Tafuta

Kard.Tagle:Kipindi cha Kazi ya Uumbaji kinakumbusha ulazima wa kulinda!

Katika Video ya Rais wa Braza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu anatoa ujumbe kwa mwezi ambao umewekwa kwa ajili ya kuhamasisha kulinda asili.Mara nyingi anasema Kardinali Tagle,tunajifanya ni wamiliki wa mali yetu na kusahau kuwa sisi ni watunzaji.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

“Ninakumbuka vizuri, kwa furaha na upendo  kuhusiana na maadhimisho ya kipindi cha Kazi ya uumbaji katika jimbo langu la Imus na Jimbo Kuu la Manila”. Hii ni kumbukumbu ya Kardinali Luis Antonio Tagle Rais  wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji  wa watu ambapo anakumbuka miaka ya hivi karibuni akiwa bado anatoa huduma yake nchini kwake Ufillipino na maadhimisho ambayo kila kipindi kile kwa wakristo ilikuwa na maana ya kupokea Mungu katika uzuri wake wa uumbaji.

Kuwa watunzaji, sio wamiliki

Katika video iliyorekodiwa kabla ya kuambukizwa yeye mwenyewe na Covid-19, Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na rais wa Caritas Internationalis amezindua kwa mara nyingine tena mwaliko wa kuungana na Kanisa la ulimwengu ili kusherehekea kipindi  cha Kazi ya  uumbaji, ambacho kilianza tangu tarehe 1 Septemba hadi 4 Oktoba 2020  katika sikukuu ya Mtakatifu Francis wa Assisi. Ni wakati wa kiliturujia ​​kusherehekea uzuri wa uumbaji katika sala, hasa katika Ekaristi na ishara za ukarimu na upendo wa Mungu, amesema Kardinali.  “Pia ni mwaliko wa kugundua tena wito wetu kama watunzaji wa Kazi ya uumbaji. Mara nyingi tunakuwa wamiliki,  kama wamiliki na tunasahau kuwa sisi ni walinzi tu” amesisitiza.

Kuwa na sauti moja.

Hiki ni kipindi kwa wakristo kuadhimisha kwa sauti moja lakini sio kipindi cha wakristo peke yake. Ni maadhimisho ambayo yako wazi na ujumbe wa kijamii na kiekolojia kwa sababu kinabainisha wazi juu ya  Kazi ya uumbaji na tunavyoishi katika maisha na tendo la kuwa kama  binadamu. Kwa maana hiyo Kardinali anahitimisha ujumbe wake akiwaalika kwamba  “ tuiishi kwa kusherehekea muungano katika familia ya uumbaji na ile familia ya wanadamu, hasa na masikini. https://www.vaticannews.va/en/vatican-city/news/2020-10/cardinal-tagle-season-of-creation-time-to-rediscover-our.htm

03 October 2020, 16:07