Tafuta

2020.03.11 Katekesi ya Papa katika Maktaba ya kitume 2020.03.11 Katekesi ya Papa katika Maktaba ya kitume 

Kuanzia Novemba ijayo Katekesi zinafanyika tena kutokea Maktaba ya kitume!

Ili kukabiliana na kuenea kwa janga la Covid-19 na kuepusha hatari zaidi kwa washiriki,tangu tarehe 4 Novemba ijayo katekesi za kila Jumatano za Papa zinarudi kufanyikia katika Maktaba ya Jumba la kitume mahali ambapo alikuwa akifanyia siku chache zilizopita hadi tarehe 26 Agosti.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni kutoka katika uwanja wa Matakatifu Damas, mjini Vatican kurudi tena katika Maktaba ya Papa, kutokana na uamuzi uliotolewa ambapo hadhira ya ushiriki inarudi kuwa mbali yaani waamini kushiriki katika katekesi Papa. Kwa maana hiyo, kila Jumatano, kama ilivyotangazwa  na  Ofisi ya Wanahabari Vatican kwamba  kuanzia tarehe 4 Novemba 2020, Papa  Francisko atafanya katekesi yake kutokea katika Maktaba ya Jumba la kitume Vatican.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari ni kwamba “hii kufuatia na kuripoti kesi chanya ya Covid-19, wakati wa kusikiliza katekesi ya Jumatano tarehe 21 Oktoba na ili kuepusha hatari zozote za kiafya kwa washiriki”.

Hata hivyo kunako tarehe 2 Septemba iliyopita, ilikuwa ni furaha ya Papa Francisko kuwaona waamini tena, mara baada ya siku 189, kwa kufuata kanuni za usalama, katika nafasi ya Uwanja wa Mtakatifu Damas, na aliwashangaza kwa maneno yake machache aliyonena kabla ya kuanza katekesi yake. Siku hiyo Papa alisema “Baada ya miezi mingi sana tunaanza tena mkutano wetu uso kwa uso na sio skrini kwa skrini. Uso kwa uso. Hii ni nzuri!”.

Ikumbukwe ilikuwa ni tarehe 26 Februari ambapo Papa Fransisko, kwa kufuata hatua za kiafya za kuzuia maambukizi, alianza kuzungumza na wakristo kutokea  katika nafasi iliyofungwa ya Maktaba ya Jumba la kitume ambapo sasa atarudi kwa mara nyingine tena, kwa  maana  hiyo, ni kuanzia Jumatano ya kwanza ya Novemba.

29 October 2020, 15:28