Tafuta

2020.01.01 Noeli-Vatican -Mti wa mapambo na Pango 2020.01.01 Noeli-Vatican -Mti wa mapambo na Pango  

Siku kuu ya Noeli:Mti wa kupamba unafika Vatican kutoka Solvenia!

Uzinduzi na kuwashwa kwa taa umepangwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 11 Desemba saa 10.30 jioni masaa ya Ulaya licha ya mapungufu yaliyopo kutokana na janga,. Na katika afla hiyo itaongozwa kama kawaida na Rais na Katibu Mkuu wa serikali ya mji wa Vatican.Asubuhi hiyo uwakilishi kutoka mahali ambapo ndiyo asili ya mti na matengenezo ya pango watapokelewa na Papa Francisko.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ishara ya matumaini na uaminifu kwa ulimwengu kwa hakika kwamba Yesu anakuja kati ya watu wake kuwaokoa na kuwafariji. Huu ndiyo ujumbe muhimu kwamba hata zaidi wakati wa dharura ya kiafya unataka kuelezea mipangilio ya Siku kuu ya kuzaliwa kwa Bwana iliyopangwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro 2020. Uzinduzi wa kiutamaduni na taa zimepangwa siku ya Ijumaa tarehe 11 Desemba 2020 saa 10.30 jioni  masaa ya Ulaya licha ya mapungufu yaliyomo kutokana  na janga, lakini katika sherehe itaongozwa kama kawaida na Kardinali Giuseppe Bertello na Monsinyo Fernando Vérgez Alzaga, wote wawili wakiwa marais  na Katibu Mkuu wa Serikali ya jiji la Vatican.

Siku hiyo hiyo, asubuhi, uwakilishi kutoka maeneo ya asili ya mti na watakaotenegeza pango kutoka Castelli na  Kočevje, watapokelewa katika mkutano na Papa Francisko kwa uwasilishaji rasmi wa zawadi hizo. Mti na pango vitabaki kwenye maonyesho hadi siku ya Jumapili tarehe 10 Januari 2021, katika Sikukuu ya Ubatizo wa Bwana kama ifanyikavyo kila mwaka. Kwa njia hiyo Italia na Slovenia ndio wafadhili wa kupamba maonyesho hayo ya mwaka huu. Kutoka Castelli, katika wilaya wa Teramo, kituo muhimu sana cha kutengeneza sanaa kutumia udongo  tangu karne ya 16, watafika na sanamu za kuzaliwa kwa Bwana kuziweka kwenye Pango ambazo ni  kubwa kuliko saizi ya kawaida. Hii ni ishara kiutamaduni wa Mkoa mzima wa Abruzzo lakini pia kitu cha sanaa ya kisasa ambacho kina mizizi yake katika kazi ya utamaduni wa udongo kwa watu wa huko Catelli.

Katika uwanja wa Mtakatifu Petro kwa maana huyo wataweka vipande vichache tu vya mkusanyiko dhaifu wa sanamu 54. Zitawekwa pembeni kwenye jukwaa lenye taa la karibu mita za mraba 125 ambazo zinazunguka sehemu ya obelisk kwenye mteremko kidogo. Sanamu zinawakilisha Mamajusi; katikati, kwenye sehemu ya juu kabisa ya jukwaa, ni kikundi cha Malaika wakati wa kuzaliwa kwa Yesu na kitakachowekwa juu ya Familia Takatifu kuashiria ulinzi wake juu ya Mwokozi, Maria na Yosefu. Katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kutaweka Mti mrefu mzuri wenye  urefu wa mita 28 na kipenyo cha sentimita 70, ambao ni kutoka kusini-mashariki mwa nchi ya Slovenia, hasa kutoka manispaa ya Kočevje, kwenye mto Rinža. Eneo la Kočevsko ni moja ya maeneo ya Kislovenia ambayo ni yenye asili ya kupendeza zaidi misitu misitu hufunika asilimia 90% ya eneo lake.

Miti hiyo aina ya (Spruce) ilienea sana huko Slovenia katika nusu ya pili ya karne ya 18, ambayo inawakilisha zaidi ya ya rasilimali 30% za msitu na ndio aina  muhimu zaidi ya miti kutegemea  mantiki ya  kiuchumi nchini humo. Tangu nyakati za zamani imekuwa ishara ya kizazi na katika tamaduni maarufu mara nyingi hutumiwa kwenye hafla ya sherehe kama sikukuu ya  mwezi Mei  Mosi au sherehe za Kuzaliwa kwa Bwana.  Katika mkoa wa Bela Krajina, kwa sikukuu ya Mtakatifu George ilikuwa ya kiutamaduni kubeba mti wa aina hiyo (spruce) katika maandamano, iliyosafishwa na kupambwa na maua na vitambaa. Spruce ndefu zaidi ya Ulaya  inaitwa ‘Sgermova smreka’ ambayo ina urefu wa mita 61.80 na iko kwenye milima ya Pohorje huko Slovenia. Ina umri wa miaka 300, na mzunguko wa mita 3 na sentimita 54 na kipenyo cha zaidi ya mita moja.

30 October 2020, 16:28