Tafuta

Watoto nchini Ufilippini wakisali Rosari kama sehemu ya Kampeni ya watoto milioni moja kusali rosari iliyoandaliwa na Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji Watoto nchini Ufilippini wakisali Rosari kama sehemu ya Kampeni ya watoto milioni moja kusali rosari iliyoandaliwa na Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji 

Maombi ya Watoto kwa Mama Maria ili dharura ya kiafya imalizike!

Katika ujumbe kwa njia ya mitandao,Papa anahimiza kusali rosari na kuungana na watoto wanaosali rosari kuombea umoja na amani.

Katika mitandao ya kijamii, Papa Francisko anawaalika watu wote kuchukua Rosari mikononi na kusali huku wakimwinulia Mama Maria ambaye ni ishara ya faraja na uhakika wa tumaini kama wafanyavyo leo hii watoto wote ulimwenguni ambao wanaombea umoja na amani.

Shule za aina zote na shule za chekechea ulimwenguni kote zinaalikwa kushiriki katika mpango ulioanzisha na Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji (ACS), kwa Watoto milioni moja kusali Rozari. Katika kufanikisha hilo wametoa vifaa katika tafsiri ya lugha ishirini na tatu ambazo zimetumika kufanya kampeni ya maombi kati ya hizo kuna lugha ya Kiarabu na lugha asili za Kiafrika.

"Ninawatia moyo kuanzisha tukio  hili ambalo linawaunganisha watoto wote ulimwenguni na  ambao watasali hasa kwa ajili ya hali halisi ngumu iliyosababishwa na janga." Ni kwa maneno hayo Papa Francisko aliyatoa Dominika iliyopita baada ya sala ya Malaika wa Bwana akikumbusha juu ya mpango ulioanzishwa na Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji (ACS) kwa kampeni ya Watoto milioni moja kusali Rosari" na ambao unawalenga shule zote hata chekechea kila kona ya dunia.

Ushiriki ni mpana  sana ambao kiukweli ni mataifa 80 ilimwenguni  kuanzia Ghana hadi Siria,  Papua Guine Mpya na nchi nyingine. Ni kampeni ambayo ilianza tangu mwaka 2005 katika mji wa Caracas, nchini Venezuela, kutokana na baadhi ya watoto waliokuwa wakiunganika kusali rosari kwa Bikira Marima mbele ya duka moja la kuuza magazeti. Kwa kuongozwa na maneno ya Padre Pio wa Pietrelcina "ikiwa watoto milioni moja watasali Rosari ulimwengu utabadilika", tangu mwaka 2008 kwa kuungwa mkono na Shirika la  Acs, kwa ngazi ya ulimwengu kwa miaka miwili sasa shirika hili linachukua wajibu wa kuendeleza tukio hili muhimu.

Katika mgogoro wa sasa , kwa mujibu wa Kardinali Mauro Piacenza, Mwenyekiti wa ACS kimataifa amesema ulimwengu wote umekuwa, na unaendelea kuwa wazi kwa virusi visivyoonekana ambavyo vimesababisha vifo vya mamia ya maelfu ya watu na kwa athari mbaya, na kwa sasa haitabiriki, matokeo ya kijamii na kiuchumi. Ulimwengu wetu sio ulimwengu uleule tena, na kile ambacho mpaka sasa kimechukuliwa kuwa cha kawaida hakifanani tena.

19 October 2020, 12:47