Tafuta

Papa Francisko atashiriki maombi kwa ajili ya amani tarehe 20 Oktoba katka Kanisa Kuu la Maria wa Mbingu(Aracoeli) Roma. Papa Francisko atashiriki maombi kwa ajili ya amani tarehe 20 Oktoba katka Kanisa Kuu la Maria wa Mbingu(Aracoeli) Roma. 

Tarehe 20 Oktoba ni sala ya kuombea amani kwa ushiriki wa Papa!

Ni kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habari Vatican, Dk. Matteo Bruni amethibitisha kuwa Jumanne tarehe 20 Oktoba 2020,Papa Francisko atashiriki katika Mkutano wa maombi kwa ajili ya amani katika Kanisa kuu la Maria wa Mbingu(Aracoeli) na katika Uwanja wa Manispaa ya Roma.

Mkutano wa sala kwa ajili ya amani katika roho ya Assisi unaongozwa na mada “ hakuna anayejiokoa peke yake:amani na udugu” uliyoandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, ambao utakuwa na sehemu mbili: Ya kwanza ni sala ya kiekumene na madhehebu mengine ya kikristo itakayofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa wa Mbingu (Aracoeli) na baadaye kufuatia afla na wawakilishi wa dini kuu za ulimwengu katika Uwanja wa Manispaa ya Roma.

19 October 2020, 12:17