Tafuta

2020.06.16 Wanafunzi wahamiaji 2020.06.16 Wanafunzi wahamiaji 

Kard.Turkison:kazi ya elimu ni kutoa mwongozo wa mafundisho fungamani!

Rais wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu amekumbusha umuhimu wa kuelimisha kwa namna ya pekee katika kipindi hiki kilichoyumbishwa na janga, na kwamba kazi ya elimu ni kutoa mwongozo wa mafundisho na kukazia elimu ya ekolojia fungamani.Amesema hayo wakati wa mkutano ulioandaliwa na chama cha mfuko wa Kipapa wa Centesimus Annus-Pro Pontefice.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ikiwa unataka kubadilisha ulimwengu, lazima ubadilishe elimu na mifano inayohusiana na elimu. Hii ni moja ya mambo muhimu yaliyofafanuliwa  katika hatua ya  pili na ya mwisho ya mkutano wa kimataifa ulioongozwa na mada “hatua muhimu za ekolojia ya Jumuiya ya Uchumi wa BinadamuI iliyoandaliwa na Chama cha Kipapa cha Mfuko wa Centesimus Annus - Pro Pontifice, tarehe 30 Oktoba 2020. Kutokana na sababu ya dharura ya Covid-19, kikao hicho pia kimefanyika kupitia jukwaa la kidigitali. Kazi  hiyo ilifunguliwa na Bi Anna Maria Tarantola, rais wa  chama cha kipapa cha Mfuko huo, ambaye alinukuu maandishi kutoka Laudato si'  ya Papa Francisko yasemayo: “Ubinadamu unahitaji kubadilika." Hii ina maana kwamba “kuna ukosefu wa ufahamu wa asili moja, ya kuheshimiana na hali ya baadaye inayoshiririkisha wote. Kuwa na ufahamu huu kimsingi utaruhusu maendeleo ya imani mpya, mitazamo mipya na mitindo ya maisha. Kwa maana hiyo changamoto kubwa ya kitamaduni, kiroho na kielimu inaibuka na ambayo itahusisha michakato mirefu ya kuzaliwa kwa upya ”.

Hotuba ya ufunguzi wa kikao hicho imekabidhiwa Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa Maendeleo fungamani ya Binadamu. Katika hotuba hiyo ameangazia kaulimbiu ya mkutano huo isemayo “Elimu na Mafunzo", ambapo Kardinali Turkson amekumbuka tukio la kweli ambalo limemrudisha nyuma ya nyumbani kwao, yaani nchi yake Ghana. Katika kijiji kimoja Kardinali Turkson amethibitishwa kuwa profesa mmoja alikuwa amepokea kompyuta na mashine ya kutoa kopi , na vitu vyote vilikuwa vimembatana na vijitabu vya maagizo. Mwalimu aliwaelekeza wanafunzi kuwa kila kifaa kipya kila wakati kinajumuisha kijitabu kinachoelezea ili kuwezesha matumizi yake. Vijana hao baadaye wakamwuliza mwalimu ikiwa vitu vyote vipya vinahitaji mwongozo, je kwa nini hakuna kijitabu cha maagizo wakati mtoto anapozaliwa?

Profesa alijibu swali hilo akiwaelekeza wanafunzi wake kwamba “ni kwa sababu hiyo ninyi mko hapa shuleni”. Kwa maana hiyo kazi ya elimu, Kardinali Turkson amesisitiza ni kutoa mwongozo wa mafundisho na fungamani. Elimu katika ekolojia fungamani ni muhimu sana. Hatimaye Kardinali Turkson amesisitiza kuwa ndiyo lengo kuu la elimu jumuishi ya ikolojia ambayo inategemea hitaji la kufikiria juu ya faida ya wote katika vitu vyake  vitatu muhimu. Ni katika kutoa maelekezo kama vile ya maisha, ya Dunia na mara tatu ya uhusiano wa mwengine, binafsi na wa Mungu.

30 October 2020, 17:54