Tafuta

Kardinali Tauran alikuwa shuhuda wa kweli wa majadiliano ya kidini Kardinali Tauran alikuwa shuhuda wa kweli wa majadiliano ya kidini 

Kardinali Tauran alikuwa shuhuda wa kweli wa mazungumzo ya kidini!

Hata katika hali ya ugonjwa Kadinali Tauran alipitia uzoefu wa Ayubu kwani Ayubu katika uzoefu wake wa ugonjwa na kuishiwa nguvu alishuhudia katika maisha yake kwamba“mimi ninajua kuwa mwokozi wangu yu hai na siku ya mwisho atanifufua.Nitamwona Mungu. Mimi mwenyewe kwa macho yangu nitamtafakari.Ni katika mahubiri ya Kardinali Parolin,wakati misa ya kumbukumbu ya marehemu huyo.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vtican

Tarehe 24 Oktoba 2020 ilifanyika misa kwa ajili ya kukumbukuka na kuombea Marehemu Kardinali Jean-Louis Tauran aliyekuwa rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mazungumzo ya Kidini na Camerlengo wa Kanisa la Roma alizaliwa huko Bordeaux, Ufaransa  kunako tarehe 5 Aprili 1943.  Na mauti yalimfikia tarehe 5 Juali 2018 huko Hartford, nchini Marekani. Misa ya kumbu kumbu hiyo imeongzwa na Kardinali Petro Parolin, Katibu wa Vatican katika Kanisa lake Kuu la Mtakatifu Apolinare Roma. Katika mahubiri alikumbuka maisha ya Kardinali huyo mwanadiplamsa na ambay aifanya kazi nzuri sana ya kitume na kwa maana hiyo kuendelea kusali kwa ajili yake katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Apolinare maha ambapo masalia yake yamelazwa.

Akitazama Injili liyosomwa ambapo Yesu akitoa hotuba yake ya mwisho. Hiyo inakuja wakati wa hali ya mahangaiko mahali ambapo baada ya Karamu ya mwisho na wafuasi wake na usiku, ulikuwa ni wakati wa kuagana.  Kuagana huko siyo kimwili tu lakini pia kiroho, sula ambalo lilikuwa kikiambatanisha na uchungu kwa ajili ya matarajio ambayo Yesu alikuwa ajibu wakati unaomsubiri. Kwa kuzingatia Yuda alikuwa tayari ameondoka, Petro angeweza kumkana na wengine wote wangeweza kumkimbia. Katika hali hiyo Yesu lakini hatamki maneno magumu ya chuki, lakini ya kutia moyo kwa upendo na kuhimiza matumaini kwani anasema “msiangaike mioyoni mwenu (Yh 14,1) . Asili ya neno hiyo halioneshi wasi wasi au hofu ya juu juu bali inakwenda katika mzizi wa hofu ya ndani, mahagaiko yale ambayo ukung’uta kweli kweli maisha na tathimini ya mwisho kutokana na kujihisi upweke na bila kuwa na ulinzi wowote mbele ya hatari na kifo.

Ni neno ambalo hata Yesu mwenyewe alihisi mpaka akalia machozi kwa ajili ya rafiki yake Lazaro (Yh 11,33).  Kwa maana hiyo ni wazi kwamba Yesu alikuwa anaona wasi wasi mkuu wa wafuasi wake, kuona kwamba hao hawakuwa na matajio yoyote kwa sababu ya kuondoka kwake.  Sabu yake ni kutokana na kwamba Yesu anaeleza kuondoka kwake, lakini hatawaacha peke yao kwa sababu anakwenda kuwatengenezea makao ili mahali alipo yeye na wao waweze kuwapo  (Yh 14,2-3). Hii ina maana ya adhati ambayo daima inasindikiza matatizo na kuishi kwetu kwa sababu tunatakiwa kuishi na uwepo wa Mungu. Maneno ya Yesu yatakata kuwa na uhakika ambao ni msingi mkuu wa Pasaka. Ni wazi kwa kuwa baada ya mateso, kifo, ufufuko na kupaa mbinguni, Yesu anapata nafasi  mpya kwa ajili yetu ambayo kabla ya hapo hatukuwa nayo amesisitiza ardinali Parolin. Yeye alichukua ubinadamu wetu katika kona ya kifo hadi kutufikisha mbele ya uso wa Mungu baba. Yesu ni mtu kweli , ambaye ni ubinadamu wetu, ni mwili kweli na alishinda mauti akarudi kwa Mungu baba yake na baba yetu . Sisi siyo wafungwa wa kushikilia na kubaki katika dunia, bali tuna nafasi ambayo imehifadhiwa daima mbinguni ka ajili yetu.

Kadinali Tauran alipitia uzoefu wa Ayubu kama Somo lililosomwa, kwani Ayubu katika uzoefu wake wa ugonjwa na kuishia nguvu alishuhudia kwa hakika katika maisha yake   kwamba “mimi ninajua kuwa mwokozi wangu yu hai na siku ya  mwisho atanifufua. Nitamwona Mungu. Mimi mwenyewe kwa macho yangu nitamtafakari (Ay 19,25-27).  Kwa kuhitimisha amesema kuwa Kardinali Tauran  katika maisha yake ya kitume  alifanya mazungumzo kuwa sababu ya maisha , kwa kuweka msingi wa matumaini kwa Yule aliye njia , ukweli na maisha na kwa maana hiyo atuombee hata sisi , ili urithi wake uwe sababu ya kuwa thabiti katika changamoto ambazo tunakabiliana nazo duniani na kuwa mashuhuda wa matumaini ambayo tunasubiri huko mbinguni ( Wakol 1,5 .

Ikumbukwe Marehemu Kardinali Tauran , kunako tarehe 29 Machi 2014 Papa Francisko alimthibitisha  tena kama Rais wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini. Viel vile mnamo tarehe 20 Desemba 2014 Papa Francisko alimteua kuwa Camerlengo wa Kanisa Takatifu katoliki la  Roma. Wakati wa uhai wake alishiriki baraza la Makardinali  kunako Aprili 2005 waliomchagua Papa mstaafu  Benedikto XVI  na katika Baraza la  Machi 2013 waliomchagua Papa Francisko. Kardinali Jean-Louis Tauran alifariki tarehe 5 Julai 2018 huko Hartford, Marekani. Katika uhai wake alikuwa mjumbe wa Wa Baraza la Kitengo cha  II cha Sekretarieti ya Vatican; wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki kwa ajili ya Maskofu;Wa Tume ya kipapa kwa ajili ya jiji la Vatican; wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha umoja wa Kanisa, na Utamaduni; Tume ya Usimamizi wa Taasisi ya fedha ya Shughuli za  Kidini (I.O.R.).

26 October 2020, 14:31