo vibaki vipaumbele muhimu. Hata hivyo kiongozi huyo amesema hayo huku akiashiria uhusiano mkubwa kati ya njaa na umaskini. Ya kwanza, kwa mujibu wake amesema  inaathiri vibaya ya pili, ni athari kwa afya inayohusishwa na kiwango kikubwa na ubora wa chakula ambao huathiri uwezo wa watu kujifunza na kufanya kazi. Kwa maana hiyo Askofu Mkuu  amehimiza, kwamba umasikini na njaa lazima vishughulikiwe pamoja, kupitia njia kamili inayojumuisha masuala ya kiuchumi, maisha endelevu na ulinzi wa jamii.

Sayari yetu inakabiliwa na uhusiano uliopotoka kati ya chakula na lishe kwani, wakati mamilioni ya watu wanateseka na kufa kwa njaa ulimwenguni kote , kiukweli zipo tani za chakula ambazo hutupwa kila siku, kiasi kwamba mtu moja kati ya tisa hana uwezekano wa kupata chakula cha kila siku, na kama hiyo haitoshi Askofu Mkuu amekumbusha kwamba “idadi inayoongezeka ya watu ya kupata chakula ikiwa sio peke yake ni vyakula vya hali ya chini kabisa , ambavyo husababisha kuongezeka uzito, unene na magonjwa yanayohusiana na lishe. Kwa maana hiyo wito wa askofu mkuu ni kupunguza gharama ya chakula chenye lishe na kufanya chakula bora kiwe na gharama nafuu kwa kila mtu.

Mantiki kuu ya kijamii na kiuchumi inayosababishwa na janga la Covid-19, kwa mujibu wa Mwakilishi wa  Kudumu amesema, imezidisha mazingira magumu ya watu wanaosumbuka na njaa na utapiamlo, kwa sababu  ya kupungua kwa tija ya kilimo na vizuizi vya mauzo ya nje na kusababaisha umaskini na ukosefu wa chakula kwa wale ambao wanategemea uchumi wa chakula cha kilimo. Kwa namna ya pekee, wafanyakazi wa msimu ambao hawawezi kupata kazi za msimu na hawawezi kusaidia familia zao na mamilioni ya watoto, kwa sababu ya kufungwa kwa shule, hawana chakula cha shule, ambazo zinawakilisha sehemu muhimu ya mahitaji yao ya kila siku.

Kwa sababu hii, Askofu Mkuu Caccia aomba kubuni hatua maalum na za dharura kwa sekta ya kilimo, kwa sababu usalama wa chakula utapatikana tu wakati miundo ya kijamii itajibu mahitaji ya haki na kuheshimu hadhi ya ndani wa kila mtu. Kinachohitajika, ameongeza kusema  ni fikira mpya, ambayo ni sera za maendeleo ambazo zinaweka mwanadamu katikati, badala ya kuhimiza utamaduni wa kutupa, ili kukuza haki kijamii, mshikamano na heshima kwa matunda ya dunia mama  na kazi ya binadamu ili kuhakikisha upatikanaji sawa wa bidhaa na rasilimali muhimu kwa kudumisha maisha na kukuza maendeleo fungamani ya kila mtu.

Mwakillishi huyo wa  Kudumu mtazamo wake  maalum wa hotuba yake pia ulikuwa ni kwa wanawake na watoto, ambao amesema mara nyingi ni waathiriwa wa unyanyasaji wakati wa mizozo ya silaha. “Vatican inapenda kurudia kusema kwamba matumizi ya unyanyasaji wa kijinsia kama silaha ya vita haikubaliki na lazima ikomeshwe, amesisitiza  Askofu Mkuu na kwamba “ Mbele ya uhalifu huo mbaya, hatupaswi kamwe kupuuza hali ya watoto hao waliotungwa mimba kama matokeo ya ukatili wa kijinsia katika vita. Mama na watoto ni waathiriwa  wasio na hatia na hakuna jitihada na hivyo lazima kuhakikisha ujumuishwaji wao kamili katika jamii”. Kwa kuongezea, amesema kufuata nyayo kwa namna ya  haki na bila upendele hata kwa wahudumu wa Umoja wa  Mataifa UN ambao  hufanya uhalifu wa unyanyasaji. Askofu Mkuu Caccia hatimaye amehimiza kujumuisha wanawake katika nyanja zote za mchakato wa amani, hasa katika kuzuia, utatuzi wa migogoro, ujenzi wa amani na michakato ya kibinadamu.

19 October 2020, 15:59