Tafuta

Bwana Mike Pompeo, Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani amekutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin aliyekua ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher. Bwana Mike Pompeo, Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani amekutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin aliyekua ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher. 

Mike Pompeo wa Marekani Akutana na Kardinali Parolin mjini Vatican

Kardinali Parolin amekutana na kuzungumza na Bwana Mike Pompeo kutoka Marekani. Katika mazungumzo yao ambayo yamedumu kwa takribani dakika 45, wamegusia kuhusu misimamo ya pande hizi mbili mintarafu mahusiano ya kidiplomasia na China. Wamezungumzia kuhusu: vita na machafuko ya kisiasa yanayoendelea kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican akiwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican, Alhamisi, tarehe 1 Oktoba 2020 wamekutana na kuzungumza na  Bwana Mike Pompeo, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani. Katika mazungumzo yao ambayo yamedumu kwa takribani dakika 45, wamegusia kuhusu misimamo ya pande hizi mbili mintarafu mahusiano ya kidiplomasia na China. Wamezungumzia kuhusu: vita na machafuko ya kisiasa yanayoendelea kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao.

Dr. Matteo Bruni, Msemaji mkuu wa Vatican amesema kati ya nchi zilizogusiwa ni pamoja na Ukanda wa Caucasus, eneo linaloundwa na Georgia, Armenia na Azerbaijan bila kusahau hali tete huko Mashariki ya Kati na Ukanda wa Mediterrania. Katika siku za hivi karibuni, Bwana Mike Pompeo, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani amekuwa akitoa shutuma nzito dhidi ya Vatican mintarafu Mkataba wa Muda kati ya Vatican na China uliotiwa mkwaju tarehe 22 Septemba 2018. Msimamo huu wa Bwana Mike Pompeo dhidi ya Vatican umezusha taharuki kubwa miongoni mwa vyombo vya mawasiliano ya jamii. Kardinali Pietro Parolin amesema Vatican inatarajia kupyaisha Mkataba wake na China, ingawa bado ni wa muda mfupi. Kimsingi, huu ni mkataba unaogusa shughuli za kichungaji, ili kuhakikisha kwamba, maaskofu wanakuwa na umoja kamili na Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Kardinali Parolin
02 October 2020, 14:45