Tafuta

Vatican News
Askofu Mkuu Gabriele Giordano Caccia Askofu Mkuu Gabriele Giordano Caccia  

Vatican-Ask.Mkuu Caccia:Ni wakati wa kunyamazisha silaha Afrika ya Kati!

Inahitajika kuwasaidia wale wote wanaotumia silaha kwa njia isiyo ya haki ili kuweka chini vyombo hivi vya kifo.Amesema hayo Askofu Mkuu Gabriele Caccia,mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa UN wakati wa hotuba yake tarehe Mosi Oktoba 2020 huko New York,Marekani.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Umefika wakati wa kunyamazisha silaha na kufanya maendeleo ya kweli katika suala la maendeleo muhimu nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Hayo yamesema na Askofu Mkuu Gabriele Caccia, mwakilishi  wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa UN wakati wa hotuba yake tarehe Mosi Oktoba 2020  huko New York Marekani, katika mkutano wa ngazi ya mawaziri juu ya hali halisi ya Afrika ya Kati.  Kwa mujibu wa kiongozi huyo amesema inahitajika kuwasaidia wale wote wanaotumia silaha kwa njia isiyo ya haki ili kuweka chini vyombo hivi vya kifo! Msaada na ufadhili wa mtiririko haramu wa silaha na wa vikundi ambavyo havifanyi jitihada  kwa ajili ya umoja na uzuri wa nchi lazima vikomeshwe. Aidha ameongeza kwa kuwataka raia wote wa nchi hiyo ya Kiafrika kutoka kila aina ya maisha, bila kujali asili ya kikabila, kutoka kwa washiriki wa kidini au kwa imani yoyote ya kisiasa ili kuhamasisha maendeleo fungamani.

Taifa, kiukweli, liko katika wakati muhimu wa kihistoria kwani mwezi Desemba umepangwa kufanyika uchaguzi wa wabunge na urais, ambapo Vatican inatarajia kuwa uwe wa amani kwa sababu wakati umefika kwa idadi ya watu kuanza kuandika sura mpya pamoja ya historia ya nchi, amesisitiza. Licha ya makubaliano ya amani yaliyotiwa saini huko Bangui mnamo Februari 2019 kati ya serikali ya kitaifa na vikundi vyenye silaha, mivutano na mapigano makali yanaendelea katika nchi ya Afrika ya Kati, kiasi kwamba watu wengi waliohamishwa makazi bado wanayo mahitaji makubwa ya kibinadam. Kwa sababu hiyo, Askofu Mkuu Caccia amehimiza mazungumzo kati ya pande zote, kwa nia ya Mkataba, ili kuhamasisha mazingatio zaidi ya ahadi zilizowekwa. Na zaidi kwa mujibu wa Mwakilishi wa Kudumu amehimiza pia kuzingatia athari ambayo janga la Covid-19 linaendelea kudhuru jumuiya nzima ya Afrika ya Kati.

Hadi sasa nchini, humo virusi hivi vimerekodi visa karibu elfu 5 kwa ujumla. Kwa mujibu wa mwakilishi wa Kudumu pia ameshutuma dhidi ya wale ambao, kwenye karatasi, huchagua kujitoa kisiasa lakini wakati wa kutenda ni vitendo vya kutisha kwa idadi ya watu kwa njia isiyostahili ahadi thabiti ya uwazi na demokrasia. Vitendo kama hivyo vinazuia maendeleo muhimu na husababisha machafuko zaidi na migawanyiko amesema  Askofu Mkuu Caccia. Na wale wanaolipa gharama  ya juu ni watu maskini na walio katika mazingira magumu zaidi ya idadi ya watu. Kwa hakia  vijana wananyimwa elimu na wanalazimishwa kinyume cha sheria kuingia kwenye vikundi vyenye silaha, ambapo ni waathiriwa  wa vurugu kubwa; wanaume na wanawake hawawezi kulima mashamba yao na kwa hivyo kuweza kujipatia riziki inayofaa, wakilazimishwa kuishi kwa hofu kutokana na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

Askofu Mkuu Caccia hata hivyo amekumbusha kuwa  kuna ukosefu wa mahitaji ya kimsingi na hata misaada ya kibinadamu wakati mwingine inashindwa kuwafikia wahitaji kwa sababu ya dharau ya utawala wa sheria inayotekelezwa na vikundi vyenye silaha. Kufuatia na hayo Askofu Mkuu Caccia amekumbuka kuwa kunako mwaka 20216 kwa utashi wa Papa Francisko, Vatican ikiwa ishirikiana na Hospitali ya Bambini Gesu, Roma ilitoa mchangi muhim sana na wenye kufaa katika husuma na kusaidia ujenzi wa Hospitiali ya Watoto mjini Bangui kwa kuboresha namna hiyo hali ya maisha ya watoto mahalia. Kupanga, kufadhili miundo mipya, mafunzo ya madaktari wa watoto na kukuza maendeleo ya jumuiya zote mahalia ndizo zana zilizowekwa kwa miaka minne sasa. Hatimaye Mwakilishi wa Kudumu ametumia maneno ya  yake  Baba Mtakatifu, kuwa yake aliyotamka mnamo 2015 hasa katika nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambayo ni wito “kwa watu, viongozi wao na wenzi wao ili  kufanya kazi bila kukoma kwaajili ya  umoja, utu wa binadamu na amani  kwa kuzingatia haki”.

03 October 2020, 15:54