Tafuta

Basilika ya Mtakatifu Petro Basilika ya Mtakatifu Petro 

Papa ameteua Tume ya Mambo ya Hifadhi

Taasisi hiyo ilikuwa imeoneshwa tayari na Kanuni mpya kwa ajili ya Ununuzi na ili kusimamia mikataba kadhaa ambayo kwa sababu ya tabia zake iko nje ya vifungu vya Kanuni sawa na hiyo.

VATICAN

Baba Mtakatifu Francisko amemteua mwenyekiti na wanachama wa Tume ya Mambo ya Hifadhi. Hii ni habari iliyotangazwa na Msemaji wa Vyombo vya habari kwa waandishi Vatican. "Baba Mtakatifu tarehe 29 Septemba 2020 alimteua Kardinali Kevin Farrell kuwa Mwenyekiti wa Tume ya masuala ya Mambo ya Hifadhi na Katibu, Askofu Mkuu Filippo Iannone. Wajumbe wa Tume hiyo pia waliteuliwa  na hao ni  Askofu Fernando Vérgez Alzaga, Askofu Nunzio Galantino na Padre Juan Antonio Guerrero"

Hiyo ndiyo itakuwa tume ambayo itaamua juu ya kesi kwa mfano kuhusu vitendo gani vya hali ya uchumi lazima vihifadhiwe. Ili kuelewa maana ya uamuzi huo, ni muhimu kurudi nyuma kwenye yale yanayosomeka katika "Kanuni za uwazi, udhibiti na ushindani wa mikataba ya umma ya Vatican na Jiji la Vatican",  iliyochapishwa mwezi Juni iliyopita. Katika kifungu cha 4 cha maandishi hayo yaliyoidhinishwa na Papa, kwa ufupi kama kanuni ya manunuzi ilibainishwa kuwa matumizi ya sheria hiyo yalitumika katika mikataba yote ya umma isipokuwa kesi zingine.

Miongoni mwa kesi ambazo sheria haitumiki, kwa maana "d" yaani kifungu hicho hicho,  "mikataba iliyoainishwa moja kwa moja na Sekretarieti ya Nchi na Gavana, kwa kiwango cha uwezo wao na ambayo ina angalau moja ya sifa zifuatazo”:

"Ni muhimu kutimiza majukumu ya kimataifa, ikiwa chombo hicho hicho kinaamuru sheria za utoaji mikataba moja kwa moja";

"Wanafadhiliwa kikamilifu au kwa sehemu na shirika la kimataifa au taasisi ya kifedha ya kimataifa na sehemu ya mikataba ya makubaliano  juu ya taratibu zinazofaa";

"Wanazingatia  mambo yaliyofunikwa na dhamana ya usiri iliyotajwa katika ibara ya 39 ya Motu Proprio kuhusu ‘Huduma ya Uangalifu'";

"Wanazingatia ofisini usalama wa Baba Mtakatifu, wa Vatican na Kanisa la Ulimwenguni au ni muhimu wanafanya kazi ili kuhakikisha utume wa Kanisa ulimwenguni na kuhakikisha uhuru na uhuru wa Vatican au Serikali ya  Jiji la Vatican";

Kifungu cha 4 cha Kanuni kwa ajili ya  manunuzi kilihitimishwa kwa kifungu kifupi (aya ya 2), ambayo ilisema kwamba "Kamati ya Udhibiti iliyoteuliwa na Mamlaka Kuu inasimamia Mikataba iliyotajwa katika aya ya 1 barua d hapo juu".  Tume iliyoundwa  siku za hivi karibuni kwa maana hiyo inachukua kazi hizi za ufuatiliaji na usimamizi.

05 October 2020, 15:09