Tafuta

Caritas Internationalis inaomba  jumuiya ya kimataifa kushughulikia kwa haraka hatua zilizolengwa kupambana na uhaba wa chakula,kwani watu wengi wanateseka walioathirika na covid-19. Caritas Internationalis inaomba jumuiya ya kimataifa kushughulikia kwa haraka hatua zilizolengwa kupambana na uhaba wa chakula,kwani watu wengi wanateseka walioathirika na covid-19. 

Siku ya Chakula Duniani:Angalisho la Caritas Internationalis kwa waliohatarini!

Katika fursa ya tukio la Siku ya Kimataifa ya chakula,tarehe 16 Oktoba,Caritas Internationalisi imetoa angalisho kuhusu tatizo la hupatikanaji wa chakula kwa walioathirika zaidi na covid-19.Kwa hivyo wanaomba msaada wa haraka kwa Jumuiya ya kimataifa katika hatua zote zinazofanywa kupambana na uhaba huo,utunzaji wa mazingira,kumaliza migogoro na kukuza mipango elendelevu ya kilimo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Hatua zilizolengwa kupambana na uhaba wa chakula, zinazohusiana na utunzaji wa mazingira, kumaliza migogoro, kukuza mipango endelevu ya kilimo na utambuzi wa maeneo ya kipaumbele kwa usalama wa chakula, ndiyo Caritas Internationalis inaomba  kwa jamuiya ya kimataifa kwa kuzingatia  fursa ya Siku ya Chakula Duniani ambayo inaadhimishwa kila tarehe 16 Oktoba ya kila mwaka. Tayari mwezi Mei uliyopita taarifa  ya shirikisho hili inakumbusha kuwa lilikuwa limetoa tahadhari juu ya athari mbaya ambazo janga litaleta na hatua za kuzuia kuenea kwa Covid-19 zingeweza kutokea  na ukosefu wa usalama wa chakula. Takwimu za sasa zinatisha . Kulingana na Shirika la Mpango wa Chakula Ulimwenguni, watu milioni 230 wako katika hatari ya kufa njaa. Milioni 130 zaidi ya mwaka jana.

Wanaolipa gharama kubwa kwa mara nyingine ni waathiriwa kwa mujibu wa Bwana Aloysius John, Katibu Mkuu wa Caritas Intenationalis na kwamba Janga limeongezea kwa nguvu ukosefu wa vyakula na kukosesha hupatikanaji wa chakula kwa wale ambao tayari walikuwa ni maskini. “Caritas Internationalis inaamini kuwa chakula ni haki msingi na haki kwa wote ambao ni waathirika na amba oleo  hii wanakosa kwa sababu ya janga la virusi au covid-19. “Ikiwa jirani yetu nateseka na njaa ni kazi ya wajumbe wote wa jumuiya ya ulimwengu kuhisi kama wahusika wa kuweza kutenda kwa haraka na kwa namna ya kuwa na mshikamano”, mesema Bwana Aloysius.

Katika roho ywa waraka wa’ Fratelli tutti’, yaani ‘wote ni Ndugu’, Caritas Internationalis inaomba nguvu zote mshikamano na nguvu ya uwanjibikaji mbele ya walio hatarini zaidi. Utandawazi wa mshikamano ndiyo lazima uwe kama kipaumbele cha  kufikiria daima ili wote wawe na  chakula na  kama haki msingi, kama anavyosisitiza Papa Francisko na kukumbusha kuwa : “Kama ilivyo  kupoteza na kutupa chakula ni sawa  na kuwanyima wengine chakula wanachohitaji ili kuishi”.

Kwa  wito huo kwa viongozi wote wa kisiasa wanatakiwa kuchukua hatua zinazohitajika. Hasa, wanaombwa kutoa msaada kwa mashirika ya kibinadamu na fedha zinazohitajika ili kujibu mahitaji ya haraka; kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko tabianchi, na  ulinzi wa mazingira. kuhamasisha kilimo kidogo kwa kutenga fedha kwa shughuli hizo; kukomesha vita na mizozo ambayo inalazimisha mamia ya maelfu ya watu kuhama na kuongeza uhaba wa chakula; kubainisha maeneo ya kipaumbele ya usalama wa chakula ili kukuza miradi ya maskini zaidi. Kwa maelezo zaidi ya Siku hiyo Caritas internationalisi umetoa kamepni mpya ya ukosanyi  wa fedha: www.caritas.org/wfd2020.

16 October 2020, 11:33